CRDB bank na mitandao ya simu mnatuibia

Joined
Mar 7, 2017
Posts
11
Reaction score
13
Kila ninapohamisha fedha toka bank kwa njia ya simu ni lazima niwe na salio la kawaida kwenye simu, tatizo ni pale ninaporuhusu kukatwa salio la kawaida ili muamala ukamilike salio linakatwa halafu muamala haukamiliki kwa nini msiwe mnakata salio baada ya muamala kukamilika hamuoni kama huo ni wizi ba unyanyasaji kwa mteja wenu.
 
Tatizo sio CRDB.. Tatizo umejiunga kwa kutumia line ya Voda.. Tumia tigo au Airtel.. Na sio CRDB tuu, Bali hata NMB kama umejiunga kwa kutumia line ya Voda..

Nenda branch ya karibu na wewe na CRDB, waambie unahitaji kubadi namba inayotumika kwenye simBanking, watakusaidia mkuu..

Pole sana..
 
Umenena vyema mkuu voda ni michosho ilaukijiunga kupitia tigi,halotel na airtel iko vizuri hawakati pesa
 
Voda wanatamaa wanyonyaji sana sio CRDB na miamala Yao ikikwama ujue imekula kwako
 
Umenena vyema mkuu voda ni michosho ilaukijiunga kupitia tigi,halotel na airtel iko vizuri hawakati pesa
Kwa hyo hata nisipokuwa na salio kwenye lain ya tigo au airtel naweza kuacess menu ya simbanking?
 
Voda ni tofauti na mitandao mingine wao hawafanyi kama mitandao mingine ambayo hukata pesa mara moja tu kwa mwaka ili uweze ku access USSD code za bank zote bure.
 
Umenena vyema, hayo malalamiko yake apeleke Voda.
 
Sory naomba kuuliza ivi CRDB wana Bonus account?? ile ambayo haikatwi bank charges za mwisho wa mwezi
 
tumia laini ya Tigo mkuu wao ni bure hakuna makato
 
Voda wananikera sana nataka nibadilishe nitumie line ya airtel au tigo maana hawaendi na wakati umekuwa mtandao wa kipumbavu sana,nashindwa hata kununua vocha kupitia simu banking.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…