Baba_Enock
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 7,076
- 2,457
Jamani kuna watu wanaomkumbuka Mwalimu MPANDE wa Moshi Technical
Wale wa Makumira Sec. kule Arusha Mpoo!
Nawakumbuka marafiki zangu 1987 kina Robet Kasambala, Henry Shaushi, Ramadhani Macha, Shem Mwakayoka, Mushii, Peter Musuguri, Manambi Choka, Peter Mmari, Jeroo toka Nairobi na wengineo. Siku ya PURI na NYAMA, yaani Jumatano jioni, fujo ilikuwa inaanza saa 12 jioni. Kuna siku vurugu ilizuka ktk PURI hadi sufuria kubwa ikakutwa master-parade! Nakumbuka sana unywaji "GONGO" kule kwa Mama Jack na MBEGE kwa Samora siku za weekend. Du, kazi kwelikweli!
Unanikumbusha mbali mukubwa, enzi hizo sisi(MKWAWA HIGH SKUL) siku ya wali (JMOSI) unavaa nguo safi, unaenda kusomea dh huku bakuli kuuubwa lipo kwenye begi. Wengine wanawahi kupanga line saa tano wakati msosi tunagawiwa saa saba.
Tehe teheeeeeeeeeeeee ..........................
Korogwe girls mpoooo???
Mnakumbuka enzi za maborbo ( Tanga Tech) vs Galanos .....ilikuwa mpambano kwelikweli!...
mabesti wetu walikuwa Galanos.... Tanga Tech nao wanashindania attention.... KG tunawasare tuu..maana chice for the boys was limited!
Watu wa Dar Tech mpo?
Namkumbuka sana mwalimu Ngole wa Engineering Science. Mi ndo nilikuwa mkali darasa zima.
Na siku ya kula wali unavaa nguo za mapigano. Uji ukiwa hauna sukari na maharage yamejaa wadudu lakini mnagombania!
Kwa shule za madume unaongelea wiki moja tu? Hata mwezi mzima mzee. Siku hiyo ni hatari. Ikibidi nguo zitaazimwa kwa washikaji town!
Ila ukiingia kwenye muziki ni kuwa mwangalifu ili blues ikipigwa usiwe single vinginevyo utaondoka ukimbini. Na mademu wasiotaka kucheza blues kibano ni halali yao. Kwanza kwa nini wamekuja disco kama hawataki kucheza. Ila blues yenyewe inavyochezwa du, ni hatari tupu. Hata hivyo disco ni mara moja kwa muhula so enjoying for 3 or more hrs was something you wouldn't want to miss hata kama una malaria!!