Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Leo Septemba 26, 2025 – Umesainiwa mkataba wa ujenzi wa Hoteli ya Nyota Tano ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA Africa Region) itakayojengwa katika eneo la Njedengwa Jijini Dodoma.
Hafla ya utiaji saini imefanyika leo katika Ukumbi wa Spika, Bungeni Jijini Dodoma, na kuongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson.
Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, Dkt. Tulia amesema hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota tano itakayojengwa kwa kipindi cha miezi 22 inatarajiwa kuwa ya kwanza jijini Dodoma. Aidha, amebainisha kuwa wazo la kuanzishwa kwa mradi huo lilitokana na ushawishi wa Spika Mstaafu wa Bunge, Hayati Job Ndugai, mwaka 2019.