Crdb waiba katika akaunti yangu

Crdb waiba katika akaunti yangu

Mpaka sasa masaa 24 yamepita ila sijapata pesa na kwenye akaunti kiasi nilicho toa hakimo
 
CRDB mbona hiyo ni tabia yao tu? Tena hata katika ATM unatoa pesa inahesabu mwishowe hazitoki ila inakupa risiti kuw aumechukua. Ilinipata siku moja halafu ilikuwa ni ijumaa, ikabidi niwatokee jumamosi asubuhi na risiti yangu wananitaka niandike barua na kuweka na risiti, hela wakarudisha baada ya siku mbili. Wahuni hawa. Huduma mbovu sana katika CRDB na nyodo nyingi kwa kuwa wana wateja!!
 
Hamieni benki ndogo ndogo zina nidhamu na wateja!
Hawa wakubwa kiburi na wafanyakazi wao ndio balaa!
 
Kaka unakosea......hii product bado ni changa apa kwetu Tanzania nikimaanisha aina mwaka,ivyo matatizo ya ela kutomfikia mlengwa muda muafaka au kutokufika yapo ila in long term yatapatiwa ufumbuzi.hii product ni mapinduzi makubwa and its an african born technology.........Benki aina haja ya kukuibia cjui laki mbili zako au elfu hamsini

Tatizo waafrika tumekubali kuubatiza UZEMBE na kuuita majina mengi.... bahati mbaya, vuta subira, usiwe na wasiwasi, ndio tunaanza anza nk. Alivyoelezea jamaa utaona kabisa kuna uzembe! Kama fedha inachukuwa muda mrefu zaidi kwanini wateja wasiambiwe! Kama usiku wanazima sijui 'system', kwanini wateja wasihabarishwe. Kwa kifupi majibu ya wachangiaji wengi yamelinda uzembe na si kupiga vita!
 
Umepanic mkuu..
CRDB wana namba kama 4 za call centre..hizo zilikuwa busy na wewe ukapanic..
Uzoefu wangu na CRDB-MPesa ni kuwa hela unayotoa kwenye account (kwenda Mpesa) ikizidi kuwa kubwa ndio huchukua muda mrefu zaidi..
mara ya mwisho nilipozungumza na call centre walidai kuwa inaweza kuchukua maximum time ya saa 24 kufikia account yako ya Mpesa...
Ni upotevu wa muda lakini ndiyo hivyo tena....
 
Mpaka sasa masaa 24 yamepita ila sijapata pesa na kwenye akaunti kiasi nilicho toa hakimo

Angalia salio la Mpesa..
kama haionekani kokote nenda CRDB Branch ukatoe maelezo ya huo muamala (transaction reference number)..
 
Ulihamisha saa ngapi? Make muda mzuri ni kuanzia asubuhi saa mbili hadi jioni. ukihamisha usiku inatokea hivyo na ukiwailiza wanakuambia systeam inakua imezimwa. ila utarudishiwa tu. make mimi mara zote ilirudishwa. na hizo namba usipige muda ambao sio wa kazi make hupati mtu.

mkuu usikubali upewe jibu kama hilo, waulize hivo ni system gani ambayo inakuwa imezimwa!? kwa kweli customer care kwa bongo ni mbovu. whites ukimwambia system cjui imefanyeje hakuelewi na anafunga a/c yake
 
Wabongo tumezoeshwa huduma mbovu.
Wanakwambia unapata pesa yako fasta kwa kutumia simu, halafu ikichelewa uvumile na watu wanaunga mkono!!
Kama unaweza kupata fedha kwa kutumia simu baada ya saa 24 kuna efficiency gani hapo!!

Kuna mahali nilikwenda kupata huduma nikafuata taratibu zote lakini wakawa wananiambia "usijali muda si mrefu mambo
yatakuwa ok" wakati muda unaenda....nikawaambia niambieni exactly ni saa ngapi ili nijue la kufanya, wakanihudumia fasta....Ajabu ni kwamba wako wateja wengine pale walioniona kama mtu mnoko.

Naamini hakuna mtu mjinga kama yule anayenyenyekea anachopaswa kupata tena akiwa amelipia.
 
Leo ni siku ya tatu wakuu sijapata pesa zangu,mwanzo niliambiwa nisubiri kidogo nikafanya hvo thn nikaambiwa nisubiri masaa 24 nikafanya hvo sasa mpaka leo masaa 36 hiyo pesa bado imegoma tu, huu si ni utapeli wa waziwazi wakuu
 
...Niweke wazi tu kwanza mimi ni Mteja wa CRDB kama wewe Mkuu.Kuna maswali kadhaa ya kujiuliza kabla huja-panic sana kuhusu hili:
Je hii ni mara ya kwanza kuitumia hiyi huduma?
Kama sio mara ya kwanza, ina maana huko nyuma umeishawahi kuitumia na hukupata matatizo yoyote sio??
Maelezo yako ni kama unaunganisha kupotea pesa zako na kukatwa simu yako inapojibiwa, lakini elewa kuwa huo utakuwa ni uzembe wa huyo mpokea simu tu na si kwa sababu anajua kuwa umeibiwa na hivyo hataki hata kusikia unachotaka kusema! Fahamu Mpesa na Switchboard ni sehemu mbili tofauti.

Mimiimeishawahi kunitoke mara 2 hali ya kutuma pesa isiingie kwenye simu yangu lakini iwe imeondolewa kwenye accaount yangu ya CRDB.
Hiyo mara ya pili ilichukua karibu masaa 16 kupata hela yangu kuanzia jumamosi saa 11 jioni hadi jumapili saa Tano mchana!
Jema ni kwamba nilifuata taratibu hizo hizo ulizofuata wewe na bahati njema zaidi ni kuwa mimi nilipokelewa kwenye hizo namba unazosema na kuelezwa kuwa kuna mtu alighafirika na kusahau kufanya alichotakiwa kufanya ili hela ihame!
Waliomba radhi kwa hilo na nikakubali yaishe kiungwana.
Naamini hela yako ipo.
Kazana kupiga hiyo namba ama ukiona vipi sogea kwenye tawi lolote la CRDB lililo karibu nawe ueleze madhila yako na ninaamini utapata Uchache (Wingi????) wako!
Utujulishe Kitakachoendelea.
Pole sana Mkuu.

Ni dhahiri system ya transfer BANK -> MPESA siyo automated ndio maana transfer inachukua muda mrefu na prone to human error.
 
...HAWA CRDB SASA WAMANICHEZEA.
Toka jana nimefatilia mpaka leo sijapata kila nikienda naambiwa niwe mvumilivu sasa leo tena nimekwenda naambiwa niende kesho hivi huu si ni wizi wa mchana kweupe,
SASA NAHITAJI KUWASHITAK KWA UBADHILIFU WALIONIFANYIA HIVO NAOMBENI MSAADA WA KISHERIA WAKUU NIANZE VIPI KUWAFUNGULIA KESI

MAONI YENU NI MUHIMU SANA KWANGU ASANTENI,

Pole kwa usumbufu uliopata,kama upo dar then fika tawi la azikiwe..wanaweza wakakusaidia kwa haraka.
 
Subiria kama siku 2 hivi za kazi. It happened to me once, nilitransfer pesa J.mosi ikaingia J.5. Kumbuka tunaishi dunia ya 3
 
CRDB ni majanga nilitumia visa card yangu ya bank ingine wakanichapa laki saba na ishirini alafu ukiomba irudishwe unaambiwa usubiri siku 45 sasa kama vitu vya kidigitali tunasubiri siku zote si bora turudi analojia tu wakui??
 
Hamieni benki ndogo ndogo zina nidhamu na wateja!
Hawa wakubwa kiburi na wafanyakazi wao ndio balaa!

...Hizi Banki ndogo ndogo bado zinabembeleza Wateja. Nazo zikiisha kuwa Kubwa Kubwa mambo yatakuwa yale yale! Tatizo sio Benki kuwa Ndogo ndogo ama kubwa kubwa! Tatizo ni Poor Costumer Care...!

 
Huwa najiuliza, kama benki wanafanya kosa unakua wajibu wa nani kifuatilia? Kwamba kosa litokee kwao.....ila gharama za ufuatiliaji zitoke kwa mteja.
Mteja ana haki zozote za kudai fidia ya madhara ya matatizo ya mfumo wa benki?
 
pamoja na kuwa benki zinamasumbufu mara kadha, sidhani kama ni sahihi moja kwa moja kusema benki wamekuibia kwa kuwa case yako inahusisha mtandao wa simu. Je unahakika gani kwamba lipo benki na sio system ya simu kupokea hela kutika benki. Tunafahamu kuwa mpesa kuna transaction za mamilion/bilion kwa siku na kuwa hawa wanatemporary account ya kuweka fedha zako benki ijapokuwa unaziona katika simu yako. Kwa hivyo nadhani ujaribu kufuatilia kote kote na sio konclude kuwa ni benki wamekuibia wakati mpesa sio platform yao. Ingekuwa ni within bank hapo sawa. Ni mtazamo tu tusilalame tu bila kuangalia undani wa tatizo.
 
Back
Top Bottom