CRDB Bank jirekebisheni, mikopo ni jambo la dharura

CRDB Bank jirekebisheni, mikopo ni jambo la dharura

Faru dume

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2012
Posts
471
Reaction score
116
Habari wakuu,

Mimi kama mdau wa bank hii ya CRDB naomba nitoe dukuduku langu na kama yupo mfanyakazi au mtendaji wao tafadhari rekebisheni matatizo yenu, haiwezekani process ya mkopo ikachukua wiki tatu mpaka mwezi na Bado fedha/mkopo hamtoi, hivi hamjui mkopo ni kitu cha dharura?

Naombeni kama mmeshindwa kutoa huduma hii kwa haraka basi muwe wa wazi tu tusipotezeane muda.

Naomba kuwasilisha.
 
CRDBni bank ya ovyo sana kwa wafanyabiashara wadogo na wakati. Mikopo yao kwa kiasi kikubwa inawalenga wafanyakazi hasa wa serikalinj na mashirika makubwa.
Hata wafanyakazi siku ni majanga matupu boss
 
CRDBni bank ya ovyo sana kwa wafanyabiashara wadogo na wakati. Mikopo yao kwa kiasi kikubwa inawalenga wafanyakazi hasa wa serikalinj na mashirika makubwa.
Kazi ya kukopesha ni kazi ngumu na inahitaji umakini sana. Huwezi kumkopesha kila mtu mwenye shida. Kinachangaliwa kwenye kukopa ni uwezo wa mkopaji kurudisha. Wabongo ulikiwalegezea baada ya mwaka utakuwa umefunga benki hata kama ilikuwa kubwa kiasi gani. Tuseme kwa ujumla kinachofanya kukopa Tanzania kuwe kugumu ni uhakika wa wakopaji kurudisha walichokopa.
 
Japo mimi mwenyewe nahitaji iwe kwa haraka,lakini kwa tabia za Watanzania wote tena,umeongea kila kitu mkuu,umemaliza,hii tred iishie hapo
 
Hili nalo ni tatizo.watu wanapenda kukopa.kwenye kulipa inakuwa ugomvi.
 
Kukopa hakukwepeki. Lakini mikopo yenye riba kubwa ambayo haina mbadala mwingine huwa shida kwenye marejesho. Naamini watanzania wengi sio wabaya wa kutoa marejesho, tatizo ni riba ambazo hazirejesheki.

Hili nalo ni tatizo.watu wanapenda kukopa.kwenye kulipa inakuwa ugomvi.
 
Si sahihi. Haya yanasemwa siku zote kwamba watanzania hawapendi kulipa mkopo, lakini si kweli. Kuna mambo mengi yanatesa mkopaji kama riba kubwa, kutokupewa elimu wazi ya mkopo wanaochukua n.k. Wengi hugundua wamebeba mzigo wanapoanza kupeleka marejesho.

Japo mimi mwenyewe nahitaji iwe kwa haraka,lakini kwa tabia za Watanzania wote tena,umeongea kila kitu mkuu,umemaliza,hii tred iishie hapo
 
Kuna ile shida ya mtandao isiyoishaga. [emoji3]
 
Baadhi ya matawi wana mambo ya ajabu ajabu kuna ka bank officer flani nlikua natoa pesa nyingi ila akaunti sijafungulia tawi hilo, akaniambia ngoja tuwatumie email ukipofungulia account nikamwambia sawa. baada ya muda ananiambia haifahamiki watajibu saa ngapi au lini.. wee nikamwambia usiniletee utopolo hapa email inachukua siku??? Mbona baada ya 2hrs nilizama bulk cash kuchukua mpunga uko tayari!
 
Kuna rafiki yangu Ni mtumishi aliporocess mkopo unakaribia mwezi sasa hajapata mkopo.....
 
Si sahihi. Haya yanasemwa siku zote kwamba watanzania hawapendi kulipa mkopo, lakini si kweli. Kuna mambo mengi yanatesa mkopaji kama riba kubwa, kutokupewa elimu wazi ya mkopo wanaochukua n.k. Wengi hugundua wamebeba mzigo wanapoanza kupeleka marejesho.
Yaani ilivyo tu ndugu Watanzania wengi si walipaji wa madeni yawayo yoyote. Ndio maana vikundi vingi vya kukopeshana vinakufa. Ukitaka kujua watanzania 90% sio walipaji wazuri wa madeni,uwe na duka labda la vifaa vya magari hivi, hata yule usiemdhania kwamba anaweza akawa msumbufu atakusumbua mbayaa. Hata kama ana kazi au biashara nzuri tu inayomuingizia hela,lakini wakishakopa akimaliza ile shida yake siku hiyo hataki kabisa kulipa,mtakusukumana sana. Watanzania wengi akimaliza shida yake tu,kulipa anaona tabu kabisa. Na ukitaka kulijua zaidi fuatilia wale wanaokopesha mitaani kwa riba wale unapoenda kukopa aither uache gari au wanashika nyumba,viwanja n.k kulingana na thamani ya pesa unayokopa na inakuwa kwa makubariano ya muda fulani. Wakopaji wengi wanafirisiwa na wakopeshaji. Na sababu kubwa ya kufirisiwa ni ksbb moja Watanzania sio walipaj. Mbili ujanja janja mwingi. Tatu Watanzania wengi wanapoenda kukopa anakuwa hana udhoefu au adea nzuri au hajui kabisa kitu anachoenda kuzalishia hiyo hela anayoenda kukopa. Let say amesikia tu kilimo cha matikiti kwa mtu mmoja,amempa tu hesabu ya kwenye makaratasi kwamba yanalipa,kesho huyo mbio kwenda kukopa. Ndio maana bank unapoenda kukopa lazima wakufuatilie wajiridhishe je kweli unaweza kurejesha hiyo hela. Bank wenyewe huwa wanajisikia vibaya kufikia hatua ya kuuza zamana ya mteja mfano nyumba,ndio maana mpaka kufikia hatua ya kuuza nyumba yako lazima waende na wewe taratibu,wakiona unaendelea kulipa hata kwa kidogo kidogo tofauti na makubariano bado wanaendelea kukuvumilia. Mwisho nikuambie tu Watanzania asilimia kubwa sio walipaji
 
CRDB UKITAKA MKOPO WA UJASIRIAMALI,
WEKA HADI MIEZI MITATU.
KUJA KUUPATA HADI HUNA HAMU NAO,
UNAJIKUTA USHATENGENEZA TATIZO KUBWA LA KUTATUA KWA MILION 10 WAKTI ULIKUW UNAHITAJI mil 3 tu.
 
Back
Top Bottom