Zamazamani
JF-Expert Member
- Jun 13, 2008
- 1,869
- 787
Binafsi pia sijawahi kufanya nao biashara,ninachokifahamu ni kwamba,kwakua wanamawasiliano na wewe watakupigia sim kila mara kuulizia umefikia wapi,kwa kweli inahitaji uvumilivu sana mana ni wasumbufu.
Nimewahi kufanya biashara na kampuni nyingine inaitwa Beforward,jamaa wako smart sana.
wadau,naomba kuuliza,kias cha chin kabisa kununua used car kama tax hiv from japan ni tsh ngap?.naomba msaada wenu wadau
Wapendwa wana Jamvi,
Niko kwenye mawasiliano na hii kampuni inayojishughulisha na kuuza magari yaliyotumika huko Japan. Wenye hii kampuni ama ni wahindi au Wapakistani. Nimeongea nao kwa simu na kupitia skype pia. Wanataka kuniuzia gari na makubaliano yapo katika hatua za mwisho. Sijawahi kufanya biashara na hawa watu, hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza.
Kwa kuwa pesa itakayotumika kwenye manunuzi ni kubwa, nimeogopa kuendelea na hii deal bila kutafuta ushauri. Je kuna mtu amewahi kufanya nao biashara hawa jamaa? Wako genuine kiasi gani?
Naogopa kuuvaa mkenge mchana kweupeee!!!!!.
Tiba
FEEDBACK:
Kufuatia ushauri wa baadhi ya wadau hapa JF, niliamua kuingia makubaliano ya kununua gari na hawa jamaa wa SBT Japan. Ukweli ni kwamba wako very aggressive business wise na ukijitokeza kuwauliza kitu basi wanakuwa hawako tayari kukupoteza kwa hiyo kila wakati watakupigia simu, watakutumia email, watakutumia message through skype ilimradi wahakikishe wako na wewe karibu. Hali hii ilinitisha na ndio maana nilikuja hapa kuomba ushauri.
Tulikubaliana kwamba niwatumie nusu ya pesa ya gari na wao wakiishaipata wataanza process za kuship gari. Hilo lilifanyika. Walipomaliza shipping process wakanitumia copy ya bill of lading na mimi nikatuma nusu ya pesa zilizokuwa zimebaki. Baada ya kupokea hizo pesa ndio sasa wakanitumia original documents. Jana agent wangu aliniletea gari nyumbani likiwa katika hali nzuri kabisa na ni gari ambalo nilikuwa nimelichagua. Ila hawa jamaa tulitofautiana nao kitu kimoja kidogo. Tulikubaliana bei in dollars na invoice waliyonitumia ilikuwa in dollars. Nilituma pesa in USD lakini wanapozipokea waniambia wamepokea JPY. Matokeo yake at the end of the deal nilijikuta nalipa USD 200 zaidi kutokana na wao kuingiza hizo pesa kwenye JPY account na wala sio USD account. Niliwaambia warekebishe hicho kitu.
Kutokana na hii tabia ya kukubali nusu malipo na ukimalizia malipo ndipo wakutumie original docs, ndio maana magari mengi wanayo yasupply hawa jamaa yanakaa bandarini muda mrefu kwani endapo kwa mfano ukikosea kidogo wakati wa kutuma hela na hizo hela labda zikarudi ndio utume upya, basi unapoteza muda mwingi na wakati huo labda unakuta gari linakuwa tayari limefika bandarini.
Nawashukuru wadau wote waliochangia na kunihakikishia kwamba jamaa ni wazuri na hawatanifanyia utapeli. Kwa kifupi ni kwamba I recommend them in case any one of you want to do business with them.
Cheers,
Tiba
Hello Tiba: Nipokwenye mazungumzo na hawa jamaa wa SBT ila kabla sijawatumia pesa nikaona nitafute japo some information kuogopa kutapelewa ndipo nilipoikumbuka JF. Naomba unisaidie uzoefu wako wamenipatia namba hii ya akaunti yao
BankName: The Bank of Tokyo-Mitsubishi UFJ,Ltd.
Branch:YOKOHAMA EKIMAE BRANCH
AccountName: SBT CO., LTD.
Accountnumber: 251-0008956BJWHQAI
Alphabetsare your virtual account code to trace out your payment. every customer hasdifferent virtual account number that is ( BJWHQAI )
SwiftCode: BOTKJPJT
ThankYou and Best Regards,
Given by
Faisal Sabir
Mkuu hawawezi kukupa account namba ambayo sio ya kwao au feki. Tatizo lao ni kwamba wao gari wanalitangaza kwa bei in terms of dollars. Lakini wewe ukituma hizo dola zinaenda kuingia kwenye Japanese Yen account as a result kwa kutumia exchange rate ya bank unakuta hizo dola sasa zinakuwa pungufu halafu wanakwambia utume pesa za ziada kujalizia hilo pengo.
Cha msingi waulize kama hiyo account ni ya USD au JPY? Kwa vyovyote waambie utatuma dola kwenye hiyo account lakini wasirudi kwako kukwambia pesa hazitoshi kwani exchange rate difference should not be your problem.
Tupatie feedback ya itakavyo kwenda. Nataka kufanya nao biashara tena lakini nataka kujua kama wameisha jirekebisha kwa upande huo.
Tiba
Naomba contact zao mkulu.beforward ni habari nyingine......very smart....yaani hata mimi ninge ji commit kwa 100% assurance!
Naomba contact zao mkulu.
Tiba Ni kweli ofisi zao (sbt) zipo mtaa wa samora opposite na Ttcl head quarter. Maagent wao wako fresh with full info. about japan cars.Kwa sasa nasikia wana agent na ofisi zipo mtaa wa Samora according to one JF member. Mimi binafsi sijaziona hizo ofisi za huyo agent.
Tiba
Tiba Ni kweli ofisi zao (sbt) zipo mtaa wa samora opposite na Ttcl head quarter. Maagent wao wako fresh with full info. about japan cars.
Nimerudi kutoa mrejesho kama ulivyoniomba Tiba. Nimepokea gari wiki mbili zilizopita, SBT wako vizuri in customer caring nimepigiwa simu mpaka zingine nikawa napotezea. Na wameniambia wanaomba wanipigie mwaka mzima ili kufahamu kama gari inafanya kazi vizuri tumekubaliana once a month. Nashukuru kwa taarifa za awali mlizonihakikishia juu ya kampuni hii. I wish to recommend this company to anyone looking used vehicle from Japan. Thanks Tiba and others.