Crazy things you did in secondary school

Crazy things you did in secondary school

~Hata hizo barua unazojiandikia mwenyewe, hununui stamp hata siku moja! Stamp inafutwa muhuri na kutumika mara kadhaa! I think Shirika la Posta na Simu (jina la enzi hizo) halikupata chochote kwa barua kutoka mashuleni!

nilikuwa nasugua ule muhuri kwenye nywele vizury kabsa na barua zinaenda kama kawa..... enzi za RUKSA HIZO
 
Siku ya Graduation pale Mazengo Sec mwaka 1985, kiongozi wa sherehe alikuwa mshikaji wangu Kasanga. Basi nilimfuata na Kisadolini changu na akanijazia Pilau. Pilau la Mazengo miaka hiyo lilikuwa kali sana. Kwa wenyeji wa Dodoma watakuwa wanamkumbuka Mzee Mapilau na yale Mapipa yake (SHABA). Nilikula siku hiyo hadi nikawa siwezi kuhema. Jamaa walishangaa kuwa mbona hawaoni tumbo kutokea. Basi kutoka siku hiyo nikajulikana kuwa nina tumbo kama la Mamba, linafutuka pembeni.......
Upuuzi wa Mazengo ilikuwa ni chooni. Utakuta mtu anapita koridoni na karatasi yake anaipekecha ili ilainike.... "pyeke pyeke pyeke..." na akitoka huko basi anapita kwenye ule mti nyuma ya bweni la Mwongozo na kujipigapiga na mtawi. Hii ilikuwa inasaidia kuuwa ile perfume uliyoikwaa kule NYUMBA KUBWA. Ule mti ulikuwa na harufu moja kali sana na ukitoka hapo unanukia freshi. Mabinti wa Msalato, mlivumiliaje ile harufu??

Hakuna hata kilichobadilika toka miaka hiyo mpk nami nilipomaliza zengo(ni mmoja wa tuliokuwa wa mwisho kabisa kumaliza toka mazengo mpk st.john unvst)..harufu ya beach haina mfanowe..ililazimu kuvua nguo zote ndo ukapate huduma..daaa
 
Nakumbuka ilikua j2 na j3 ilikua ni siku ya usafi,na mimi nilikua sijafua shati nilicho kifanya nilikata kora nikalifua nikalifaa na sweta kesho tulipokua ktk ukaguzi kilicho fuata ni balaah tupu
 
ilikuwa saa mbili asubuhi mwaka 1989 pale Tambaza boys, basi likatushusha muhimbili enzi hizo UDA, Tukawa kundi kubwa tunaelekea shule, kufika viwanja vya muhimbili walimu na wanafunzi wengine wako mstalini, mwalimu mmoja mnoko pamoja s.master wakatusimamisha wote wakitutenganisha na waliowahi.

tukaambiwa chuchuma chini anzeni kichurachura kuelekea shule ya msingi muhimbili then mnarudi mstalini Tambaza ukifika unapata bakora unaelekea class.

Sasa kilichotokea wakati tunaruka kichurachura jamaa mmoja akasema tukifika muhimbili primary hakuna kurudi nyuma kwenye bakora tunasimama wote na kuaanza mbio kulelekea muhimbili hospital,diamond jubilee na kwengineko town kama faya.

walimu walibaki midomo waza tukazurura posta ,library hasi kesho tukaje shule walimu hawamjui hata mmoja.

eeeh eeeh ilikuwa kali maanake,

Ha haa hii Kali Kuliko
 
Yaani Sikonge umenichekesha. Sasa wakati mnakuja buggy msalato, behind the dining kuna jiko and behind it kuna vyoo vya chodisa. Hali ilikuwa vile vile.

Uzuri tulikuwa hatusikii harufu ya toilet manake mlikuwa mnanuka jasho na pombe lol
Siku ya Graduation pale Mazengo Sec mwaka 1985, kiongozi wa sherehe alikuwa mshikaji wangu Kasanga. Basi nilimfuata na Kisadolini changu na akanijazia Pilau. Pilau la Mazengo miaka hiyo lilikuwa kali sana. Kwa wenyeji wa Dodoma watakuwa wanamkumbuka Mzee Mapilau na yale Mapipa yake (SHABA). Nilikula siku hiyo hadi nikawa siwezi kuhema. Jamaa walishangaa kuwa mbona hawaoni tumbo kutokea. Basi kutoka siku hiyo nikajulikana kuwa nina tumbo kama la Mamba, linafutuka pembeni.......
Upuuzi wa Mazengo ilikuwa ni chooni. Utakuta mtu anapita koridoni na karatasi yake anaipekecha ili ilainike.... "pyeke pyeke pyeke..." na akitoka huko basi anapita kwenye ule mti nyuma ya bweni la Mwongozo na kujipigapiga na mtawi. Hii ilikuwa inasaidia kuuwa ile perfume uliyoikwaa kule NYUMBA KUBWA. Ule mti ulikuwa na harufu moja kali sana na ukitoka hapo unanukia freshi. Mabinti wa Msalato, mlivumiliaje ile harufu??
 
Last edited by a moderator:
Hahahahaa, mambo ya MSAZENGO wewe wacha kabisa. Natamani kuwapa Wa-Anglican eneo jingine na pale kuirudisha Mazengo yangu. Nilipita mwaka huu na kupaona, eti Chuo Kikuu, too sad. Msalato itabidi niende siku moja nipaone tena.

Ila tulikuwa washamba, yaani hata kuweka kamba za kukaushia nguo, ni shida. Yaani shule inakosa waya za kuweka ili wanafunzi wakaushe nguo? Vitu vingine ni U-Africa hadi basi tu.

800_800imagesstorySWTBusiness1104PICTURE2.jpg

Yaani Sikonge umenichekesha. Sasa wakati mnakuja buggy msalato, behind the dining kuna jiko and behind it kuna vyoo vya chodisa. Hali ilikuwa vile vile.

Uzuri tulikuwa hatusikii harufu ya toilet manake mlikuwa mnanuka jasho na pombe lol
 
Hahaha msalato pamechakaa kweli. Afadhali mazengo pamekuwa chuo patakuwa maintained.

Nyie uongozi wenu haukuwa na vision bwana. Msalato kulikuwa na kamba zenye 6 lines na urefu wa kutosha kwa kila block. Tena kulikuwa na laundry places.

Zina masinki kwa ajili ya kufulia na mabomba. Na upande kuna platform za kupasia na sockets. Joyce Mgana was good kiukweli.

Aliruhusu kuweka nywele dawa kwi kwi kwi
Hahahahaa, mambo ya MSAZENGO wewe wacha kabisa. Natamani kuwapa Wa-Anglican eneo jingine na pale kuirudisha Mazengo yangu. Nilipita mwaka huu na kupaona, eti Chuo Kikuu, too sad. Msalato itabidi niende siku moja nipaone tena.

Ila tulikuwa washamba, yaani hata kuweka kamba za kukaushia nguo, ni shida. Yaani shule inakosa waya za kuweka ili wanafunzi wakaushe nguo? Vitu vingine ni U-Africa hadi basi tu.

800_800imagesstorySWTBusiness1104PICTURE2.jpg
 
Hahaha msalato pamechakaa kweli. Afadhali mazengo pamekuwa chuo patakuwa maintained.

Nyie uongozi wenu haukuwa na vision bwana. Msalato kulikuwa na kamba zenye 6 lines na urefu wa kutosha kwa kila block. Tena kulikuwa na laundry places. Zina masinki kwa ajili ya kufulia na mabomba. Na upande kuna platform za kupasia na sockets. Joyce Mgana was good kiukweli. Aliruhusu kuweka nywele dawa kwi kwi kwi

hivi shule za girls nayo wanakuwaga na makundi(kuwa na majina yao na chata),sisi tulishindikana shuleni kwetu enzi hizo kupiga chata zetu,uzuri tuliowakuta walikuwa na vikundi vyao, sisi tulikuwa kundi la watu kama 15, mguse mmoja uone mziki, halafu wengi wanakuwaga wahuni na walioshindikana either wavuta ganja au walevi,sisi tulijitenga na wengine kulikuwa na kacumba kadogo cha watu 16 ndani hostel,tulijichagua na kujipnga wenyewe.
 
Me nakumbuka tulifukuzwa shule baada ya kumteka dogo mmoja wa form 3 kisha tukampiga na kumvunja miguu yote, kisa, alikuwa anajiona mzuri sana shule nzima.
Enzi hizo niko form 1 term ya pili.

Nasikia huyo dada now yuko pale Bandari, ila anachechemea mguu wa kushoto naana ulishindikana kunyoosheka fresh.
Mungu nisamehe.....ulikuwa utoto tu.
 
duuuuuh.....we ulikuwa noma.....lkn mdo utoto.........
 
Marangu sec jamani ni hatari siku ya wali kula mtu atajua maana kengele ikipigwa ni ushahudi tu kila mtu yupo kwa foleni. Zaidi ni st magret wakija kwenye disco marangu sec mmmmmmmm

Hawa St. Margareth pamoja na kwamba tulikua twakutana nao sana viunga vya Samanga, Rauya na Marangu Mtoni yote siku za Ijumaa na Jumapili (watu wakienda kuabudu) bado siku za debate liambatanalo na debe ilikua patashika haswa.
 
nakumbuka kidato cha tano pale saint maurus nimetoka kutoa speech brother kanuti akagundua nimevaaa soksi tofauti halafu zilikua chafu akaniamrisha nivue pale assemble then niwaoneshe wanafunzi wenzangu ilikua mwaka2008
 
nakumbuka mwaka 2005 wkt npo kidato cha 4 ktk shule inaitwa Bismarck ipo mkoan Mwanza nlizushiwaga natembea na mwalim wang wa masomo ya biashara eti kisa kila pepa ya Book keeping na Commerce nlikua naongoza mim, pia nakumbuka mwaka 2007 wkt npo kidato cha 6 ktk shule ya wavulana ya Azania nlimpgaga ngum dereva wa daladala ya Temeke/Muhimbil baada ya mwanafunz wa kidato cha kwanza kusukumwa na kufarik, yan iyo fujo yake haikua ndogo kwa maana wanafunz wa Azania 2lizagaa ktk vitua shaz kufanya fujo
 
naikumbuka hiii
 
Pale Shirati sekondari miaka ya 1973 na 1976 Siku ya wali na nyama nilivyokuwa nakuwa wa kwanza mstari wa kuchukua chakula then kwa dakika tatu nimesharudi kuchukua kingine kama sijala vile.
Sie tulikuwa tunapanga mstari kugawiwa chakula.

73' au 93'?
aisee..sina hata dalili ya kuzaliwa
 
Back
Top Bottom