Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu Jeshi la Polisi, CP, Suzan Kaganda amewataka Makamanda wa Polisi wa Usalama Barabarani wa Wilaya nchini (DTOs) kusimamia majukumu yao ipasavyo wakati wa kujaza fomu ya taarifa ya ajali za barabarani.
CP. Kaganda ametoa maelekezo hayo Jijini Arusha Juni 21, 2024, wakati akifungua kikao kazi cha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Makamanda hao kutoka wilaya za mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga kuhusu shughuli za Mfuko na umuhimu Jeshi la Polisi katika uchakataji madai ya fidia kwa mfanyakazi aliyepata ajali hususan za barabarani.
Huyu ilibidi awe IGP , lakini kwa vile ana vinasaba vya kutenda haki, high reasoning, professionalism hawawezi kumpa. Wanawapa watu wanaofikiri kwa kutumia misuri ya bunduki