Asia mi nafikiri una panic bure, ukirejea post yangu iliyopita nilikuwa najibu hoja ya kwamba "eti hata hao jamaa wakiuza share zao CRDB can still float its shares". Hili ndilo nililokuwa nalizungumzia, na nimelieleza kitaalamu kabisa. Kama wewe ni mfuatiliaji wa mienendo ya masoko ya Hisa utafahamu kuwa perception ya market players ndio ina athiri kwa kiwango kikubwa kupanda ama kushuka kwa bei za hisa (let alone the performance).
Utaona hata katika GFC inayomalizika hivi sasa, kampuni nyingi ziriathirika kutokana na perception ya market players. Ndio maana soko la hisa la NY na London yalipotetereka moja kwa moja tukaona masoko mengine ya ulaya na asia yakianza kuterereka.
CRDB kumilikiwa na watanzania si kinga ya kutoanguka wala kutopika financials zake (sisemi kama wanapika). Utakumbuka kwamba Enron ilidondoka miezi 9 tu baada ya kutangaza faida ya mwaka uliotangulia (na pia miaka 12 nyuma ilikuwa ikipata faida tu). Kwa hiyo wewe kupata gawio toka CRDB Ltd ianzishwe si kinga ya share zake kutoporomoka!! Enron hao hao August 23, 2000 price per share ilikuwa US$ 90 na Nov 28, 2001 bei ikashuka mpaka kufikia below US$ 1.
Ndio maana nika emphasise katika kuimarisha CMSA na DSE ili ziweze kutusaidia wawekezaje si wa CRDB tu bali watanzania kwa ujumla!!
Sina hard feeling na CRDB bali huo ni mtizamo wangu huru tu.
Tuambiane ukweli hata kama unauma