Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Itakumbukwa Ronaldo Ronaldo ameshinda mataji mawili makubwa kwa ngazi ya kimataifa baada ya kuiongoza Ureno kutwaa EURO 2016 sambamba na kutwaa taji la UEFA Nations League 2019.
Baada ya mchezo huo Ronaldo amedai eti hazitafuti rekodi bali rekodi zinamuandama” na kubainisha kuwa kushinda EURO na Ureno ni sawa na kushinda KOMBE LA DUNIA.
Soma Pia: Maajabu ya Cristiano Ronaldo, afikisha magoli 900 michuano rasmi
Mshindi huyo mara 5 wa Ballon d’or alifunga bao lake la kihistoria katika dakika ya 34 ya mchezo kwenye michuano ya Ligi ya Mataifa Ulaya kati ya Ureno dhidi ya Croatia mjini Lisbon, Ureno.