Covid 19- watanzania tutakula kule tu tulipopeleka mboga

Luthertz

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2018
Posts
206
Reaction score
832
Nimekuwa na kawaida ya kujisomea habari za covid19 kwenye mataifa mbalimbali ndani ya na nje ya Afrika. Nimeona jinsi viongozi mbalimbali wamefanya kazi bega kwa bega na wataalam wa afya kwenye kukabiliana na janga ili. Serikali za nchi mbalimbali ndani na nje ya Africa, zimejitahidi kununua vifaa kwa ajili ya matabibu na kwa ajili ya kupima watu ambao wanahisi wana dalili za covid19.

Nimesoma pia na kuona jinsi wanasayansi ndani ya Uganda wamejaribu kutengeneza test kit ya kupima corona virus.

Jambo kubwa ambalo limenifurahisha ni kuona serikali nyingi ndani na nje ya Afrika zimeonesha kuthamini wataalamu wa afya. Na hii ni kwa manesi, madaktari, na wapimaji huko maabara. Jamii nyingi ndani na nje ya Afrika zimeonesha kuthamini sana mchango wa hawa wafanyakazi wa sekta ya afya.

Katika kusoma taarifa hizo za nje ya nchi yangu Tanzania, nikaamua kulinganisha na yanayoendelea hapa kwetu. Nikaongea pia na baadhi ya wafanyakazi kwenye hii sekta nyeti. Nikaona siyo tu kwamba hawapewi motisha lakini hata vifaa (PPE) hawana.Siyo kwamba hawana kabisa, vipo ila ni vichache sana.

Wataalam wetu wa afya wanajitahidi sana lakini wanakatishwa tamaa na viongozi wetu.

Nimeona bango kwenye internet ambapo msikiti flani nje ya nchi yetu ulikuwa ukiwashukuru health care workers kwenye ili janga la corona virus. Na hata makanisa yamefanya hivyo hivyo.

Hapa kwetu hawapewi any kind of motivation na mbaya zaidi wanapelekewa sampuli za mapapai, fenesi, mbuzi, oil ya magari n.k ili kuwajaribu.Wanajaribiwa kwa vifaa ambavyo hawakununua wao, havikuwa tested, na hata havifanyiwi service ya maana. Wanajaribiwa na vitu ambavyo hata waliotengeneza vifaa hawakuwahi fikiria kwamba ipo siku atatokea mwehu na kupeleka oil ya gari ikapimwe corona virus.

Sasa baada ya kuona wanayofanya majirani zetu, nchi nyingine za Afrika na nchi za mabeberu nikaona kwamba mimi mtanzania niache kuangalia wenzetu wana handle vipi ili janga, bali nimsikilize mtukufu Rais wetu mpendwa. Kwanini? Sababu tutakula pale tulipopeleka mboga. Sisi tunaye Rais na huyo ndiye tuliyenaye.
 
ni kweli kabisa ndio wa kwetu, hata awe je, so tuvumilie, mzazi akiwa mbaya hutakiwi kumwambia maana waweza kupata laana, so tuvumilie kwani hamna namna🤔😲😷
EXHdBnuWoAIakFM-2.jpg
 
Shida ya Tz siasa nyingi,visingizio vingi yaani wanaume watz hata wakishindwa kulala na wake zao wamefika stage ya kutafuta visingizio vya kila namna
 
Nimekuwa na kawaida ya kujisomea habari za covid19 kwenye mataifa mbalimbali ndani ya na nje ya Afrika. Nimeona jinsi viongozi mbalimbali wamefanya kazi bega kwa bega na wataalam wa afya kwenye kukabiliana na janga ili. Serikali za nchi mbalimbali ndani na nje ya Africa, zimejitahidi kununua vifaa kwa ajili ya matabibu na kwa ajili ya kupima watu ambao wanahisi wana dalili za covid19.

Nimesoma pia na kuona jinsi wanasayansi ndani ya Uganda wamejaribu kutengeneza test kit ya kupima corona virus.

Jambo kubwa ambalo limenifurahisha ni kuona serikali nyingi ndani na nje ya Afrika zimeonesha kuthamini wataalamu wa afya. Na hii ni kwa manesi, madaktari, na wapimaji huko maabara. Jamii nyingi ndani na nje ya Afrika zimeonesha kuthamini sana mchango wa hawa wafanyakazi wa sekta ya afya.

Katika kusoma taarifa hizo za nje ya nchi yangu Tanzania, nikaamua kulinganisha na yanayoendelea hapa kwetu. Nikaongea pia na baadhi ya wafanyakazi kwenye hii sekta nyeti. Nikaona siyo tu kwamba hawapewi motisha lakini hata vifaa (PPE) hawana.Siyo kwamba hawana kabisa, vipo ila ni vichache sana.

Wataalam wetu wa afya wanajitahidi sana lakini wanakatishwa tamaa na viongozi wetu.

Nimeona bango kwenye internet ambapo msikiti flani nje ya nchi yetu ulikuwa ukiwashukuru health care workers kwenye ili janga la corona virus. Na hata makanisa yamefanya hivyo hivyo.

Hapa kwetu hawapewi any kind of motivation na mbaya zaidi wanapelekewa sampuli za mapapai, fenesi, mbuzi, oil ya magari n.k ili kuwajaribu.Wanajaribiwa kwa vifaa ambavyo hawakununua wao, havikuwa tested, na hata havifanyiwi service ya maana. Wanajaribiwa na vitu ambavyo hata waliotengeneza vifaa hawakuwahi fikiria kwamba ipo siku atatokea mwehu na kupeleka oil ya gari ikapimwe corona virus.

Sasa baada ya kuona wanayofanya majirani zetu, nchi nyingine za Afrika na nchi za mabeberu nikaona kwamba mimi mtanzania niache kuangalia wenzetu wana handle vipi ili janga, bali nimsikilize mtukufu Rais wetu mpendwa. Kwanini? Sababu tutakula pale tulipopeleka mboga. Sisi tunaye Rais na huyo ndiye tuliyenaye.
Tanzania wenye fikra kama zako ni wachache. Unakuta watu huko mitaani wanafurahia watumishi waliosimamishwa kwa sababu ya kisanga hicho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom