CRDB mjitafakari!

CRDB mjitafakari!

kilambimkwidu

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2017
Posts
6,097
Reaction score
7,199
Mteja anapokea fedha kwenye accounts yake fedha zinafika na kusoma lakini mteja hawezi kutoa.

Mteja anafanya muamala, m.f, anatuma hela kwenda kwenye mtandao wa simu, ombi linapokelewa na kushughulikiwa hakuna feedback kama imefanikiwa au la.

Mwingine anafanya muamala wa kutuma, hela inatoka na haifiki kwa mpokeaji.

Customer experience kwa hii benki ni hovyo kabisa. Hovyoo!!
Screenshot_20220623-083257_Instagram.jpg
 
Mteja anapokea fedha kwenye accounts yake fedha zinafika na kusoma lakini mteja hawezi kutoa.
Hapo tatizo ni la tigo au crdb? Kwa maono yangu crdb anataka kukwepa majukumu yake kwa kusingizia tigo, fuatilia paka mwisho kataa hayo majibu ya kukulizisha ili uondoke
 
Hapo tatizo ni la tigo au crdb? Kwa maono yangu crdb anataka kukwepa majukumu yake kwa kusingizia tigo, fuatilia paka mwisho kataa hayo majibu ya kukulizisha ili uondoke
Benki imeamua kukimbia mteja wake na mumuacha 'akafe' mbele
 
Hiyo fedha bado iko bank, inawezekana imetokana na tatizo la mifumo; waandikie barua ili wafanye 'reconciliation' na tigo, ili uweze kupata fedha yako.

Ilishawahi kunitokea miaka ya nyuma, niliamisha laki 8 (nbc) kuja kwenye simu (voda); pesa ilitoka kwenye akaunti, ila kwenye simu haikufika; ilinichukua mwezi mmoja mpaka pesa kuipata, baada ya kuandikiana sana barua, pamoja na wao kukaa vikao.
 
Niliachana na CRDB baada ya kadi yangu kumezwa kila nikitaka kutoa hela. Siku moja alfajiri nimeenda ATM nilikuwa na short trip nimeingiza kadi ikamezwa na ATM nikasema; fine.

Nikakaa kama siku nne hivi nikaenda kwenye ofisi zao ndani, nikasubiri takribani lisaa moja na nusu na nikakabidhiwa kadi yangu.

Baada ya kutoka nje ya ofisi nikasema ngoja niingie kwenye ATM nikatoe pesa kidogo looooh! Kadi yangu ikamezwa tena, huo ndio ulikuwa mwisho wa mimi kutumia CRDB.

Hii ilinitokea mwaka 2020.
Mpaka sasa sitaki hata kuwasikia.
 
Kwa kifupi customer care kwa Tanzania bado ni 0% kwa wengi ni mashirika machache sana yameuphold ubora wa hii issue ya customer care ila wengine wanachojua customer care ni kupokea tu simu au kufanya reply kwenye mitandao.
 
Niliachana na CRDB baada ya kadi yangu kumezwa kila nikitaka kutoa hela. Siku moja alfajiri nimeenda ATM nilikuwa na short trip nimeingiza kadi ikamezwa na ATM nikasema; fine.

Nikakaa kama siku nne hivi nikaenda kwenye ofisi zao ndani, nikasubiri takribani lisaa moja na nusu na nikakabidhiwa kadi yangu.

Baada ya kutoka nje ya ofisi nikasema ngoja niingie kwenye ATM nikatoe pesa kidogo looooh! Kadi yangu ikamezwa tena, huo ndio ulikuwa mwisho wa mimi kutumia CRDB.

Hii ilinitokea mwaka 2020.
Mpaka sasa sitaki hata kuwasikia.
Hii imenitokea leo
 
Customer Service kibongobongo ni mtihani sana, hata kwenye mitandao ya simu nako ni kisanga pia.

I wish wangekuwa Responsible kwa madhara wanayosababisha kwa kutojali wateja.

Wamekusikia watalifanyia kazi Mkuu.
 
Back
Top Bottom