CRDB yaamuriwa kumlipa Zawadi Bahenge milioni 300 kwa kutumia picha yake kwenye matangazo bila ridhaa

CRDB yaamuriwa kumlipa Zawadi Bahenge milioni 300 kwa kutumia picha yake kwenye matangazo bila ridhaa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeiamuru Benki ya CRDB kumlipa fidia ya Sh300 milioni Zawadi Bahenge kwa kutumia picha yenye sura yake kwenye matangazo ya kibiashara bila ridhaa yake.

Pia mahakama imeiamuru benki hiyo kuondoa picha zote za balozi huyo wa Tacaids kwenye mabango yake ya kibiashara yaliyosambazwa nchi nzima.

Mahakama imefikia uamuzi huo katika hukumu iliyotolewa jana Aprili 30, 2024 na Hakimu Mkazi Mkuu, Rahim Mushi, katika kesi ya madai aliyofungua Bahenge dhidi ya benki hiyo akiilalamikia kwa kutumia picha yake kwenye matangazo ya kibiashara katika kampeni ya ‘Tupo kuijenga biashara yako’ bila ridhaa yake.

“Ifahamike kutumia picha ya mlalamikaji kwenye matangazo ya kibiashara umeingilia faragha yake bila ya ridhaa yake,” amesema Hakimu Mushi katika hukumu hiyo na kuamuru.

View attachment 2978528
Wakili wa kujitegemea, Ferdinand Makole akiwa na Zawadi Bahenge baada ya kutolewa hukumu ya kesi ya madai ya CRDB kutumia picha ya mteja wake (Bahenge) bila ridhaa yake.​
Amekula bingo
 
Kwanini ni yeye tu dhidi ya makampuni makubwa nchini?
Huo ni mchezo unatengenezwa na watu waliomo ndani ya taasisi zinazo shitakiwa au wakishirikiana na kampuni za kuandaa matangazo ya biashara kwa niaba ya hizo taasisi.
Yupo jamaa yangu marehemu kwa Sasa alikuwa anapewa dili na wafanyakazi wa kampuni fulani kubwa ya mawasiliano (simu) anafungua kesi za madai wamejenga mnara wa simu kwenye eneo lake.

Yeye mkazi wa Dar wanamlimpia nauli na hotel aende kuhudhuria kesi Mtwara, akishinda wanampa ya mboga nyingi wanakula wenyewe.
 
Haiwezekani mamlaka ya juu ya benki ipo, mabango yakasambaa nchi nzima bila mamlaka za juu za benki kuyaona na kujiuliza yametoka wapi, nani kayalipia, kayaidhinisha.... Kuna mwanasheria wa CRDB, kitu kama hiki lazima kipitie kwake.......MWANASHERIA....... hajui kuwa kutumia sura/jina la mtu katika biashara ni kosa... Kuna internal arrangements zilihusika kufanya haya na kumwambia binti kadai fidia mahakamani.........
Yaani benki wanakaa na kuona picha ya binti na kuamua kuiweka kwenye matangazo, basi likapita..... common ens e and intuition does not support that!
Ila mtu kutumia nembo ya Simba sio kosa ?
Sio kwa ubaya nauliza tu
 
Back
Top Bottom