Credibility Check: SBT Japan Kampuni ya Kuuza Magari


Mi nishafanya nao tena mzigo nimeupata November niliagiza October. Cjaona kama ni wajanja wajanja na kwa kweli gari niloipata iko vizuri saana. Nakushauri endelea nao tu cóż uzuri SBT hii ni site Yap tofauti na Bfoward na Car trade view ambazo ni free site. So u receive what u ordered.
 
Mbona utaji haina ya gari mkuu?au itakua hiyo tu Tanzania mzima
 

Mkuu nakushukuru kwa mchango wako. Nitafuata ushauri wako kwa karibu.

Tiba
 
Mbona utaji haina ya gari mkuu?au itakua hiyo tu Tanzania mzima

Mkuu unataka nikutajie aina ya gari ninalolitaka wewe ni supplier inawezekana unalo?

Tiba
 

Asantr mkuu kwa ushauri.

Tiba
 

Mkuu nitakuPm nikupatie stock number ya hilo gari. Asante kwa kujitokeza kunisaidia.

Tiba
 
Last edited by a moderator:
SBT wako poa niliagiza gari kwao.....lilikuja bila shida yoyote kwa muda ule ule. Tatizo lao wako aggressive sana kwenye mawasiliano........utakuta kwenye simu, email, Skype, Sms etc. Mimi nilikuwa nadeal na Mohamed Afraz.

Mkuu asante kwa mchango wako na ushauri.

Tiba
 
Hawa jama wa SBT ninamiaka karibu 2 nafanya nao kazi mimi huwa nawapa credit kubwa kwasababu wanajua biashara wanaku upadte kila hatua pia hata kama huna haja na gari watakukumbusha tu so wako serious na kazi sio tatizo letu huwa tuanjaribishiwa kufanya biashara kama wewe hapo sasa hivi unapresha kubwa wewe tuma hiyo pesa halafu huyo peter wa SBT ndo manager wao kwa tanzania ndo maana wameona unataka kununua lakini unawasiwasi na hao sales account wako ndo maana anapewa boss wao ajaribu kuzungumuza na wewe pia swala ya kuwa ni wapakstani is not an issue kwasababu mbona afraz nimefanya naye pia kuna dada wa indonesia pia anaitwa Maricon Bais pia anashingilia account za watu hapa tanzania bishara ni matanganzo kama unaogopa kupingiwa simu so watajuaje au watafanyaje biashara you have to know also they doing business sio wanakaa kama sisi hapa bongo unasubiria wateja na biashara yako ya nyanya(Prof muhongo said).
ni pm nikupe direction it so easy to do business online nowdays.
 
SBT ni kampuni nzuri na ya mda mrefu sana,naona kuna bwana hapo juu aliogopa kidogo uliposema uliongea na mpakistani,biashara ya magari Japan na Dubai imeshikiliwa na wa Pakistan hivyo usishtuke,75% ya used car dealers Japani ni wapakistani ukiongea na Mjapani wengi wameajiriwa tu,Dubai AL AWEER ndio sehemu kubwa duniani inayouza magari used ya mkono wa kulia na almost 90%ya showroom ni za wapakistani,kuna siku nilimwuliza jamaa mmoja Dubai kwanini showrooms nyingi ni za wapakistani akaniambia hawa jamaa wanapesa nyingi sana za unga hivyo wengi wao wanaamua waziweke kwenye magari kama biashara(sina uhakika).
Turudi kwenye mada hiyo kampuni ipo na ni nzuri lakini wauza magari wanatabia ya kuchukua order na baada ya hapo wanakutafutia gari wanazunguka minadani mpaka watalipata, na wakilipata watachezea odometer na kusoma KM zozote ambazo mteja anataka.Kuna bwana mmoja hapo juu alisema aliagiza gari wakamwambia lipo UK ni kweli wanafanya hivyo gari linawezakuwa lefthand drive wakabadili likawa righthand drive ndivyo biashara hii ilivyo(sio wote).
Wasiliana nao usiogope kwamba ni wa Pakistani,matatizo ya used cars yapo kwa dealer wengi sana,maana gari zao nyingi ni za ukarabati,niliwashanunua Rav 4 toka kwenye kampuni kubwa sana walisema ni 2004 model lakini baada ya kuikagua chasis nikagundua ni 2002,niliwainunua hiace ikasumbua gearbox baada ya kuifungua nikakuta ilikuwa ya kichina!!!matatizo kwenye used cars yapo,ndio maana njia nzuri ya kununua used car ni kuliona na kulichambua otherwise ni gamble tu.
 

Habari, yeah ni vizuri kuondoa kupata ushauri ili uwe na uhakika ya unachoenda kukifanya. Binafsi hawa jamaa nilikaribia kufanya nao biashara miezi michache iliopita, baadae nilisita baada ya kuona wao wananisumbua sana kwa kunipigia pigia simu kila wakati kama vile wananilazimisha tufikie mwafaka. Sina hakika sana juu ya uaminifu wao lakini sina imani nao kabisa.
Binafsi nimeshanunua gari kwenye kampuni mbili tofauti; ilionivutia zaidi ingawa bei zao ni kama ziko juu ni kampuni ya AUTOREC. Gari zao ni kama mpya, lakini pia wanatoa waranti. Ushauri: Pesa mama ikishakutoka ndio basi tena ni kama maji, kama utaipata basi itakuwa sio ile tena; vizuri uwe na uhakika wa 100% ya unachokwenda kukinunua, rahisi mara nyingi huwa garama zake baadae.
 

Mkuu kwa kauli ya huyo ninaye wasiliana naye hawana agent hapa Tanzania kwa sasa ila wako mbioni kuwa na ofisi. Hata hivyo tumezungumza na kufikia hatua nzuri. Tumekubaliana nitume 50% ya gharama ya gari halafu wao wafanye shipping arrangements. Wakimaliza watanitumia scanned copy ya bill of landing. Nikiishapata hiyo bill of landing na kuhakikisha kwamba gari iliyokuwa shipped ndio hiyo niliyokubaliana nao kununua nitume 50% iliyobaki na wao wanitumie Orginal bill of lading.

Ila jamaa wako aggressive sana katika biashara.

Tiba
 

Yap Tiba, unatoa nusu gari ikifika Dar port unamalizia. Mimi mwenyewe walinifanyia hvo. Pia huwa wananipigia cm kuulizia kama nataka kununua tena. Wako Very serious kufanyafolloup.
 
SBT sio wabaya, sio matapeli pia.
Ila wasumbufu kwenye mawasiliano, wanaweza wakakupigia hata mara 10 kwa siku so inakua kero.
 

Unmaanisha nini hapo kwenye red?
 
Hata mimi niliwakimbia. Hiyo marketing strategy inaleta wasiwasi sana. Nilichagua gari na tukakubaliana. Ikawa simu,email kila siku. Siku nakwenda kudeposit wakapiga simu nipo benki somebody Sande, roho yangu ikaghairi nikaacha.
 
Unmaanisha nini hapo kwenye red?

Namaanisha kuwa, SBT wanauza magari yao kwa kutumia site yao(webpage), wakati Befoward na Car trade view ni free site. Wao wanauza magari ya wateja na wanachukua commission.
 
Namaanisha kuwa, SBT wanauza magari yao kwa kutumia site yao(webpage), wakati Befoward na Car trade view ni free site. Wao wanauza magari ya wateja na wanachukua commission.

be foward sio free site
 
Namaanisha kuwa, SBT wanauza magari yao kwa kutumia site yao(webpage), wakati Befoward na Car trade view ni free site. Wao wanauza magari ya wateja na wanachukua commission.

Ni tradecarview pekee ndiyo hawauzi magari, beforward wanauza magari na ndiyo kampuni inayoongoza kuuza magari used africa kwa sasa, nao pia unaweza kuwapata kwenye website yao Japanese Used Cars | BE FORWARD, ni kampuni kama sbt, na hata sbt nao pia wanauzia tradecarview, autotrader na kwingineko. Ni chaguo la mnunuzi tu, unakoona gari zuri kwa bei umeipenda unanunua kokote.
 
Hata mimi niliwakimbia. Hiyo marketing strategy inaleta wasiwasi sana. Nilichagua gari na tukakubaliana. Ikawa simu,email kila siku. Siku nakwenda kudeposit wakapiga simu nipo benki somebody Sande, roho yangu ikaghairi nikaacha.

Hahahaa, ukaona kama wanakuvuta wakulize?..sbt sijawahi kuskia wameliza mtu pesa, lakini wana mambo yao ambayo yanakera wakati mwingine utafikiri unadeal na kanjanja flani mwenye njaa!
 
Hata mimi niliwakimbia. Hiyo marketing strategy inaleta wasiwasi sana. Nilichagua gari na tukakubaliana. Ikawa simu,email kila siku. Siku nakwenda kudeposit wakapiga simu nipo benki somebody Sande, roho yangu ikaghairi nikaacha.

Customer Service kwenye nchi yetu ipo chini sana,ukiingia dukani mwenye duka anakukodolea macho kama vile umepotea njia,sometime anakuwa busy na game kwenye simu yake,ukitoa pesa bila aibu anakwambia hana chenji!!!wenzetu wanajua umuhimu wa mteja,wanajua bila wewe wao si kitu ata ukienda kwenye malls zao hawatazami una simu gani au umeshuka kwenye gari gani wataonyesha kukujali sana.Ni kweli hao jamaa wanafuatilia sana mteja kwa simu,mails nk.Kwa sisi ambao hatujazoea tunajua tunaibiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…