Credibility Check: SBT Japan Kampuni ya Kuuza Magari

Tiba

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2008
Posts
4,605
Reaction score
3,176
Wapendwa wana Jamvi,

Niko kwenye mawasiliano na hii kampuni inayojishughulisha na kuuza magari yaliyotumika huko Japan. Wenye hii kampuni ama ni wahindi au Wapakistani. Nimeongea nao kwa simu na kupitia skype pia. Wanataka kuniuzia gari na makubaliano yapo katika hatua za mwisho. Sijawahi kufanya biashara na hawa watu, hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza.

Kwa kuwa pesa itakayotumika kwenye manunuzi ni kubwa, nimeogopa kuendelea na hii deal bila kutafuta ushauri. Je kuna mtu amewahi kufanya nao biashara hawa jamaa? Wako genuine kiasi gani?

Naogopa kuuvaa mkenge mchana kweupeee!!!!!.

Tiba

FEEDBACK:

Kufuatia ushauri wa baadhi ya wadau hapa JF, niliamua kuingia makubaliano ya kununua gari na hawa jamaa wa SBT Japan. Ukweli ni kwamba wako very aggressive business wise na ukijitokeza kuwauliza kitu basi wanakuwa hawako tayari kukupoteza kwa hiyo kila wakati watakupigia simu, watakutumia email, watakutumia message through skype ilimradi wahakikishe wako na wewe karibu. Hali hii ilinitisha na ndio maana nilikuja hapa kuomba ushauri.

Tulikubaliana kwamba niwatumie nusu ya pesa ya gari na wao wakiishaipata wataanza process za kuship gari. Hilo lilifanyika. Walipomaliza shipping process wakanitumia copy ya bill of lading na mimi nikatuma nusu ya pesa zilizokuwa zimebaki. Baada ya kupokea hizo pesa ndio sasa wakanitumia original documents. Jana agent wangu aliniletea gari nyumbani likiwa katika hali nzuri kabisa na ni gari ambalo nilikuwa nimelichagua. Ila hawa jamaa tulitofautiana nao kitu kimoja kidogo. Tulikubaliana bei in dollars na invoice waliyonitumia ilikuwa in dollars. Nilituma pesa in USD lakini wanapozipokea waniambia wamepokea JPY. Matokeo yake at the end of the deal nilijikuta nalipa USD 200 zaidi kutokana na wao kuingiza hizo pesa kwenye JPY account na wala sio USD account. Niliwaambia warekebishe hicho kitu.

Kutokana na hii tabia ya kukubali nusu malipo na ukimalizia malipo ndipo wakutumie original docs, ndio maana magari mengi wanayo yasupply hawa jamaa yanakaa bandarini muda mrefu kwani endapo kwa mfano ukikosea kidogo wakati wa kutuma hela na hizo hela labda zikarudi ndio utume upya, basi unapoteza muda mwingi na wakati huo labda unakuta gari linakuwa tayari limefika bandarini.

Nawashukuru wadau wote waliochangia na kunihakikishia kwamba jamaa ni wazuri na hawatanifanyia utapeli. Kwa kifupi ni kwamba I recommend them in case any one of you want to do business with them.

Cheers,

Tiba
 
Wadau, please anayeijua hii kampuni anisaidie nisije ingizwa mjini na utu uzima wangu huu.

Tiba
 
Wapendwa wana Jamvi,

Niko kwenye mawasiliano na hii kampuni inayojishughulisha na kuuza magari yaliyotumika huko Japan. Wenye hii kampuni ama ni wahindi au Wapakistani. Nimeongea nao kwa simu na kupitia skype pia. Wanataka kuniuzia gari na makubaliano yapo katika hatua za mwisho. Sijawahi kufanya biashara na hawa watu, hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza.

Kwa kuwa pesa itakayotumika kwenye manunuzi ni kubwa, nimeogopa kuendelea na hii deal bila kutafuta ushauri. Je kuna mtu amewahi kufanya nao biashara hawa jamaa? Wako genuine kiasi gani?

Naogopa kuuvaa mkenge mchana kweupeee!!!!!.

Tiba

Huo kenge ingekuwa ni kaptula ningekuambia imekufika magotini. Soma magazeti
 
Mkuu magazeti yanaizungumzia hii kampuni? Au sijakuelewa.

Tiba
 
Binafsi pia sijawahi kufanya nao biashara,ninachokifahamu ni kwamba,kwakua wanamawasiliano na wewe watakupigia sim kila mara kuulizia umefikia wapi,kwa kweli inahitaji uvumilivu sana mana ni wasumbufu.
Nimewahi kufanya biashara na kampuni nyingine inaitwa Beforward,jamaa wako smart sana.
 
Ni kweli mkuu, simu wameishanipigia karibu mara tatu hivi tumeongea. Vile vile nimeongea nao kupitia skype na wana online chat yao ambayo tumeitumia pia kufanya mawasiliano. Tatizo langu sijui kama wako genuine, unaweza kuwatumia pesa ukawa mwisho wa mchezo na gari wasitume. Kuhusu hao be forward, nimesikia sifa zao kwamba hawana longo longo lakini bahati mbaya gari linalolihitaji wao hawana kwenye stock kwa sasa.

Tiba
 
Mkuu magazeti yanaizungumzia hii kampuni? Au sijakuelewa.

Tiba

Nilikuwa naagiza gari mwezi wa kwanza nikachagua gari wakaniambia nina bahati kwa kuwa stock niliyochagua ipo baharini inakuja bandari ya Dar hivyo haitanichukulia muda sana. wakanipa na Bill of lading kumbe wametwist dates kwenye ile soft copy ya BL. Nilipokwenda kwa rafiki yangu ni clearing agent akacheki na TRA kumbe ile gari ilifika bandarini siku nyingi na ina port charges kibao. Ni jana tu nimeona kwenye gazeti TRA wanapiga mnada magari yao
 
Mkuu Tougher, asante kwa ufafanuzi. Ina maana waliokufanyia hivyo ni hawa hawa SBT Japan au ni kampuni tofauti. Inaelekea hawa SBT hawana ofisi Tanzania. Nipe ufafanuzi wa ziada mkuu.

Tiba
 
The Pakistani are bad news, for what I hear. Kwanini usiongee na beforward?
 
Ndio mkuu Abdulhalim, hawa jamaa kama sio wahindi, basi ni wapakistani kwa muonekano wao na lafudhi yao. Be forward hawana hilo gari ninalolitaka kwa sasa. Kwabhiyo mkuu unsnishauri niachane nao hawa jamaa?

Tiba
 
SBT Japan tatizo lao kubwa ni kwamba wanapakia gari zao kabla hata hawajapata wateja na zinafika bandarini wanaanza kusumbua wateja, mm mwenyewe walishapiga sana cm mpk ck hz ctak hata kuzipokea, hawajajipanga sawasawa bado!
 
Mkuu Tougher, asante kwa ufafanuzi. Ina maana waliokufanyia hivyo ni hawa hawa SBT Japan au ni kampuni tofauti. Inaelekea hawa SBT hawana ofisi Tanzania. Nipe ufafanuzi wa ziada mkuu.

Tiba

Tiba
Ni wao wenyewe nilikuwa nawasiliana nao toka huko, i have emails to confirm. Nilikuwa robo saa away from kuingia mkenge, nilikuwa nawasilian na mtu anaitwa Obadia Zia, nilipochomoa akaja huyu Hafiz Ishaq Ahmed, baadae tena akaja huyu Muhammad Ilyas. Walipoona nazidi kuwakatalia wakamleta huyu mwenye jina kama la kibongo Pete Andrew Cariaga.
 
SBT Japan tatizo lao kubwa ni kwamba wanapakia gari zao kabla hata hawajapata wateja na zinafika bandarini wanaanza kusumbua wateja, mm mwenyewe walishapiga sana cm mpk ck hz ctak hata kuzipokea, hawajajipanga sawasawa bado!

Asante mkuu nashukuru kwa mchango wako. Sasa wakipakia gari kabla halijapata mteja likifika Bandarini inakuwaje? Wana agent wao hapa Tanzania kweli?

yah..hawa jamaa kweli ni kampuni ipo na inauza magari na ndege pia. ni kubwa tu but wana tatizo moja na ucheleweshwaji wa kusafirisha gari. Mwaka jana nilinunua gari tika kwao gari ilkaa miezi mitatu ndio ikafika ikiwa haina spea tairi na betri imekufa. So for advice go to another company. Be foward ni wazuri kiutendaji but magari yao yanamikwaruzo sana na yameenda mileage kubwa.
kuna kampuni inaitwa tradecarview wako vizuri sana. nimefanya nao kazi mara mbili bila tatizo lolote.
 
Tiba
Ni wao wenyewe nilikuwa nawasiliana nao toka huko, i have emails to confirm. Nilikuwa robo saa away from kuingia mkenge, nilikuwa nawasilian na mtu anaitwa Obadia Zia, nilipochomoa akaja huyu Hafiz Ishaq Ahmed, baadae tena akaja huyu Muhammad Ilyas. Walipoona nazidi kuwakatalia wakamleta huyu mwenye jina kama la kibongo Pete Andrew Cariaga.

[/TABLE]

Asante mkuu kwa ufafanuzi. Unaona faida ya kufanya credibility check? Bila hivyo na mimi ningejikuta matatani na hawa jamaa.

Tiba
 
Asante mkuu nashukuru kwa mchango wako. Sasa wakipakia gari kabla halijapata mteja likifika Bandarini inakuwaje? Wana agent wao hapa Tanzania kweli?

Tiba

Inakaa na ndio maana tra wanapiga mnada coz hazijapata wateja bado, ila kuanzia mwz wa 11 kuna agent alikuwa anatoa anapeleka bond, atleast hiyo inawasaidia wakipata mteja aende akachukulie kule wanaepukana na storage wateja!
 
yah..hawa jamaa kweli ni kampuni ipo na inauza magari na ndege pia. ni kubwa tu but wana tatizo moja na ucheleweshwaji wa kusafirisha gari. Mwaka jana nilinunua gari tika kwao gari ilkaa miezi mitatu ndio ikafika ikiwa haina spea tairi na betri imekufa. So for advice go to another company. Be foward ni wazuri kiutendaji but magari yao yanamikwaruzo sana na yameenda mileage kubwa.
kuna kampuni inaitwa tradecarview wako vizuri sana. nimefanya nao kazi mara mbili bila tatizo lolote.

Mkuu Dikembe,

Asante kwa mchango wako. Kwa hiyo hawa jamaa kwa upande mwingine hawako makini katika biashara yao. Hao be forward hawana aina ya gari ninalolitaka. Ngoja nitembelee hiyo website ya tradecarview.

Tiba
 
Ndio mkuu Abdulhalim, hawa jamaa kama sio wahindi, basi ni wapakistani kwa muonekano wao na lafudhi yao. Be forward hawana hilo gari ninalolitaka kwa sasa. Kwabhiyo mkuu unsnishauri niachane nao hawa jamaa?

Tiba
I hear jamaa wa Pakistan wanatabia ya kukupa gari tofauti na walilokuonesha kwa picha na specs.
 
Back
Top Bottom