Nakumbuka nipo AZANIA SEC ,,
kipindi hicho asubuhi tunapewa SKONS NA CHAI....
basi ikifika SAA NNE ,,tunajisogeza canteen kwa ajili ya kupata skons,,
monitor anakwenda dirishani anatoa ID anakabidhiwa fuko la mikate ,
nakumbuka ilikuwa scons flani za njano njano hivi...basi kichekesho ni kwamba,,
darasa zima lilikuwa na wanafunzi 37 hivi..
lakini Mara nyingi huwa halitimii wote,,,
tunakuwa wengine hawana muda wa kusubiri scons,,
muda wa break wanakimbilia nje kwenye mihogo ya kukaanga na juice za ukwaju..
kwahyo sometimes tunakuwa wanafunzi kumi au si zaidi ya 15... Lakini scons tunapewa idadi ile ile 37 hata kama tupo wawili ,,,
Sasa basi yule monitor ataanza kugawa scons,,
kama watu watatu wanne hivi,,
halafu fujo zinaanza kugombea ule mfuko wa scons,,
yaani vumbi tupu..
sasa ukiuliza chanzo cha fujo ni nn? wanasema scons za kupewa bila kugombea zinakuwa sio tamu,,
duu..basi baada ya fujo zile za kugombea scons kwisha,,
ndy baadhi ya wanafunzi wanapata head lines za kwenda kuandika ubaoni,,
mfano amng'ata mwenzie sikio wakigombea scons,
,halafu wanaacha hivyo ubaoni,,
basi mwalimu akija anaona yaliyoandikwa pale ubaoni ,,
na baadhi ya wanafunzi wamejaa vumbi tupu.
tena ule udongo mwekundu..
basi darasa zima ilnakuwa ni vicheko,,
kumcheka yule aliyekosa,,au aliyechafuka na vumbi wakati wa kugombea scons..
Dah,,,aisee shule ni kipindi cha mpito.....
na siku tusipogombea mikate wanasema ya le sio mitamu kabisaa...