Siku zote kuna faida na hasara hata ukiweka katika kibubu, mfuko wa rambo ukachimbia, ukazichimbia handaki,uka weka kokote unakoona umeweka salama ipo siku utakwama tu!
Cha msingi kwa technologia tunayoenda nayo mahaka/wezi wa mtandao wataongeza ni wewe kuwa na tahadhari na kusoma vipeperushi mbalimbali ili ujielimishe usije ibiwa ukisubiri mtu asome kwa ajiliyako utakuja lipia gharama ya muda wake/utaibiwa.
Na uwe na akaunti katika benki tofauti ili moja iwe ya mobile na nyingine usitake huduma hiyo ili uweze kufuatilia kwaurahisi pesa zako na matumizi yake kwani Simbanking/Nmb mobile na nk ufuatiliaji wake ni mgumu na Hizi huduma ni nzuri zinarahisisha kazi zetu. Kwahiyo kuwa na akaunti mbili moja jiunge ila nyingine usijiunge na uliyojiunga isiwe na pesa nyingi sana ziwe ni za kuhudumia matatizo madogomadogo na isiyounganishwa weka pesa zako kwani ikitokea wizi ni rahisi kufahamu kilichofanyika na utarudishiwa kirahisi.
Mobile banking ni nzuri sana ila tumia kwa uangalifu maana pesa kupotea ni rahisi kwani unaweza kuchukua muda wowote na wakati wowote na popote pale na inaweza ukawa unaibiwa senti ndogo sana usijue au usione adhari kwa mapema.
Kuibiwa benki hutaweza kuzuia maana si wote wanaojua salio/masalio yao au riba wanayopata kwa miezi 3 au mwaka mzima cha msingi ni kupunguza uchotaji wa vijisenti vyako ambapo unaweza kuuliza salio hata mara 3 kwa siku hali kuna wengine hata hawajui salio lao na wengine masalio/salio lao ni kuna milioni ngapi na laki ngapi, makumi elfu hawajui hata kama wamechukua karatasi ya salio.
Nashauri waliojiunga watumie kwa uangalifu na si kuacha kutumia kwani matumizi ya huduma hiyo ni makubwa kuliko unavyodhani wewe na hayana weekend na hayana muda wa kazi wala wa sikukuu au siku ya mapumziko bali ni kutatua tatizo kwa urahisi na kutumia muda mchache