CRDB kuweni makini. Ada Loan yenu ni huduma nzuri iliyokosa maafisa masoko makini

CRDB kuweni makini. Ada Loan yenu ni huduma nzuri iliyokosa maafisa masoko makini

Kiti cheupe

Member
Joined
Apr 8, 2024
Posts
7
Reaction score
8
Benki ya CRDB wamekuja na huduma mpya inayoitwa Ada Loan. Ni bonge la ubunifu, lakini tatizo ni kwamba maafisa masoko wameifanya kuwa huduma ngumu sana kwa mteja kuipata.

Mfumo wa benki unazitaka shule zioanishe mfumo wa shule na mfumo wa CRDB ili mteja alipiwe ada ya mtoto wake.

Shule nyingi hazitaki, maana utaratibu huo unaanika taarifa zao za siri kwa benki ya CRDB, kama vile majina ya wafanyakazi, idadi, mapato ya shule, malipo ya kodi, n.k.

Hiki ndicho kinachokwamisha shule nyingi kukataa hiyo huduma, japo wazazi wanahangaika huku na kule kutafuta shule zenye huduma hii.

Ushauri wangu kwa CRDB ni watumie kigezo kimoja tu: shule kuwa na akaunti ya CRDB basi inatosha.

Mzazi aende benki, ajaze fomu za kuomba kulipiwa, halafu benki ilipe moja kwa moja na kumpa mzazi risiti apeleke shule.

Ninyi maafisa masoko mliolundikana hapo CRDB, huu ugumu wa hii huduma hamuoni? Mtu mwenye D2 anaona kitu ambacho wenye digrii na master's hawaoni kweli?
 
Ni kweli Cha muhimu shule Ina akaunti crdb ,mzazi atajaza taarifa basi ada inalipwa, mambo mengine ni kufanya hii huduma isiwe na tija, Kwa mfano mm naweza kopa milioni 2.5+ , lakini kwangu ni useless Kwa sababu shule haina huo mfumo wanaotaka crdb.
 
Nakazia.....marekebishp yafanyike...CRDB muwe wasikivu
 
Tafuteni ada kwa namna nyingine achaneni na hiyo loan.
 
Back
Top Bottom