CRDB Bank na makato ya matumizi ya kadi za ATM

Kweli hali ni mbaya. Ila hiyo ni kawaida mkuu kila benki lazima wakate gharama za uendeshaji
Nadhan umenielewa vibaya, mimi sijakataa gharama za uendeshaji

Mimi ninapigana na crdb kwamba kwanini wakate pesa yangu kulipa deni kwa wafadhili wakati deni ni la kwao?
 
Yaani uko serious kabisa uhame benki kisa Elfu 15?

Hiyo elf 15 unayo ona ni ndogo inavimbisha matumbo ya wenzako huko,, kinacho jadiliwa hapa sio udogo wa pesa leñgo nikwanini wakate hela ya mteja bila makubaliano yoyote tena hakuna taarifa yoyote ya kumtaarifu mteja,, bañk ni sehemu inayo aminiwa sana kuwa ni safe kwa kutunza pesa lakini kuna wizi mdogo mdogo tena wa akili sana sababu binadamu tumekuwa wapuuziaji wa mambo madogo madogo,, tubadilike jaman wewe kama unaona hiyo elfu 15 ndogo kuna mwingine hiyo ndiyo balance yake ya mwaka,, hivi viteñdo inatakiwa tuvipinge kwa pamoja ña si ubinafsi USIJIANGALIE WEWE MWENYEWE MKUU
 
Taasisi za serikali ni wezi tu.mimi natumia bank of Africa(no)haina huo uhuni
 
Kwanza akaunti yako ni ya aina gani,Inacashflow kiasi gani,Una Hela?Maana wakati mwingine kulalamika kwa ajili ya 17000 kunaweza kuwa nako ndio chanzo cha matatizo.Wanaocha Ela zao Benki zikatwe ni wale wenye Bili kadhaa.Ila kama hela yako ya Mawazo we Tumia Tigo PESA,MPESA AIRTEL MONEY Kuweka PESA YAKo
 
Kabla ya kutoa hela zako zote huko unapotaka kwenda fanya udadisi ujue je kuna uafadhali???

Isije ikawa unaruka mkojo halafu unakanyaga m*vi
 
Sisi tulishakubali matokeo! Tunachofanya fedha ikiingia benk inaondolewa upesi.
 
Hwa Hawa ni kuasha damu kabisa
 
Mimi sikulijua hilo la kukatwa 15000 ila la 2000 kila mwezi nalijua na waliniambia pamoja nakatwa 2000 kama gharama ya uendeshaki lakini pia ni Bima ya maisha waliambia kama niikifariki wao wanatoa sh. 5000,000 kusaidia msiba na sikumbuki vizuri kuhusu wategemezi wangu. Pia fedha ndani ya Bank ya CRDB zinaangaliwa sana na mifumo ya kiusalama yaani kama umeingiziwa hela nyingi utaulizwa maswali kama nini.
 
Sehemu rasmi ya kupata ufumbuzi wa wizi huu ni Benki Kuu(BOT).
 
Shida ya watanzania wengi,hatujali sana mambo ya msingi,na mataasisi mengi yalishaliona hili.Ingekuwa hii mada ya inahusu ngono ungepata wachangiaji wengi ila kwa sababu ni ni hii mada,wachangiaji watakuwa wachache.
sio watz tu sema watu weusi kwa ujumla tupo ivo. asiyetaka akajie mbele (kwa sauti ya mange)🪡🪡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…