Afrikasana
JF-Expert Member
- Oct 27, 2021
- 320
- 288
Kamanda wa kupambana na rushwa Hamduni Salum wasaidie sana watu wa Tanga.
Ofisi za TAKUKURU jiji la Tanga wamekua watu wasiotenda haki kwa kutofuata miiko ya kazi.
Wanakua watoa siri hata ukiwaeleza juu ya viongozi wala rushwa wao wanakua washanunuliwa na hao viongozi. Ukitokatu ofisi za TAKUKURU utashangaa kuambiwa na mtuhumiwa habari zote ulizopeleka huko nimeshazipewa.
Ingawa aliondolewa kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga tangia mwaka jana lakini bado hakuna jipya ameacha masalia yaliyokomaa hapo
TAKUKURU Tanga imekua wapowapotu,maeneo ya watu yanauzwa mara mbilimbili na watu wa ardhi lakini wakipewa taarifa hakuna linalofanyika.
Ukweli nikwamba matapeli wa ardhi bado wapo wanatishia watu mtaani kuuza maeneo yao,tena wanatembea na polisi eti ni watu wa mipango miji na TAKUKURU wamelala fofofo kama wamedungwa sindano kali za usingizi hawachunguzi wanasubiri wapelekewe taarifa na wakipelekewa wanaona imejitokeza fursa kwao na sio kazi
Kwabahati mbaya sana Tanga haijapata viongozi wanaotatua migogoro ya ardhi,kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Mh. Rais. Bado wanyonge wanaporwa haki zao na wahusika wanapeperushatu bendera kwenye magari.
Ili kujua kama Tanga rushwa imekomaa hata waandishi wa habari Tanga mjini hawapo na mkiwaita kutoka wilayani huko nakuwapa habari wakitoka hapo wanalala nazo mbeleee.
Kama wakija kwenye mikutano ya hadhara hata baada ya wananchi kuwaita kutoka maeneo mengine wanakuja na hao viongozi kwenye magari yao. Halafu angalia sasa kitakachoripotiwa
Eti Tanga ni jiji lakini hakuna mwandishi wa ITV, Star TV,TBC,Channel Ten nk katikati ya jiji badala yake eti Channel Ten wanaripoti zaidi Handeni na Lushoto kisa walishaona labda mazingira sio rafiki kwao ila harufu ya rushwa ipo.
Waletwe watumishi waadilifu kwani watanzania wanaoweza hiyo kazi niwengi.
Ni bora ofisi za TAKUKURU Tanga zikafungwa maana hazina tija kwa wananchi wa Tanga. Zipo kesi zenye zaidi ya mwaka lakini TAKUKURU hawayang'azi
CP Hamduni anza na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga akiondoka na watumishi wala rushwa walioachwa na yule aliyesimamishwa mwaka jana ndio labda ofisi itatenda haki.