Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,605
- 3,176
Wapendwa wana Jamvi,
Niko kwenye mawasiliano na hii kampuni inayojishughulisha na kuuza magari yaliyotumika huko Japan. Wenye hii kampuni ama ni wahindi au Wapakistani. Nimeongea nao kwa simu na kupitia skype pia. Wanataka kuniuzia gari na makubaliano yapo katika hatua za mwisho. Sijawahi kufanya biashara na hawa watu, hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza.
Kwa kuwa pesa itakayotumika kwenye manunuzi ni kubwa, nimeogopa kuendelea na hii deal bila kutafuta ushauri. Je kuna mtu amewahi kufanya nao biashara hawa jamaa? Wako genuine kiasi gani?
Naogopa kuuvaa mkenge mchana kweupeee!!!!!.
Tiba
FEEDBACK:
Kufuatia ushauri wa baadhi ya wadau hapa JF, niliamua kuingia makubaliano ya kununua gari na hawa jamaa wa SBT Japan. Ukweli ni kwamba wako very aggressive business wise na ukijitokeza kuwauliza kitu basi wanakuwa hawako tayari kukupoteza kwa hiyo kila wakati watakupigia simu, watakutumia email, watakutumia message through skype ilimradi wahakikishe wako na wewe karibu. Hali hii ilinitisha na ndio maana nilikuja hapa kuomba ushauri.
Tulikubaliana kwamba niwatumie nusu ya pesa ya gari na wao wakiishaipata wataanza process za kuship gari. Hilo lilifanyika. Walipomaliza shipping process wakanitumia copy ya bill of lading na mimi nikatuma nusu ya pesa zilizokuwa zimebaki. Baada ya kupokea hizo pesa ndio sasa wakanitumia original documents. Jana agent wangu aliniletea gari nyumbani likiwa katika hali nzuri kabisa na ni gari ambalo nilikuwa nimelichagua. Ila hawa jamaa tulitofautiana nao kitu kimoja kidogo. Tulikubaliana bei in dollars na invoice waliyonitumia ilikuwa in dollars. Nilituma pesa in USD lakini wanapozipokea waniambia wamepokea JPY. Matokeo yake at the end of the deal nilijikuta nalipa USD 200 zaidi kutokana na wao kuingiza hizo pesa kwenye JPY account na wala sio USD account. Niliwaambia warekebishe hicho kitu.
Kutokana na hii tabia ya kukubali nusu malipo na ukimalizia malipo ndipo wakutumie original docs, ndio maana magari mengi wanayo yasupply hawa jamaa yanakaa bandarini muda mrefu kwani endapo kwa mfano ukikosea kidogo wakati wa kutuma hela na hizo hela labda zikarudi ndio utume upya, basi unapoteza muda mwingi na wakati huo labda unakuta gari linakuwa tayari limefika bandarini.
Nawashukuru wadau wote waliochangia na kunihakikishia kwamba jamaa ni wazuri na hawatanifanyia utapeli. Kwa kifupi ni kwamba I recommend them in case any one of you want to do business with them.
Cheers,