Credibility Check: SBT Japan Kampuni ya Kuuza Magari

Credibility Check: SBT Japan Kampuni ya Kuuza Magari

Binafsi pia sijawahi kufanya nao biashara,ninachokifahamu ni kwamba,kwakua wanamawasiliano na wewe watakupigia sim kila mara kuulizia umefikia wapi,kwa kweli inahitaji uvumilivu sana mana ni wasumbufu.
Nimewahi kufanya biashara na kampuni nyingine inaitwa Beforward,jamaa wako smart sana.

beforward ni habari nyingine......very smart....yaani hata mimi ninge ji commit kwa 100% assurance!
 
wadau,naomba kuuliza,kias cha chin kabisa kununua used car kama tax hiv from japan ni tsh ngap?.naomba msaada wenu wadau
 
Wadau nimerudi hapa jamvini kutoa feedback kama nilivyoahidi. Hawa jamaa wako safi na kibiashara wako very aggressive na hivyo unaweza kufikiri wanajaribu kukuingiza chaka kumbe nia yao ni kutotaka kumpoteza mteja yeyote anaye wanasiliana nao.

Tiba
 
mimi sina hamu nao, kama walivyoeleza wenzangu hapo juu, walionyesha wana magari stock ya Dar, nikapenda gari wakanitumia invoice, wakti wote huo hawakuwa wanasema chochote zaidi ya kunambia hii gari iko dar utaipata ndani ya siku moja. na hayakuwa mawasiliano ya muda mfupi kama siku moja au mbili ilikuwa ni wiki mbili. nilipotuma hela tu walipoipata, ndo wananambia inadaiwa storage fee dola 950, namuuliza mtu wa TRA ananambia storage fee ni dola 12 kwa siku, kuna uwezsekano hizo dola 950 ikawa kidogo kwani lina zaidi ya miezi 3, nikawambia mbona hamkusema tangu mwanzo? hii ni flaud. baada ya kusumbuana sana ndo wakakubali kunitumia gari lingine toka japani kwa bei na aina ile ile.

wakatuma, lakini nadhani kwa makusudi, hawakutuma export inspection certificate wala JAAI certificate of appraisal, kitu kinachopelekea upigwe faini na TBS kwa kuingiza gari bila kukaguliwa, kuwauliza wakanambia ni kweli halikukaguliwa kwa sababu tulikupatia gari hilo kwa hasara kubwa. Hivyo binafsi sina zuri kwao.
 
Hello Tiba: Nipokwenye mazungumzo na hawa jamaa wa SBT ila kabla sijawatumia pesa nikaona nitafute japo some information kuogopa kutapelewa ndipo nilipoikumbuka JF. Naomba unisaidie uzoefu wako wamenipatia namba hii ya akaunti yao

BankName: The Bank of Tokyo-Mitsubishi UFJ,Ltd.
Branch:YOKOHAMA EKIMAE BRANCH
AccountName: SBT CO., LTD.
Accountnumber: 251-0008956BJWHQAI
Alphabetsare your virtual account code to trace out your payment. every customer hasdifferent virtual account number that is ( BJWHQAI )
SwiftCode: BOTKJPJT

ThankYou and Best Regards,

Given by

Faisal Sabir

Wapendwa wana Jamvi,

Niko kwenye mawasiliano na hii kampuni inayojishughulisha na kuuza magari yaliyotumika huko Japan. Wenye hii kampuni ama ni wahindi au Wapakistani. Nimeongea nao kwa simu na kupitia skype pia. Wanataka kuniuzia gari na makubaliano yapo katika hatua za mwisho. Sijawahi kufanya biashara na hawa watu, hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza.

Kwa kuwa pesa itakayotumika kwenye manunuzi ni kubwa, nimeogopa kuendelea na hii deal bila kutafuta ushauri. Je kuna mtu amewahi kufanya nao biashara hawa jamaa? Wako genuine kiasi gani?

Naogopa kuuvaa mkenge mchana kweupeee!!!!!.

Tiba

FEEDBACK:

Kufuatia ushauri wa baadhi ya wadau hapa JF, niliamua kuingia makubaliano ya kununua gari na hawa jamaa wa SBT Japan. Ukweli ni kwamba wako very aggressive business wise na ukijitokeza kuwauliza kitu basi wanakuwa hawako tayari kukupoteza kwa hiyo kila wakati watakupigia simu, watakutumia email, watakutumia message through skype ilimradi wahakikishe wako na wewe karibu. Hali hii ilinitisha na ndio maana nilikuja hapa kuomba ushauri.

Tulikubaliana kwamba niwatumie nusu ya pesa ya gari na wao wakiishaipata wataanza process za kuship gari. Hilo lilifanyika. Walipomaliza shipping process wakanitumia copy ya bill of lading na mimi nikatuma nusu ya pesa zilizokuwa zimebaki. Baada ya kupokea hizo pesa ndio sasa wakanitumia original documents. Jana agent wangu aliniletea gari nyumbani likiwa katika hali nzuri kabisa na ni gari ambalo nilikuwa nimelichagua. Ila hawa jamaa tulitofautiana nao kitu kimoja kidogo. Tulikubaliana bei in dollars na invoice waliyonitumia ilikuwa in dollars. Nilituma pesa in USD lakini wanapozipokea waniambia wamepokea JPY. Matokeo yake at the end of the deal nilijikuta nalipa USD 200 zaidi kutokana na wao kuingiza hizo pesa kwenye JPY account na wala sio USD account. Niliwaambia warekebishe hicho kitu.

Kutokana na hii tabia ya kukubali nusu malipo na ukimalizia malipo ndipo wakutumie original docs, ndio maana magari mengi wanayo yasupply hawa jamaa yanakaa bandarini muda mrefu kwani endapo kwa mfano ukikosea kidogo wakati wa kutuma hela na hizo hela labda zikarudi ndio utume upya, basi unapoteza muda mwingi na wakati huo labda unakuta gari linakuwa tayari limefika bandarini.

Nawashukuru wadau wote waliochangia na kunihakikishia kwamba jamaa ni wazuri na hawatanifanyia utapeli. Kwa kifupi ni kwamba I recommend them in case any one of you want to do business with them.

Cheers,

Tiba
 
Hello Tiba: Nipokwenye mazungumzo na hawa jamaa wa SBT ila kabla sijawatumia pesa nikaona nitafute japo some information kuogopa kutapelewa ndipo nilipoikumbuka JF. Naomba unisaidie uzoefu wako wamenipatia namba hii ya akaunti yao

BankName: The Bank of Tokyo-Mitsubishi UFJ,Ltd.
Branch:YOKOHAMA EKIMAE BRANCH
AccountName: SBT CO., LTD.
Accountnumber: 251-0008956BJWHQAI
Alphabetsare your virtual account code to trace out your payment. every customer hasdifferent virtual account number that is ( BJWHQAI )
SwiftCode: BOTKJPJT

ThankYou and Best Regards,

Given by

Faisal Sabir

Mkuu hawawezi kukupa account namba ambayo sio ya kwao au feki. Tatizo lao ni kwamba wao gari wanalitangaza kwa bei in terms of dollars. Lakini wewe ukituma hizo dola zinaenda kuingia kwenye Japanese Yen account as a result kwa kutumia exchange rate ya bank unakuta hizo dola sasa zinakuwa pungufu halafu wanakwambia utume pesa za ziada kujalizia hilo pengo.

Cha msingi waulize kama hiyo account ni ya USD au JPY? Kwa vyovyote waambie utatuma dola kwenye hiyo account lakini wasirudi kwako kukwambia pesa hazitoshi kwani exchange rate difference should not be your problem.

Tupatie feedback ya itakavyo kwenda. Nataka kufanya nao biashara tena lakini nataka kujua kama wameisha jirekebisha kwa upande huo.

Tiba
 
nilijua kuwa hawa jamaa wako na agent hapo dar!! Ama ni story tu????
 
Nashukuru kwa anagalizo na nitatoa mrejesho. Kila la kheri

Kwa sasa nasikia wana agent na ofisi zipo mtaa wa Samora according to one JF member. Mimi binafsi sijaziona hizo ofisi za huyo agent.

Tiba
 
Jamani kuna Autocom Japan, it's new company but very smart
 
Kwa sasa nasikia wana agent na ofisi zipo mtaa wa Samora according to one JF member. Mimi binafsi sijaziona hizo ofisi za huyo agent.

Tiba
Tiba Ni kweli ofisi zao (sbt) zipo mtaa wa samora opposite na Ttcl head quarter. Maagent wao wako fresh with full info. about japan cars.
 
Last edited by a moderator:
Tiba Ni kweli ofisi zao (sbt) zipo mtaa wa samora opposite na Ttcl head quarter. Maagent wao wako fresh with full info. about japan cars.

SBT generally ni wazuri kwani uwa wananipigia simu kuniuliza performance ya gari waliloniuzia. Kwa sasa mwaka umepita lakini bado wanafuatilia. Kwa hilo nawapa credit.

Tiba
 
Last edited by a moderator:
Nimerudi kutoa mrejesho kama ulivyoniomba Tiba. Nimepokea gari wiki mbili zilizopita, SBT wako vizuri in customer caring nimepigiwa simu mpaka zingine nikawa napotezea. Na wameniambia wanaomba wanipigie mwaka mzima ili kufahamu kama gari inafanya kazi vizuri tumekubaliana once a month. Nashukuru kwa taarifa za awali mlizonihakikishia juu ya kampuni hii. I wish to recommend this company to anyone looking used vehicle from Japan. Thanks Tiba and others.
 
Mkuu Bhageshi,

Asante kwa mrudisho nyuma juu ya hii Kampuni. Kwa kweli when it comes to customer care they are more than good. Mimi kwa siku hizi za hivi karibuni hawajanipigia kuulizia performance ya gari lakini wananipigia kunishawishi ninunue gari lingine kutoka kwao. Nikipata pesa na nikahitaji gari, sitasita kufanya nao biashara. Na gari waliloniuzia performance yake ni super. Sasa nina mwaka nalo, hakuna shida yoyote iliyojitokeza ni kupiga mwendo tu.

Kama ulivyosema, na mimi sisiti kufanya recommendation kwa yoyote anayetaka gari kudeal na hawa jamaa.

Tiba
 
Back
Top Bottom