Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Dada yake Cristiano Ronaldo, Katia Aveiro, amesema kuwa nahodha huyo wa Ureno anakaribia kuaga rasmi timu ya taifa baada ya Kombe la Dunia 2026.
Akizungumza na Sport TV, Katia amesema:
“Kwa taarifa nilizonazo, huu utakuwa mwisho wake. Furahieni kumtazama akiwa bado uwanjani. Sio kwamba ataaga leo, lakini muda huo unakaribia. Ninaamini huu ndio mwisho wa safari yake na timu ya taifa.”
Soma: Cristiano Ronaldo amefikisha jumla ya mabao 975 katika maisha yake ya soka
Endapo itakuwa hivyo, Ronaldo atahitimisha safari yake ya zaidi ya miaka 20 akiwa ameweka rekodi nyingi na kuiongoza Ureno kutwaa mataji makubwa, ikiwemo Euro 2016 na UEFA Nations League 2019.