Crescentius Magori afafanua masharti magumu ya FIFA kwa wachezaji waliobadili Uraia ili waweze kucheza Timu ya Taifa

Crescentius Magori afafanua masharti magumu ya FIFA kwa wachezaji waliobadili Uraia ili waweze kucheza Timu ya Taifa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Crescentius Magori, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, ametoa ufafanuzi muhimu kuhusu mchakato wa kubadilisha uraia ili wachezaji waweze kucheza katika Timu ya Taifa ya Tanzania.

Kupitia ujumbe, Magori amesisitiza kuwa wachezaji wenye uraia wa nchi mbili wanapaswa kukidhi masharti magumu yaliyowekwa na FIFA.

Ameeleza kuwa, kwa mujibu wa kanuni za FIFA za mwaka 2020 zinazojulikana kama "wholesale modernisation," mchezaji lazima awe ameishi nchini kwa kipindi kisichopungua miaka mitano, na mzazi mmoja angalau awe raia wa Tanzania, pamoja na vigezo vingine.
IMG_2711.jpeg

Soma, Pia:

- Idara ya uhamiaji yatoa ufafanuzi dhidi ya wachezaji wa kigeni Singida Black Stars, wote ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi

- Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni
 
Kuna watu ni washamba wa pesa. Niliwahi kusema pamoja na madaraka, vyeo na pesa ila ukiwaangalia tu bado unaona kuna kaushamba wako nako na hakatakuja kuwaondoka.

Una wachezaji 12 wa kigeni unashindwa kufanya vizuri, unashindwa kuheshimu makocha wako unadhani ukifikisha wachezaji 16 wa kigeni (kwa kunajisi sheria za nchi za uhamiaji) ndiyo muujiza utatokea?

Una vijana wametapakaa nchi nzima hawana ajira za maana ila wenye vipaji vya mpira, umeshindwa kuwekeza kwenye michezo mashuleni, kwenye academies, kwenye viwanja vya kisasa mitaani na maeneo yao, leo unaamka tu kisa una access na pesa unaenda kuokota Waafrika wenzio waje wakupe miujiza ndani ya miaka 2 ili upate mtaji wa kisiasa.
 
Mbantu anaitwa 'Crescentius'. Dah, wazungu wametushika pabaya.

Samahani waungwana..nimetoka nje ya mada kidogo.
 
Asa wao ndio washika dau waambiane haya kwenye vikao vyao
Team ya taifa imeenda afcon bila hao wageni kwa Nini waone umuhimu wao Sasa kama sio siasa za mpira!?
Ukiongozwa na wahuni wanaodhani wanaweza kufanya lolote na kwamba sheria haziwahusu wao utashangaa yale yaliyomo vichwani mwao na wanayodiriki kufanya.

Hawashindwi kutengeneza taarifa feki za mzazi wa mchezaji wakiona hilo linatosha kukidhi vigezo. Mengine tutaambiwa tuwe wazalendo.
 
Kuna watu ni washamba wa pesa. Niliwahi kusema pamoja na madaraka, vyeo na pesa ila ukiwaangalia tu bado unaona kuna kaushamba wako nako na hakatakuja kuwaondoka.

Una wachezaji 12 wa kigeni unashindwa kufanya vizuri, unashindwa kuheshimu makocha wako unadhani ukifikisha wachezaji 16 wa kigeni (kwa kunajisi sheria za nchi za uhamiaji) ndiyo muujiza utatokea?

Una vijana wametapakaa nchi nzima hawana ajira za maana ila wenye vipaji vya mpira, umeshindwa kuwekeza kwenye michezo mashuleni, kwenye academies, kwenye viwanja vya kisasa mitaani na maeneo yao, leo unaamka tu kisa una access na pesa unaenda kuokota Waafrika wenzio waje wakupe miujiza ndani ya miaka 2 ili upate mtaji wa kisiasa.
Ni ushamba na upumbavu, upumbavu ni kipaji, mpumbavu ni mtu aliyebobea kwenye jambo fulani halafu hufanya tofauti na weledi kwa kulazimisha wengine wafikiri anavyotaka yeye
 
Tanzania imeenda afcon
Under 17
Under 20
Wakubwa
Wanawake
Na beach Soka
Sioni sababu ya kwenda kuhangaika na wageni
Tukiwa na grassroots programs nzuri tunaweza kupata wachezaji wengi wazuri
Wavivu wa kufikiri hulazimisha njia za mkato kwa masilahi binafsi mimi nimefuatilia kwakina kuhusu yasiyotarajiwa, (uncertainty), husabisha changamoto, yasiyotarajiwa husabishwa na 1. Taarifa. 2. Majanga. 3. Binadamu

1. Kuhusu taarifa unaweza pata taarifa sahihi lakini kama uwezo wako wa kutafsiri taarifa ni mdogo itakusabishia changamoto

2. Kuhusu majanga huwezi kuchomoka yapo ya Kimungi halafu ya kibinadamu, mfano hai wa kibinadamu gorofa lililo dondoka kariakoo hivi karibuni

3. Kuhusu binadamu, binadamu hujisabishia changamoto kwa ujinga, uzembe, uvivu, ulevi, ushamba, wivu, upumbavu ongeza tabia nyingine za hovyo za binadamu, pia huyo huyo binadamu huwasabishia wengine changamoto bila kujua ama kwa bahati mbaya na kwa makusudi rejea watu wasiojulikana

Hitimisho changamoto nyingi tunakumbana nazo katika maisha yetu ya kila siku zinasababishwa na binadamu
 
Sasa wee Magori hebu tuambie huyo Kibu Dennis wenu anazaidi ya miaka mitano hapa nchini ? Naj ee ana mzazi hapa TZ ??? Mbona yumo timu ya Taifa ??? N a alishaanza kucheza siku nyingi tuu !Acheni ujinga !!!
 
Mbantu anaitwa 'Crescentius'. Dah, wazungu wametushika pabaya.

Samahani waungwana..nimetoka nje ya mada kidogo.
City Owl ! Anamshangaa Crescentius ,Ungejiita Chikandanga Hapa Jf Ungekuwa Na Kila Haki Ya Kushangaa Hilo Jina Ila Kwa Sasa Kaa Kimya Na Usiseme Chochote.
 
Benny Haraba kaka nimesoma comments zako...ila sijakuelewa kuwa unaungana na mada au unaipinga? Yani unawasapport hao wanaowapa uraia wageni au unatushangaa tunaowaona hawajafanya vzr...
 
Mbantu anaitwa 'Crescentius'. Dah, wazungu wametushika pabaya.

Samahani waungwana..nimetoka nje ya mada kidogo.
Sawa City Owl, sijajua ID yako kwa kibantu maana yake ni nini
 
Back
Top Bottom