Covid-19: Serikali Ilinde wataalamu wetu kwa kuwapa likizo

Covid-19: Serikali Ilinde wataalamu wetu kwa kuwapa likizo

Kirchhoff

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
5,963
Reaction score
8,934
Amani Iwe Kwenu

Napenda kutoa wito kwa Serikali Yetu ya Awamu ya Tano Kuwapa Likizo Wataalamu wetu kada mbali mbali, hasa waliopo Dar Es Salaam, ili kuwaepusha na janga Hili la Corona Virus Desease 2019.

Nimewasiliana na Mzee mmoja mfanyakazi wa TBS, Ni mtaalamu aliyesomeshwa kwa gharama kubwa Nchi mbalimbali kwa kutumia Fedha zake na Kodi zetu, anasema bado wanaenda kazini Hadi wakati huu ambapo maambukizi yamezidi.

Huyo Ni mfano tuu na kwa umri wake akidaka covid ameenda na maji.

Tusijejikuta tumebaki bila Wataalamu baadae.

Kwa upande mwingine biashara zote zinazotegemea utalii zimedorora na kwa taarifa Kama Covid-19 itaisha mapema biashara zitaanza kuchangamka December.

Walimu wa Shule za Private hawana mshahara hivi Sasa wanataabika huku mtaani, wengine wanakimbilia vijijini. Kuna Mwalimu mmoja wa kike Jumamosi amehitaji ef 30 kwa malipo ya mwili... Dah Hali si Hali.

Bila mshahara sisi wafanyakazi wa kampuni binafsi hatutakufa kwa Corona Bali njaa.

Serikali ya Awamu ya Tano ondoeni Makato ya PAYE na kusamehe Kodi kwa kampuni Binafsi ili walao Tupate Mshahara nusu wa kutusogeza wakati huu.

Kwa upande mwingine wazazi tuendelee kuwaweka busy watoto kwa kazi za Sanaa na masomo mbali mbali.

Kwa Jina La Baba Na La Mwana Na La Roho Mtakatifu. Amina.

Tusifu Utatu Mtakatifu Sasa na Hata Milele.

Mungu Mtakatifu, Mtakatifu Mwenye Nguvu, Mtakatifu Unayeishi Milele, Utuhurumie sisi na dunia nzima.

Kwa Jina La Baba Na La Mwana Na La Roho Mtakatifu. Amina.
 
Ni swala la muda tu ndugu, subiri watalindwa kwa kupewa likizo bila malipo soon.
 
Nyie si ndio huwa mnawaambia vijana wajiajiri. Kumbe mnaogopa njaa nje ya ajira.

Nipatie namba ya huyo mwalimu wa kike nimsaidie hiyo elfu thelathini.

Kwa upande wa kudhibiti Corona, nchi hii imefeli vibaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna ulazima wa shughuli za maofisi kuendelea, wapunguze idadi ya watu au wawape wafanyakazi wengine likizo. Janga linaweza kupita na wataalamu wa kutosha, tuache mzaha....
 
Kama hamtaki kazi acheni, kuna vijana wengi wapo mtaani hawana ajira wapo tayari kufanya kazi kwenye mazingira yeyote

Sent using Jamii Forums mobile app
stress zitakuua kabla ya korona. kumsimesha mtaalamu kama mhasibu, kanali, mwalimu, daktari, padre ni gharama sana ya pesa na muda.

serikali kote duniani haziajiri tena bali zinahamishia watu kwenye uhitaji.

usishangae ukasikia tangazo walimu waliopita jkt wakaripo kwa Mkuu wa wilaya walipo haraka sana....wataenda

utasikia mwenye dip ya afya akaripoti haraka hospitali iliyokaribu nae akiwa na vyeti vyote......

ikiwa mbaya hali kiongozi atalia hadharani kama wa Italia kuomba huruma.

mataga na UV hamuoni mbele
 
Back
Top Bottom