Cristiano Ronaldo Akubali Yaishe, Huu Ndio Mwaka wake wa Mwisho

Cristiano Ronaldo Akubali Yaishe, Huu Ndio Mwaka wake wa Mwisho

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Cristiano Ronaldo ametoa kauli inayoweza kuwa ishara kubwa ya mwisho wa safari yake ya soka, akisema mwaka 2026 huenda ukawa mwaka wake wa mwisho kucheza soka la kulipwa.

Akizungumza katika mahojiano na jarida la Vogue, nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 amesema:

“Huenda huu ukawa mwaka wangu wa mwisho katika soka. Nataka kuacha urithi wa ajabu. Tayari nina mipango yote ya maisha yangu ya baadaye.”

Ronaldo amesema tayari ana picha kamili ya maisha yake baada ya soka, akitarajia kutumia muda zaidi kusafiri, kuwa na familia yake na kufurahia michezo mingine kama padel.

Kauli hiyo imezua gumzo kubwa duniani, huku Ronaldo akiwa bado anaendelea kuichezea Al-Nassr na akiwa katika harakati za kufikia rekodi ya mabao 1,000 katika maisha yake ya soka.

1786970878397.png
 
Kama vipi mabeki wa Uarabuni wamkazie asifikishe hayo magoli yake 1000 anayotaka kuyafikia, halafu tuone kama atastaafu.
Kwa msimu huu hafiki izo goli labda asogeze mbele kustafu
 
Bado magoli 24 GOAT afikishe 1000. Wasimchoshe, wampe penati zake 15 na magoli ya tap-in 9. Tayari ni Legend. Kombe la dunia atabeba akiwa kocha wa Ureno au Brazil
 
Eeh hii story ya Ronaldo inauma kweli, lakini mabeki wa Uarabuni wamemaliza kazi kama wamemfanya akae kimya. Huyo mzee bado ana njaa ya goli, lakini akifikisha 1000 atakaa tu kwenye sofa akitazama mechi za zamani. Lol, mwaka 2026 ni mbali, tutaonana hapo!
 
Maisha yapo kasi sana aisee yaani rinaldo huyu anastaafu soka daah
 
Back
Top Bottom