CRDB Bank na makato ya matumizi ya kadi za ATM

Bora kufunga akaunti maana ni matapeli.

Wanaposema mfadhili mbona wafadhili hawarejeshewi fadhila? Ina maana walikopa?

Mkataba wa ATM na Mteja hakuna kipengele cha makato ya 15k kwa mwaka.

Matokeo ya kulipana mishahara mikubwa bila ubunifu wa vyanzo
 
Mimi nilitumiwa laki 2 kwenye NMB account halafu nikaacha kuitoa kama wiki 2 hivi. Kuja kuangalia nakuta laki na ishirini imekatwa. Yaani niliambulia Tshs. 80,000/= tu. Niliwalaani sana NMB na nikaona ni wezi kabisa. Majizi makubwa
Duh
Lakini mimi nilishaachana na NMB kitaaambo
 
Mimi nilitumiwa laki 2 kwenye NMB account halafu nikaacha kuitoa kama wiki 2 hivi. Kuja kuangalia nakuta laki na ishirini imekatwa. Yaani niliambulia Tshs. 80,000/= tu. Niliwalaani sana NMB na nikaona ni wezi kabisa. Majizi makubwa
Bro hiki kitu kinawezekana kikatokea ila ukifatilia utajua imetokaje au mkopo wamekata lakini haiwezekani wachukue tu kirahisi hivyo watu wanatunza USD miaka nenda rudi mkuu hizo Bank na hazichukuliwi kirahisi wewe wiki mbili tu?
 
Yaani uko serious kabisa uhame benki kisa Elfu 15?
Jamaa anajichanganya tu, benki takribani 20,000 wamepewa ruhusa ya kutengeneza hizo kadi kwa majina ya benki zao, na kwa bahadhi ya benki, mmiliki wa kadi ni lazima alipie ada ya kila mwaka. Hapo atakuwa anawaonea tu CRDB. Akumbuke kuwa VISA card ni kampuni yenye wana hisa na kadi hizo unaweza kuzitumia katika benki yoyote mwanachama katika nchi yoyote.
 
Hata Nmb wanakaa hz pesa kwenye card kuanzia ile ya personal Account
 
Benki karibu zote zinafanya hivyo, kumbuka hizo kadi mabenki wamepewa ruhusa ya kuzitengeneza kwa majina ya benki zao. Lakini mmiliki yupo na ni kampuni yenye wanahisa kabisa, annual fee ni kawaida.
 
Yaani uko serious kabisa uhame benki kisa Elfu 15?
Sometimes tunafanya vitu kwa kutokujua.
Sema crdb mimi siwaelewi. Kuna muda naweza kupokea transfer labda ya dollar 190 wakapita na laki nzima nikashangaa kwenye akaunti kuna 380000 ukiwauliza jibu wanalokupa wao ndiyo ela waliyoipokea.
Muda mwingine unapokea labda dollar 3000 unaikuta ela yote bila hata shilingu 10 kukatwa. Yani siwaelewi.
Pia kuna mambo tunafanya bila kujua.
Mimi nina akaunti mbili so nna kadi 2.
Akaunti ya kwanza ni ya dollar ya federal commumity bank ya US na ya pili ya crdb.
Sasa bwana mimi sina sim banking eti kisa niliona airtel money wana huduma ambapo unaweza kuhamisha pesa toka kadi kuja airtel money as long as ni mastercard, visa au union pay.
Nikihamisha kutoka kadi ya federal bank hawakati ela nyingi ni just 5% ya kiasi uchahamisha na wanakwambia wao airtel. Sasa nikitaka nunua vivocha umeme nafamya hvyo.
Sasa hii tabia nikaihamishia crdb, kumbe mbali 5% ya gharama za kuhamisha nao crdb wanakulima 12000 haijalisha uwe ulihamisha 1000, au 500 au 1000000.
Mimi nilikiwa sijashtuka kwasababu sina tabia ya kutazama bank statement.
Kuna siki nimenunua vocha za buku 2000 kama mara 6 au zaidi.
Baada ya muda nmeenda atm naona .bona salio silielewi elewi. nikawapigia huduma kwa wateja maelezo sijaelewa.
Nikawatumia email kuwaomba bank statement. Mzee naona 12000 makato yamefuatana.
Nikawapigia kuwauliza ndipo wakanieleza.
Nilikoma tangu siku hiyo kukurupukia vitu. Na iwapp nisingefatanisha hayo manunuzi mpaka leo nisingejua maana nmekuwa nikitumia hyo njia zaidi ya mwaka labda mara 1 kwa mwez au miezi miwili so wakikata si notice.
Hapo shida sio wao bali ilikuwa mimi
 
Hata sisi tunaotumia NMB Master Card tunakatwa 10,000 kila mwaka.
 
Mkuu, labda hamkuelewana lugha tu. Visa card ziko chini ya Visa International Services Association, hii imewaruhusu mabenki duniani kote kutengeneza hizo card. Kwenye mabenki mengi mtumiaji wa kadi anapaswa kulipa ada ya kila mwaka.
 
Hizo bank wanacheza na exchange rates, most of the time wanakupa the lowest rates available in the market ili wamaxikise profit coz na wao huwa wanauza hiyo dola. Na pia kuna bank transfer charges ukikombine hapo lazima upate maumivu.
 
Hizo bank wanacheza na exchange rates, most of the time wanakupa the lowest rates available in the market ili wamaxikise profit coz na wao huwa wanauza hiyo dola. Na pia kuna bank transfer charges ukikombine hapo lazima upate maumivu.
Hata kama mkuu yani $190 wakupe 380000. Mimi siwaelewi kabisa. Halafu 3000 ukupe yani imeingia pesa ambayo ukipga unapata rate 2500. Na hii si mara moja na sijawahi kupata maelezo ya kueleweka kwa sababu hata bankstatement inaonyesha ela iliingia kwa akaunti in tshs haionyeshi ilikuwa dollar ikawa converted to tshs kwa rate ya kiasi gani.
So hata customer care wala anakuwa hajui akiangalia yeye anaona tshs tu
 
Kwa mwaka heri yako wewe maana ni 15K malipo ya card plus 24K Makato yako ya mwaka jumla ni 39K,

Mimi stanbink kwa mwaka Makato yote 180K, nikaona this is too much, siweki hela tena uko.
 
Bro hiki kitu kinawezekana kikatoka ila ukifatilia utajua imetokaje au mkopo wamekata lakini haiwezekani wachukue tu kirahisi hivyo watu wanatunza USD miaka nenda rudi mkuu hizo Bank na hazichukuliwi kirahisi wewe wiki mbili tu?
Nilivuta statement, nikaona ni makato ya mwezi na ya kadi. Kuanzia mwaka 2021. Nikaishia kusikitika na kujilaumu kwa nini sikuwekewa hela hiyo EQUITY bank ambako ningeikuta kama ilivyo, bila kujali kama sijaweka fedha kwa muda mrefu. NMB, CRDB ni miyeyusho, wezi tu
 
Mmmmh hebu tukumbushe maana makato kwenye miamala yote ya pesa na bank yamekuja kipindi Samia ameingia na wengi walilalama sana …
Hata kama hampendi mtu msisahau sana hadi mkasema uongo………
Huu ni uongo hakuna makato yeyote wala chochote kilicho ongezwa kwenye miamala yote kipindi cha Magufuli muqche uongo…
Matatizo hayatatuliwa kwa kusingizia watu…
Mwigulu akiwa Waziri wa Fedha haya mambo ndio yameanza!
 
Mimi niko na NMB & CRDB Ila kwa yanayoendelea nafikiria nirudi Equity tu maana niliwazoea hata kufanyia manunuzi mtandaoni hawana makato ya kifaLa..
 
Hata huyo Customer Agent wa CRDB hakutakiwa kukujibu hivyo akikosea sana hizo ni confidential issue, angetakiwa kukuambia ni gharama za uendeshaji tu inatosha.
Hata benki nao wanakopa mkuu, zile charges wanazotutoza nfo wanalipia marejesho, Sasa mtu mwelewa huwezi mwambia mteja Mambo Kama hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…