Kamishna wa Operesheni Mafunzo wa Jeahi la Polisi CP Awadhi Juma Haji Leo Novemba 8,2024 amefunga mafunzo ya siku tano kwa Wakuu wa Polisi Wilaya zote Tanzania Bara na Visiwani. Mafunzo hayo yamefanyika katika Shule ya Polisi Tanzania Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Wakati akifunga Mafunzo hayo CP Awadhi amewataka Wakuu hao wa Polisi Wilaya waende kutumia elimu waliyoipata kuweka mipango kazi shirikishi ya kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024 ili uweze kufanyika katika mazingira ya amani,utulivu na usalama kulingana na imani na matarajio ya Watanzania.