manchoso
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 1,605
- 2,055
Nilikuwa namuangalia Cristiano Ronaldo katika mechi ya kufuzu Russia2018 kati ya Ureno na Uswiswi na ukweli ni kuwa anaelekea katika kumalizia maisha yake ya soka,huyu wa leo sio yule niliemzoea aliekua na kasi isiyomithilika, anaoneka kuchoka na kasi kupungua labda huu msimu/msimu ujao unaweza ukawa msimu wa mwisho wa kumuona akiwa juu katika ubora wake.
lakini nachotaka kusema kueleza hapa vijana tuna mengi ya kujifunza kutoka katika maisha ya Cristiano Ronaldo.
SOKA
Sahau kuhusu Messi,Zidane,R.de lima,Baggio,Gaucho,Rivaldo, Pele wala Maradona.Cristiano ndie mchezaji bora zaidi ambae nimebahatika kumuona sababu hao niowataja juu naamini walizaliwa na vipaji vyao ila ronaldo ni (self made) amejitengeneza mwenyewe kutokana na juhudi kujituma na kujiamini
Raul Gonzalez alipata kusema ipo siku alimuona Messi akikimbia na mpira na ule mpira ukaonekana kama vile umegandishwa na gundi mguuni kwake,ni kweli sababu Messi amezaliwa na kipaji ni raha kumuangalia ila Cristiano ni mtu wa kutumia nguvu kasi na mviziaji mzuri sana. Ronaldo hakuwa na kipaji kama mawinga Lopez,Ginola, Overmars,Duff, Robben.Figo au Quaresma n.k lakini amewapita wote hao kwa mafanikio sababu ya kujtuma na kuishi kwa malengo
Wayne Rooney katika kitabu chake ''my decade in the premier league''
Anamzungumzia Ronaldo kama ''mtu mmoja bishoo mno na ana kioo karibu na kiti cha kubadilishia nguo old traford na kabla ya mechi au mazoezi ni lazima ajiangalie na kujiweka vizuri nywele zake kabla ya kuingia uwanjani'' lakin anampongeza kwa kusema hajapata kuona dunian mtu anaejiamini kama Cristiano Ronaldo
''Nakumbuka aliwahi kutumbia mazoezini nataka kuwa mchezaji bora wa dunia na baada ya kurudi toka katika world cup 2006 nikaona haswa mabadiliko na kujituma kwa Cristiano na akaacha yale madoido yake uwanjani na chenga nyingi na akafocus katika kufunga magoli na kushinda mechi'' maneno hayo aliyasema rooney miaka mingi iliopita na leo hii Cristiano Ronaldo ana tunzo 4 za ballon d'or!!!
Na mafanikio hayo ya Ronaldo hayakuja kama mvua bali amevumilia mengi matusi na kelele za mashabiki vichaa wa uingereza kila wiki hasa baada ya kumsababishia kadi wayne Rooney katika world cup 2006 na wengi walidhani asingerudi uingereza,lakini hakujali maneno ya watu akaja kutengeneza partnership ya hatari pamoja na Rooney Tevez akiwapa Man U mataji matatu ya Barclays na taji moja la Uefa Champions League,ni winga wa kwanza katika historia kuweza kufunga magoli 42 katika mashindano yote na magoli 31 Barcalys premier league akiifikia record iliyowekwa miaka 12 nyuma na mshambuliaji wa kati Allan Shearer!!!!
Kisha akaenda Spain kwa rekodi ya dunia wakati huo paundi million 80 na Florentino Perez akasema wazi ''tumemnunua Ronaldo ili kuja kuumaliza ufalme wa Barcelona'' ambayo ilikuwa inaonekana haishindiki wakati huo Xavi,Iniesta na Messi wako katika kilele cha ubora wao na ikaonekana Barca ingekuja kutawala miaka mingi kutokana na kuwa na vijana wengine wenye vipaji kutoka la masia kwa hiyo ikaonekana Ronaldo kuumaliza ufalme wa la masia itakuwa ndoto.
La liga haikuwa rahisi kwani kila wiki alikuwa pia anazomewa na mashabiki wa timu pinzani wakimuona yupo mbali sana kujifananisha na kuufikia uwezo wa Messi, na wakati mmoja alihojiwa na muandishi wa habari anajisikiaje anapozomewa namna hiyo akasema yeye anapenda kuzomewa sababu hilo ndilo linalompa nguvu zaidi na kumfanya ajitume
Ronaldo hajamuangusha Florentino Perezi ni kweli magoli 17 katika mechi 32 alizokutanana na Barca mataji matatu ya Uefa na mawili ya la liga!!!
PESA
Ronaldo ni tajiri analipwa mshahara paundi million 19.5 kwa mwaka sawa na billion 58 za madafu😱😱😱
ana mkataba na kampuni ya Nike wenye thamani ya dola 21.7milion (Billion 45.5 za bongo) kwa mwaka na sio tu Nike ana mapato mengine kutoka Toyota, Samsung, Arnmani n.k ambayo yanamuingizia dola milion 10.7 milion(billion 24 za bongo) kwa mwaka
Sio tu soka bali bali ni mfanyabishara na hajatosheka na utajiri wake tayari ana malengo na anajua nini atafanya baada ya kustaafu soka
Anauza mavazi na viatu vya CR7 vinavyomuingizia dolaa million 6 hadi 10 kwa mwaka
ana Hotel New York, Funchal, Madrid na Madeira
Messi anaweza akaja kumpita Ronaldo kwa mataji na tuzo lakini linapokuja suala la pesa Ronaldo ni habari nyingine
Kuna mambo muhimu matatu au manne yachukue kutoka kwa Cristiano Ronaldo
Juhudi na kujituma ndiyo nyenzo za mafanikio
Jiamini
Penda kazi yako nawe mwenyewe jipende bila masharti
Ishi kwa malengo umri na ujana unakimbia haraka sana
A person who doesn't fear to die lives fully