Crazy things you did in secondary school

Crazy things you did in secondary school

Jamani kuna watu wanaomkumbuka Mwalimu MPANDE wa Moshi Technical

Of all the people, Mpande alikuwa kiboko, hasa hasa usemaji wake wa ki-swangi akiwa uwanjani ana fanya football coaching

Nakumbuka kulikuwa na mchezaji mmoja anaitwa Nasib (akicheza kama centre forward, I think) Mpande alikuwa akimwambia

"Nasib DO NOT SMOKE THE BALL MINUS TO YUA FRIENDS!" akimaanisha "Nasib usivute mpira, toa pasi kwa wenzio"
 
wa Pugu sekondary mnamkumbuka mwalimu Nampanda,alikuwa anafundisha kiswahili,du huyu mwalimu kama hajatukana katik kipindi chake hana raha.

siku moja kuna jamaa alichelewa darasani na siku hiyo mwalimu wa zamu ni Nampanda,sasa Nampanda si akamdaka porini ikabidi ampe adhabu, jamaa akaona ameonewa ikabidi amwambie mie naenda kwa mkuu wa shule kukushtakia, ikawa wanakuja wote mpaka walipofika karibu na darasa letu karibu kabisa na kwakupandia ngazi kwenda kwa mkuu wa shule Nampaanda likamwambia yule mwanafunzi"unafikiri mie namuogopa mkuu wa shule ,mie namuheshimia tu, akinizibua nami namzibua pia, kwanza mie ndio Nampanda"madenti wote tukawa tunacheka na yule aliyetaka kwenda kwa master naye kicheko.

matokeo yake jamaa akwenda kwa master
 
Wale wa Makumira Sec. kule Arusha Mpoo!

Nawakumbuka marafiki zangu 1987 kina Robet Kasambala, Henry Shaushi, Ramadhani Macha, Shem Mwakayoka, Mushii, Peter Musuguri, Manambi Choka, Peter Mmari, Jeroo toka Nairobi na wengineo. Siku ya PURI na NYAMA, yaani Jumatano jioni, fujo ilikuwa inaanza saa 12 jioni.

Kuna siku vurugu ilizuka ktk PURI hadi sufuria kubwa ikakutwa master-parade! Nakumbuka sana unywaji "GONGO" kule kwa Mama Jack na MBEGE kwa Samora siku za weekend.

Du, kazi kwelikweli!
 
Heater inaunganishwa juu kwenye dari, inashushwa kwenye chandarua! Hiyo ni baada ya watu kupewa suspension kwa kukutwa na heater, suluhisho ni kuunganisha na kuhifadhi juu ya dari, kuchemshia kitandani!!
 
Wale wa Makumira Sec. kule Arusha Mpoo!
Nawakumbuka marafiki zangu 1987 kina Robet Kasambala, Henry Shaushi, Ramadhani Macha, Shem Mwakayoka, Mushii, Peter Musuguri, Manambi Choka, Peter Mmari, Jeroo toka Nairobi na wengineo. Siku ya PURI na NYAMA, yaani Jumatano jioni, fujo ilikuwa inaanza saa 12 jioni. Kuna siku vurugu ilizuka ktk PURI hadi sufuria kubwa ikakutwa master-parade! Nakumbuka sana unywaji "GONGO" kule kwa Mama Jack na MBEGE kwa Samora siku za weekend. Du, kazi kwelikweli!

Unamkumbuka Bob Msagati na mambo ya mchakamchaka wa asubuhi! maparachichi (siagi ya wanyonge), Pimbi wa kilara na mambo ya bye bye coner baada ya prep? mIdas touch nakumbuka ukiruka mangoma bado upo kinondoni?
 
I refused to engage in a sexual relationship with my headteacher that he decided to pin 'conjured' allegations and have me suspended from school. My mum came and kicked his butt.

He lost his job and I passed my finals with flying colors!

How about that for crazy?
 
Yaani mbavu zinauma kwa kicheko....mimi nilikuwa naona nina stori za kufurahisha za skonga, kumbe kuna watu wanazo kiboko....Kana Ka Nsungu nakuvulia tai kwa stori zako za kudandia ukuta.....
 
Unanikumbusha mbali mukubwa, enzi hizo sisi(MKWAWA HIGH SKUL) siku ya wali (JMOSI) unavaa nguo safi, unaenda kusomea dh huku bakuli kuuubwa lipo kwenye begi. Wengine wanawahi kupanga line saa tano wakati msosi tunagawiwa saa saba.
Tehe teheeeeeeeeeeeee ..........................


Lol! MKWAWA, walitutimua bwenini pale Lumumba east kwa kosa la kuunganisha umeme! Sitasahau kamwe!
 
...mpaka sasa siamini tulinusurikaje na STD na 'SLIM' kwa jinsi tulivyokuwa tunatoroka hostel ya father Kanuti kwenda kubanjuka mitaa ya 'shamba street', ...mji kasoro bahari!

Mungu Mkubwa, mwe!
 
Korogwe girls mpoooo???
Mnakumbuka enzi za maborbo ( Tanga Tech) vs Galanos .....ilikuwa mpambano kwelikweli!...
mabesti wetu walikuwa Galanos.... Tanga Tech nao wanashindania attention.... KG tunawasare tuu..maana chice for the boys was limited!

W of sub.
Ulikuwepo wakati wa mwalimu Ngoma?
 
Ha ha ha ha walimwengu mmenikumbusha mbali,asubuhi kibaridi mtoni watu hawaogi wala kunawa ni kupiga mswaki na wakati wa kunawa maji yanapigwa kofi(kibao) ndio mkono unapitishwa usoni au unachovya vidole viwili na kutoa tongotongo. Ukivamia msosi wa wanaume unalambwa mkono then mkono unasuguliwa kwenye mchanga ili usijirambe. Siku za mwanzoni form 1 aka njuka unapewa sh 5 na unaagizwa sigara 5, soda mbili, kiberiti na chenji urudishe.

Tumetoka mbali, kizazi kipya hiki hakijui vurugu zetu kwenye mabehewa ya TRL opps TRC enzi hizo, unapewa warrant, unaiuza na kusafiri unasafiri na wenzako kama kawaida. Mungu atusamehe ufisadi tuliuanzisha wenyewe. Tukimaliza thread hii tukumbushane majeshi mambo ya afande na mwendo wa kunyakua, push up "up juu, up juu", ya kaazime appitite kwa wenzio nk.
 
Watu wa Dar Tech mpo?

Namkumbuka sana mwalimu Ngole wa Engineering Science. Mi ndo nilikuwa mkali darasa zima.
 
Boss swallowing this with utmost doubts of the act plus taking it in mind Chit Chat was not there at the time this thread was Posted, I deem it right it is moved here from it's original Position. :shocked:


JF Daima.
 
niliwahi kujificha sehemu ya 'wazi' nikimtoroka mwalimu wa sijui mavazi...

Alikuja darasani kunisaka na nikawa nimehamia dawati la mbele kabisa, she was huge, na alikuwa anavaa hijab...sijui ndo zilimzuia asinione...hiyo siku nilijiona mshindi
 
kuna siku mwalimu mkuu alinichapa fimbo ya usoni kisa nimechelewa asubuh na barid la iringa si nikaenda kumwambia mama kazini kwake na damu na vipande vya fimbo uson moto aliouwasha pale highlands sec walinipa uhamisho siku hiyo hiyo.
 
namkumbuka yule tcha, alikua mtu wa stori sana....alimwambiaga dogo m1 wa o levo nakuchapa halafu ukaseme kwa mama yako. kwanza mwambie mama yako. "mimi ndio nampanda" watu 2kabaki midomo wazi. kipindi hko nakaa maendeleo 1
 
Na siku ya kula wali unavaa nguo za mapigano. Uji ukiwa hauna sukari na maharage yamejaa wadudu lakini mnagombania!

wakati wa kwenda kula chakula na kunywa uji ni vita mkuu..nakumbuka nilikua navaa nguo chafu pia nabeba jagi yaani nagombania uji hadi jagi linajaa nakunywa hadi unanishinda wakati wengine wamekosa..
 
Kwa shule za madume unaongelea wiki moja tu? Hata mwezi mzima mzee. Siku hiyo ni hatari. Ikibidi nguo zitaazimwa kwa washikaji town!

Ila ukiingia kwenye muziki ni kuwa mwangalifu ili blues ikipigwa usiwe single vinginevyo utaondoka ukimbini. Na mademu wasiotaka kucheza blues kibano ni halali yao. Kwanza kwa nini wamekuja disco kama hawataki kucheza. Ila blues yenyewe inavyochezwa du, ni hatari tupu. Hata hivyo disco ni mara moja kwa muhula so enjoying for 3 or more hrs was something you wouldn't want to miss hata kama una malaria!!

mzee D.C,
shule zote zinafanana au tumesoma shule moja?
 
Back
Top Bottom