Rum six mido pale Soweto (Ujamaa) palikuwa si pakwenda kwa wale nyoya (wenye baa nyekundu moja begani - fomu wani!!) wadau nadhani mtakuwa mnakumbuka kwamba Ujamaa ni bweni lililokuwa likiongoza kwa kutrotisha (kuwasumbua) fom nyonya miaka yote! Ikiwa pamoja na kumwagiwa bichi (maji machafu), kupigwa chaga usiku au kuingizwa lokani).
Lakini kilichonichekesha zaidi ni kumkumbuka UNYAMA UNYAMA (ticha wa mota vehicle) aliyekuja Soweto kuamsha watu alfajiri siku moja akiwa mwalimu wa zamu, halafu akasikia sauti ikitokea floor ya juu kabisa ikimwambia "Unakuja kutumbusua asubuhi yote hii kwa sababu nyumbani kwako hapakaliki, wakati wenzako wanachagua wake wazuri wa kuoa we ukachagua kipori, matokeo yake unashindwa hata kulala nyumbani kwako" UNYAMA UNYAMA akajibu "Wewe unaeongea hivyo kama kweli ni mwanaume na unajua wanawake wazuri kuliko mimi shuka hapa chini tuonane"
Kituko kilikuwa kitamu yaani mpaka ilibidi jamaa waigize siku graduu!!
Ebwana nimekumbuka mambo mengi sana,
Big up sana kwa mameni KABOTA, MAGERE, MSASA, KATUNZI, mzushi TETE, KAMEME, mchungaji ISHENGOMA.