Cristiano Ronaldo anataka kuichezea Atletico Madrid, anamshawishi Simeone amsajili

Kama ataenda Atletico Madrid ndio ataenda kuwavuruga mashabiki wa Real Madrid hawatataka kumuona tena wala kumsikia.

Lile jina lote alilotengenezea pale Real Madrid litaenda kuondoka, asiombe akanyage Santiago Bernabeu, bora aende huko Saudia, na sijui atabaki vipi Man Utd kwa huu ujuaji wake aliouonesha.

Kama vipi aje kutuomba Msimbazi tupo CAF Champions League, atasifika zaidi duniani kwa kucheza Klabu Bingwa za mabara mawili tofauti.
 
Watu mapovu yanawatoka hatari kwenye habari za udaku, Yani unaona source The Sun ila watu wamekaza kumchamba Ronaldo

Kwa mtu anaefatilia mpira tu ata Kwa kiasi, hawezi kukubali eti Ronaldo atataka kwenda AT Madrid, Kwanza Kwa sababu Ronaldo ni Legend wa Real Madrid, hii tu inatosha kuonesha kuwa ni udaku

Lakini kama hiyo haitoshi At Madrid hawana uwezo wa kumlipa Ronaldo, Team zenye uwezo wa kumlipa jamaa ni chache sana huko ulaya, na nyingi zinaogopa maana zitaharibu salary scale ya taasisi

Na sababu ya mwisho, jamaa arudi Laliga ili akaprove nini tena? Yani arudi sehemu alichocheza Kwa miaka zaidi ya 8 kwakuwa alisahau kipi?

Naona kuna Team Messi kaamua kuwa kama Juma lokole, anatembeza michambo tu Kwa Ronaldo kila baada ya comments kadhaa anarudi tena kutumia maneno mapya [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kwavyovyote vile ronaldo umri umeshaenda.Ata angebaki timu moja usitegemee angekua na kubwa zaidi ya hapo alipofikia kwa umri wake.Mengine ni mitizamo tu ya mashabiki ambayo hayana uhalisia.Wakati ni ukuta.
 
Mbna Messi hajabaki Barca ili aweke hiyo legacy? Na kuwa Legend of the legends, Tena yeye ndo alitokea academy ile ile, kwann alitoka si ili maslahi yawepo anavyotaka? Useme tyuuu kwamba CR7 alibugi step kujoin Manyua, angeenda pale city mbna fresh, maana yeye lengo lake ni kucheza UCL ndo maana anahangaika hivi.
 
Lakin si tulielewana Ronaldo ni jeshi la mtu mmoja, Messi anawategemea Xavi na Iniesta
Yes CR7 ni jeshi la mtu m1, na amesha prove hilo. Wala hakna ubishi juu yake, lengo la Ronaldo ni kucheza UCL msimu huu, ndo maana anatafuta team inayoshiriki, sasa tatizo ni mshahara watu hawawezi kulipa.

Kuhusu kiwango, yuko vizuri, tena form boraa, na class kubwaa.
 
Una kipaji cha kuuguza mgonjwa,unatia matumaini pasipo na matumaini,
CR7 asubiri UEFA tu ila asisahau kua anamuangalia Messi kwenye UCL.
 
Tukubali kuwa R7 amefikia mahali pa kujitembeza kwa mujibu wa mithali isemayo; "kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza". Kama mshabiki kindakindaki wa Ronaldo imeniuma sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…