CRDB mmefanya kibaguzi haiwezekani Zanzibar mtoa mikopo isiyo na riba,Tz bara mikopo iwe na riba

Dr Msweden

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2020
Posts
2,629
Reaction score
9,530
Hii imekaaje wadau naona imekaa kibaguzi sana,ina maana sisi Tanzania bara hatuna uhitaji na hiyo mikopo au? Zanzibar ni wa muhimu sana kwenu kuliko sisi? Au Zanzibar ni masikini sana mmeamua kuwapa upendeleo?
Kila siku wajasiriamali wanalia kuhusu riba lakini mmeweka pamba masikio.
Kama swala ni imani kuwa hakuna riba bhasi kaeni hivyo hivyo bila kufungamana na upande wowote

 
Huko Ni Zanzibar.

Unaweza kuambiwa Ni mikopo isiyo na RIBA.

Kumbe inatolewa MIKOPO yenye FAIDA😀
 
Waongo tu hao..na wanafiki watupu..eti islamic bank hakuna riba?..thubutu uone..PBZ riba kama zote...hizi dini kwa unafiki zimejariwa.

Shetani hanaga rafiki..watakulima riba mpaka uchanganyikiwe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Riba hakuna lakini faida ipo..ni lugha tu
 
Kwamba crdb inashirikiana na serikali ya mapinduzi znz kutoa Mikopo isiyo na riba... Maana yake serikali ndo inatoa 'ruzuku' kwa kulipa riba za hiyo Mikopo ya crdb.

Program hiyo itanufaisha wazanzibar zaidi ya laki 7, maana'ake ni zaidi ya nusu ya wazanzibar wote watanufaika.

Si ajabu fedha inayotumika kwenye program hiyo ni ya Tanganyika
 
Bank za kislamu zinatoa mikopo bila riba, uislamu hauruhusu riba ni dhambi sababu kule Kuna waislamu wengi wameamua kutumia matakwa ya dini Yao
 
Kati ya crdb bank na serikali ya umoja wakitaifa Zanzibar Nani kamfata mwezake kuomba huduma ....huo uchumi wa bluu niwa crdb bank au waserikali ....Tanzania bara hatuna uchumi wa bluu ilaumu serikali yako iliyopeleka mikopo yenye soft condition ngazi ya halmashauri yako
 
Usijali wanaanza Zanzibar as pilot area. Mambo yakiwa mazuri itasambaa nchi nzima.

Don't worry my dear

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Hawataki tu hilo neno riba, kwa hiyo wanatuma neno lingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…