Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
...na kushinda kombe la Dunia ni sawa na kushinda nini?Baada ya kufunga magoli 900 na kuwa mwanasoka wa kwanza kufanya hivyo Cristiano Ronaldo amesema Timu yake ya Taifa kushinda Euro ni sawa na kushinda Kombe la Dunia tu, huku akibainisha kuwa tayari ameshinda mataji mawili akiwa na Ureno ambayo aliyataka sana.
Itakumbukwa Ronaldo Ronaldo ameshinda mataji mawili makubwa kwa ngazi ya kimataifa baada ya kuiongoza Ureno kutwaa EURO 2016 sambamba na kutwaa taji la UEFA Nations League 2019.
Baada ya mchezo huo Ronaldo amedai eti hazitafuti rekodi bali rekodi zinamuandama” na kubainisha kuwa kushinda EURO na Ureno ni sawa na kushinda KOMBE LA DUNIA.
Soma Pia: Maajabu ya Cristiano Ronaldo, afikisha magoli 900 michuano rasmi
Mshindi huyo mara 5 wa Ballon d’or alifunga bao lake la kihistoria katika dakika ya 34 ya mchezo kwenye michuano ya Ligi ya Mataifa Ulaya kati ya Ureno dhidi ya Croatia mjini Lisbon, Ureno.