Kabla ya uharibifu wa mifumo ya kibenki, kila kitu kilikuwa kikienda vizuri, lakini bank hiyo ikatoa tamko kuwa ilikuwa inaenda kuboresha mifumo yake, wateja wakaombwa wawe watulivu. Mara walipoanza, huduma za kibenki, kwa siku 4 mfululizo zikawa ama hazipatikani kabisa, au zikipatikana nusunusu kwa ubora duni kabisa. Baada ya kipindi walichokiita cha maboresho kumalizika, wakatuma ujumbe kwa wateja kuwa uboreshaji umekamilika, na wateja wafurahie huduma:
'
'Mpendwa Mteja, endelea kufurahia huduma zetu kupitia Matawi, CRDB Wakala, ATM, Internet Banking, SimBanking na POS wakati tukikamilisha maboresho kwenye baadhi ya huduma. Asante kwa uvumilivu wako katika kipindi hiki'
Wateja wakadanganyika, na kuuamini huo ujumbe. Walichokutana nacho wateja ni uhuni mtupu: mifumo ya simbanking ikiwa imevurugwa kwa kiwango cha ajabu. Hata ATM machines nazo zimekuwa zikifanya kazi kwa kibahatisha sana. Baadhi ya watu wanatoa pesa, wanatumiwa ujumbe kuwa wametoa pesa, lakini pesa haitoki.
Kwa kweli kama lengo lilikuwa ni kuvuruga mfumo wa banking, wahuni wamefanikiwa.
USHAURI:
1. Kwa sasa, usitumie mfumo wa simbanking, wala ATM machines kutoa pesa, kuzuia uwezekano wa kuambiwa umetoa pesa kumbe hela haijatoka.
2. Kwa sasa, kama unataka kutoa pesa, ingia ndani ya bank, na utoe kwa mfumo wa makaratasi. Ikiwezekana toa kiasi kingi ili kuzuia uwezekano wa kila mara kurudi kwenye foleni za bank. Kama hela uliyoitoa ni nyingi, kama una bank account kwenye banks nyingine au kwenye makampuni ya simu, aheri ukaweke huko ambako una uhakika wa kuitoa muda wowote unaotaka kuitumia.