Mkuu kama ulivyosema
G. O. A. T ni abbreviation ya Greatest of All Time ambapo kiswahili chake ni Bora kwa muda wote
Hapa tunaongelea mchezaji/wachezaji wa soka, hivyo tunaongelea wachezaji bora wa muda wote
Kwa uelewa wangu Wachezazaji/Mchezaji Bora wa Muda/Wakati Wote ni wale wachezaji ambao kwa uwezo walionao/waliowahi kuwa nao iwe karne ya 5, iwe karne 10 iwe karne ya 20 ama karne ya 21 wataendelea kuimbwa mpaka pasipo ukomo.
Ni wale wachezaji ambao kwa uwezo wao wangeweza ku shine miaka 1950,miaka 1970, miaka ya 2000 ama miaka ya 2050. Hawa ni wachezaji ambao pengine hutokea baada ya kitambo kupita, mfano baada ya miaka 100 au 200 wanatokea mara moja (japo enzi za CR7 na Messi zimetoa exceptional). Hawa wachezaji huwezi kuwapata mara kwa mara.
Hawa ni wachezaji ambao walicheza mpira miaka 100 iliyopita lakini kupata habari zao au kuwasikia sio mpaka u Google, automatically wanatajwa tu, likitokea jambo flani kwenye soka anatajwa... Lisipotokea jambo flani kwenye soka anatajwa. Huyo/hao ni Greatest Players of All Time kwa mtazamo wangu.
Sent from my JKM-LX1 using
JamiiForums mobile app