COVID19 Tanzania: Wagonjwa wapya 35 waongezeka; idadi yafikia 88 (Aprili 15, 2020)

COVID19 Tanzania: Wagonjwa wapya 35 waongezeka; idadi yafikia 88 (Aprili 15, 2020)

Basi tuvae helmet kabisa. Point ya hizi mask ni hajulikani nani anao nani hana, hivyo lengo kuu ni muathirika asimuambukize mwingine. Droplets zinatokea mdomoni sio machoni. Ila unaweza vaa ukijisikia ila sio inakukinga wewe bali wewe ndio unawakinga wengine.
Kwani wewe huoni kuwakinga wengine ni utu pia?kwa hiyo daktari au nesi anapovaa anamkinga Mgonjwa
 
Nadhani weekend ya pasaka iliyopita tutaijutia sana kwa sababu ya mikusanyiko mikubwa ya watu kwenye nyumba za ibada. Local transmission kama zilipewa lift ya kusambaa kwa watu wengi zaidi,tujiandae kwa misiba mingi sana[emoji24][emoji24].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe umekremishwa na ukameza bila kutafakari,mathalani upo sokoni au kwenye daladala,je akitokea mtu anakohoa au anaongea na hajavaa mask na droplets zikatua ktk uso wako na pengine ana virus nini kitatokea?
Na vilevile mask inakusaidia ku shape tabia zetu za kushika pua,mdomo kwa kujisahsu.
Jiulize wahudumu wa afya wanaovaa hizo mask wao wanaumwa?
Usipojua kanuni za kuvaa mask..mask ni hatari kusambaza ugonjwa zaidi

Kabla ya kuvaa nawa mikomo au paka sanitizer

Ukishavaa hakikisha haupeleki mkono kuiweka sawa unless umenawa au kusanitize..sasa unakuta mtu anarekebisha na kupeleka mikono tena usoni mara kwa mara

Na pia zile disposable zinauzwa kwenye meza mjini watu wanashika shika wakiwa wanachagua..ikatokea mtu ana maambukizi akazishika shika zile mask ni hatari zaidi kuambukiza Corona

Kabla hujavua mask ni lazima unawe na kusanitize mikono yako ndo upeleke mikono uvue...na ukishavua kama ni disposable unapaswa kutupa sehemu salama ukiweka vibaya unaweza kuta watoto wamachezea au kauchukua kaivaa

Kama ni N95 inapaswa kusafishwa na sanitizer tena maana ile sio disposable.


Jikinge na wakinge na wengine



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watuache! Watakao kufa wafe na watakao pona wapone. Habari ya lock down ni upuuzi mtupu. Watu wengi watapukutika kwa njaa na uharifu utaongezeka kwa kiwango kikubwa Sana.

Huu ugonjwa wanaoambukizwa ni wengi ila wanaofariki ni wachache sana. Kila mtu ajilinde mwenyewe kwa kufuata maelekezo ya wataalam.

Si busara kuwalinda wenye uwezo wakifedha wasiambukizwe kwa kuji-lock down wote na kufanya maskini wengi wafe kwa njaa na uharifu.
 
Binafsi naona kukimblia kupost idadi ya wagonjwa kuongezeka kama, washabiki wa simba na yanga haitusaidii sana.

Natamani kuona watu wakipost strong and genuine points za namna ya kukabiliana nao,

Google huko na fuatilia kwenye medias ulete points za kuokoa watu na sio kukimbilia kuandika idadi iliyo ongezeka.

Hiyo ndio itafanya jf ionekane kisima cha elimu na kuitofautisha na wale wengine wa udaku...
 
Hii mijama ni zaidi ya mipumbavu mkuu, yani kenya tu hapo kila siku wanaongezeka pamoja na lockdown na watu wanalia njaa wanataka kutoka alafu jitu kisa lipo kwa shemeji yake linalilia lockdown

Sent using Jamii Forums mobile app
Walifanya lockdown too late, hata sisi tukifanya lockdown leo still utaona maambukiz yanaendelea.

Lockdown huwa nzuri kukiwa na wagonjwa 2 sahiz bora tuache tu maana wanaogundulika ni wale wagonjwa walio na virus wanadunda na kuambukiza tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom