CRDB Bank jirekebisheni, mikopo ni jambo la dharura

Mimi nilikaaga wiki 3 pia ndo nikapata mkopo Yan ukiaza kufuatilia mkopo Crdb Bora ya anayefuatila Kutambulisho Cha Nida au control namba Tanesco lazima utakubali mziki
 

Mhanga hapa, its May 2022, and 45 Days zimepita tangu nianze mchakato wa kufatilia mkopo wa biashara, niko Morogoro, yaani 45 Days tangu siku ambayo wamekuja kunitembelea Ofisi na Dhamana na kwa upande wangu nimefanya process kwa uharaka sana, i.e kupeleka viambatanishi vyote pamoja na kulipia gharama zote za awali (Bima, Ardhi, Official Search etc, keep in mind step hii ni zaidi ya wiki mbili sasa nimeshamaliza) Kupewa form tu za mkataba ilikua mtihani mzito. Pasua kichwa hawa jamaa
 
Mimi nilikaaga wiki 3 pia ndo nikapata mkopo Yan ukiaza kufuatilia mkopo Crdb Bora ya anayefuatila Kutambulisho Cha Nida au control namba Tanesco lazima utakubali mziki

Wiki tatu kutoka Hatua ipi?? Ya kulipia kila kitu gharama za awali na kurudisha form?? Au mchakato mwanzo mpaka mwisho?
 
Wale maana yake wanakuambia usikope
 
Yaani kuna watu wanaenda kukopa sehemu wanajua kabisa kuwa hawatolipa
 
Umeongea vizuri sana lakini uhalisia hauko hivyo hata ndugu yangu
Benki hawakopeshi wazo kwa beginners
Benki ya biashara sio ya kilimo cha kusikia matikiti yanalipa

Walengwa wa mabenki ni wafanya biashara
Watumishi wa secta za umma na binafsi wenye sifa za kukopesheka

Mfanyabiashara ili akopesheke benki wao hawahitaji aseme kwamba mimi naweza kuwalipa mkinikopesha biashara yenyewe itajiongelea mfano Analipaje kodi za serikali au miamala yake kwenye account zake.

Mtumishi yeye ndio mlipaji mzuri hapo kwa sababu watakata kiasi walichokubaliana kwenye msharaha wake pasipo kuchelewa wala kutaafutana


Makundi yote ya niliyoyataja hapa ndio mojawapo ya watu waaminifu kwenye ulipaji wa madeni kumbuka wewe huwezi tu kwenda bank na kuomba mkopo ukiwa huna kipato chochote cha uhakika kwa waonavyo wao

Hapo sijasemea wenye dhamana pekee bila biashara


Benki wanakuwa hawana haja ya kuchelewesha mikopo wa wateja waliowaamini kuwaruhusu waanze process za kuwapatia mikopo.
 
Hawa watu wanazingua sana kumbe! Kuna mwanangu kajaza mafomi kibao na kusainisha kila sehema. Hajapata pesa na gar inazidi kukaa bandarini
 
Wapumbavu hao crdb
Nmb within 24 hrs unapewa chako.
 
Hii ya kutokulipa kwa Watanzania ni kama hulka. Achilia mbali mikopo, mtanzania hata akiazima chaja tu ya simu HAIRUDISHI KAMWE mpaka wewe uliemuazima uanze kuifuatilia na saa nyingine uzungushwe wee..!
 
CRDBni bank ya ovyo sana kwa wafanyabiashara wadogo na wakati. Mikopo yao kwa kiasi kikubwa inawalenga wafanyakazi hasa wa serikalinj na mashirika makubwa.
Daaaah! Ni kweli nina jamaa yangu yupo mgodini huko Tarime inaelekea mwezi sasa mkopo hawampi wanamzungusha mpaka ameomba asitishe aende NMB sijui ndio tabia ya bank au ya watoa huduma wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…