Hivi mko serious kweli, haya maneno ya kuibiwa unamwachia Mungu yanatokana na nini? Mi nilikuta 70,000 imepungua siku hiyo hakuna aliefunga benki. Walileta longo longo eti nimewapa watu password na hela imetolewa ATM, nikauliza ya wapi?, ilikua lumumba wakaniuliza na wao ulifungulia account wapi?, balaa likaanzia hapo kwenye majibu ya hovyo. Mpaka Brach manager alikuja, akanishauri niende Azikiwe nilikofungulia account. Nilienda nikaeleza mkasa mzima wakachek wakaona ni ATM ya PPF tower imehusika. Nikawaambia nataka hii hela sasahivi, nao walinisukumia PPF. nilifika hapo na ilikua mida ya kufunga, nikawaambia nataka hela sio story, ilibidi nibaki humo na watumishi kufuatilia camera tuone mwizi nani.
Wee, nguvu zote ziliniishia nilipoona ni mdogo wangu ambae nilijua hajawahi hata kuiona ATM card yangu. Basi nilijifanya simjui na nikaaga eti nitarudi kesho kwa taratibu za kuandika barua ya ku-claim. Sijarudi hadi leo.
Najua mnataka kujua huko nyumbani ilikuaje, ila nachotaka kuwaambia ni kwamba futeni hizo habari za kumwachia Mungu, dai haki yenu hadi ipatikane.