Cristiano Ronaldo anataka kuichezea Atletico Madrid, anamshawishi Simeone amsajili

Cristiano Ronaldo anataka kuichezea Atletico Madrid, anamshawishi Simeone amsajili

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Capture.JPG
Imeripotiwa kuwa Cristiano Ronaldo, 37, anamshawishi Kocha Diego Simeone ili amsajili kwa ajili ya kuichezea Atletico Madrid msimu ujao.

Ronaldo anataka kuondoka Manchester United ilia pate nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, tayari timu za Chelsea na Bayern Munich zilizotajwa kumuwania zimetamka kuwa hazina mpango wa kumsajili.

Ikiwa itakuwa hivyo atarejea Madrid ambapo akiwa hapo alikuwa kiichezea Real Madrid, akifunga magoli 311 katika mechi 292 za LaLiga kati ya mwaka 2009 hadi 2018 pia alishinda mataji manne ya Ligi ya Mabingwa.

=============================


Cristiano Ronaldo set for Atletico Madrid transfer after wantaway Man Utd star ‘convinces Simeone to sign him’

CRISTIANO RONALDO has reportedly convinced Diego Simeone to bring him to Atletico Madrid.

The Portuguese forward, 37, is desperate to leave Manchester United this summer and play Champions League football.

Ronaldo still has one year remaining on his Old Trafford contract but is yet to return for pre-season training with the Red Devils.

However, the veteran has found that interest in him is not as high as he anticipated with a number of clubs ruling themselves out of the running to sign him.

Both Chelsea and Bayern Munich have declared that they are not interested, while the star himself has zero interest in taking up a lucrative offer from an unnamed Saudi Arabian club.

However, Spanish outlet Diario AS are now claiming that Ronaldo could be about to return to Spain with Atletico Madrid.

He shot to superstardom with their rivals Real Madrid, scoring 311 goals in 292 LaLiga matches between 2009 and 2018 and won the Champions League four times.

And that made him public enemy No1 with their neighbours Atletico - but now he could be about to sensationally join them.

The report states that his representatives have spoken with Atletico boss Simeone and persuaded him to make a move to get Ronaldo back to Madrid.

It also adds that Simeone loves Cristiano and has always called him the “number 1” player.

Source: The Sun
 
Link ipo chini, katazame huko youtube, like na u subscribe asante sana.

Filamu Pictures, wanawaletea kazi ya filamu ya kitanzania iitwayo PETE

Kutana na Bwana Lidawi, mvuvi mwenye hali ngumu na mke mgonjwa na jinsi anavyoingia matatizoni kutokana na pete ya maajabu iliyofika katika ulimwengu wa wanadamu kwa ajili ya kazi maalum

Kutana na Bwana Songolo mtu tajiri, mkorofi na mkali sana, ambaye nae anajikuta yuko katikati ya mikasa hiyo ipatayo bwana Lidawi

Karibuni
 
Mliowahi kumshauri Ronaldo aondoke Madrid aende akatafute challenge kwingineko (mkiamini alikuwa greatest na angefit popote pale ukilinganisha na Messi) mje muendelee kumshauri ujinga wenu tena.
Usifikiri CR7 watu awamtaki tatizo mshahara wake na timu nyingi zime athirika ki uchumi na COVID.
Msimu uliopita alikua na Goli 20 mguuni anawazidi washambuliaji wengi tu.
 
Mliowahi kumshauri Ronaldo aondoke Madrid aende akatafute challenge kwingineko (mkiamini alikuwa greatest na angefit popote pale ukilinganisha na Messi) mje muendelee kumshauri ujinga wenu tena.
Kwan hata Messi angeenda Man U, angefanya nn? Tatizo sio kiwango cha Ronaldo, tatizo ni team aliyopo. Pia mshahara wake watu hawawezi kulipa.
 
Kwan hata Messi angeenda Man U, angefanya nn? Tatizo sio kiwango cha Ronaldo, tatizo ni team aliyopo. Pia mshahara wake watu hawawezi kulipa.
Unachosema ni sahihi, ila ingekuwa poa Ronaldo angebaki na kustaafia Madrid,bila kutaka mshahara mkubwa sana.Hiyo ingemsaidia kuweka marecord mengine kibao na hata kuheshimiwa zaidi (kuwa a legend of the legends) pale Madrid. Wachezaji wanoamuaga kubaki na timu moja huwa siyo wajinga. Ona sasa anavyoaibika!
 
Ukiachana na mshahara tatizo kubwa cr7 ni taasisi, ukimsajili umesajili taasisi inayokuja na masharti yake. Kuwa kocha wa team yenye ronaldo si kazi rahisi, wakati mwingine inakuondolea ujasiri wa kuikaripia timu kwa kiwango unachotaka pale cr7 anapokuwa sehemu ya timu kutokana na ukubwa na heshima aliyojijengea. Ni mtu ambaye anaweza kusikilizwa na umiliki wa timu na kocha ukawa matatani.
 
Back
Top Bottom