COVID19 Tanzania: Wagonjwa wapya 35 waongezeka; idadi yafikia 88 (Aprili 15, 2020)

COVID19 Tanzania: Wagonjwa wapya 35 waongezeka; idadi yafikia 88 (Aprili 15, 2020)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
MWENENDO WA UGONJWA WA CORONA NCHINI

Wizara ya Afya inathibitisha uwepo wa wagonjwa wapya 29 wa COVID-19 Tanzania bara.

Hadi sasa Tanzania idadi ya Wagonjwa imefikia 88 na wote wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa wataalam afya.

Wagonjwa wapya leo ni 29 kwa bara na 6 kwa Zanzibar.

8C1FFD3B-3D17-4FD5-B1F0-DE34DB15F298.jpeg

IMG_1434.jpg
 
"Wizara ya Afya inatoa Taarifa ya Ongezeko la Wagonjwa 29 wa Corona Nchini hadi Kufikia 88 kutoka 53 tuliowatolea Taarifa ya awali. Wagonjwa Wapya wote ni Watanzania kati ya Hawa waliopo Dar es Salaam ni 26 na 2 Mwanza na Mmoja Yupo Kilimanjaro "
Waziri wa Afya @umwalimu Leo
 
Hali hii ni matokeo ya kuuchukulia poa huu ugonjwa(wengine hawataki kunawa,kukwepa mikusanyiko,n.k).

Kama tunafikiri tunaikwepa "lockdown", basi tujue tunaitafuta tena kwa speed ya mwanga.

Hali ikiwa mbaya, watawala hawatakubali kuonekana hawachukui hatua, bali watafanya maamuzi magumu na ikiwezekana hata kutangaza lockdown(total au partial lockdown).

Tuna hatari ya kuzipiku nchi zote zinazotuzunguka.

Ni wazi tukifanya mass community testing, matokeo yanaweza kutushangaza.

Kwenda Dar kwa sasa, ni kama kwenda Italy,Spain au US.
 
"Wizara ya Afya inatoa Taarifa ya Ongezeko la Wagonjwa 29 wa Corona Nchini hadi Kufikia 88 kutoka 53 tuliowatolea Taarifa ya awali. Wagonjwa Wapya wote ni Watanzania kati ya Hawa waliopo Dar es Salaam ni 26 na 2 Mwanza na Mmoja Yupo Kilimanjaro "
Waziri wa Afya @umwalimu Leo
Mungu tu ndie anaweza kutupitisha ktk hili janga ...
 
Taarifa hii ina ukweli kiasi gani? Nawaomba wana Jf tusiwe chanzo cha taharuki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa Mkuu nimeprove BBC idadi imepanda aswaaa ila kumbuka tuliandaliwa toka wiki iliyopita kwamba tumeingia kwenye wakati wa kuambukizana nje ya maambuzi kutoka nje.Ndio maana ata Serkali imeongeza muda wa wanafunzi na wanachuo kubaki nyumbani kwa muda usiojulikana.
 
Back
Top Bottom