Cross Examination Documentation

Cross Examination Documentation

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Naomba thread hii iwe inakusanya video na documentations zote zinazohusu cross-examinations za kesi mbalimbali mahakamani kutoka pande mbalimbali za dunia.

Kati ya vitu huwa napenda sana kwa wanasheria ni pale wanapoonyesha uwezo wa cross-examination dhidi ya shahidi. Marehemu Lamwai alifanya cross-examination moja ambayo ilituachia msamiati wa Ukihiyo
 
Ipo ya Kibataka vs Kamanda Hamdani humu.

Ipo ya Lissu vs .......( nimemsahau)

Zinavutia sana.
 
Kama unaweza, tafuta link zake.
Fuatilia mlolongo wa shauri hilo ulivyokuwa leo katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu iliyopo Jijini Dar es Salaam.
-----------

Shahidi anajitambulisha..

Naitwa ASP Fadhili Bakari. Ni Afisa Polisi, Kanda maalum Dar es Salaam tangu Machi 2016.

MAJUKUMU: Ni mkuu wa kitengo Cha uhalifu wa kifedha Kanda maalum ya DSM, pia kitengo cha uhalifu wa makosa ya kimtandao kipo chini yangu.

Mnamo tarehe 10/05/2016 nikiwa ofisini alikuja mpelelezi wa Kesi, Assistant Monica na jalada la uchunguzi linalohusiana na tuhuma zilizoletwa ofisini na mkurugenzi wa wakala wa forodha CUSNA Investment na Ocean Link kwamba kuna taarifa zimesambazwa kwenye mtandao wa JamiiForums kwamba kampuni tajwa inajihusisha na wizi, ukwepaji Kodi na kughushi vitendo ambavyo vimeisababishia Serikali hasara.

Tuhuma zilizoletwa na watu wawili ambao ni Amrish Puri na Kwayu. Taarifa zilizodaiwa kusambazwa mnamo 08 Dec 2015.

Inspekta Monica alikuja kwangu ili niweze kuwasiliana na Mkurugenzi wa JamiiForums ili tupate details za wateja zitakazosaidia kwenye Kesi/uchunguzi.

Niliandika barua kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa JamiiForums ikimtaka anipe Ushirikiano wa kunipa information(Namba za simu na taarifa za usajili za watu hao). Baada ya kuandika barua na kuisani nilimpatia mhusika kufikisha kwa anaehusika, Inspekta Peter Kayumbi aliniambia siku ya pili kuwa barua imepokelewa na kusainiwa na aliyeipokea.

Sikuweza kupata information nilizokuwa nazitaka ambazo zingenisaidia kwenye kesi (Shahidi anaonyeshwa kielelezo na anasema anaitambua kuwa ndio yenyewe na kuiomba mahakama iipokee kama kielelezo). Wakili wa utetezi (Jebra Kambole) anakubali ipokelewe na hakimu anaikubali.

Shahidi anaisoma barua ambayo alimuandikia mkurugenzi mkuu wa JamiiForums kuhusu taarifa inayoihusu kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link ya kuomba taarifa za usajili na namba za simu walizotumia kipindi wanajisajili kwenye mtandao wa JamiiForums.

Barua ilipokelewa na Chrispine Muganyizi siku moja baadae, Shahidi anaulizwa kuhusu taarifa zilizopo kwenye barua na kusema kulikuwa na makosa ya kiuandishi kwenye mwaka. Shahidi anaendelea kusema hakupatiwa taarifa zozote kama alivyoomba.

Wakili wa Serikali ameishia hapo na anafuata wakili wa utetezi, Wakili Jebra Kambole.

Wakili: Umesema unamsaidia mkurugenzi wa upelelezi?
Shahidi: Sahihi

Wakili: Kwa uelewa wako wewe humfahamu mmiliki wa JamiiForums?
Shahidi: Simfahamu

Wakili: Unafanya kazi JamiiForums?
Shahidi: Hapana

Wakili: Una uhakika gani taarifa ulizoomba walikuwa nazo?
Shahidi: Nina uhakika walikuwa nazo.

Wakili : Una ushahidi?
Shahidi: Sina ushahidi mwingine

Wakili: Kwa kuwa hauna ushahidi, inawezekana huyo mtu taarifa ulizoomba alikuwa nazo au hakuwa nazo!?
Shahidi: Haiwezekani

Wakili: Kwa kuwa barua iliandikwa Mkurugenzi mtendaji, akiwemo mtu mwingine atakuwa ameonewa?
Shahidi: Siwezi kujua maana mimi sikuhusuka kwenye ukamataji

Wakili: Kifungu Cha kumi hakikupi mamlaka ya kudai taarifa. Mtoa taarifa alitenda kosa gani?
Shahidi: Hili ni jalada la uchunguzi

Wakili: Hamkuona haja kuitaarifu TRA kuhusu mtu anayekwepa Kodi?
Shahidi: Haihusiani na hii kesi. Binafsi sikuwapa.

Wakili: Unajua mtu asikupokupa taarifa unaenda mahakamani kuomba amri?
Shahidi: Sijui.
---------

Wakili Mtobesya: Naomba nipatiwe exhibit P1. Nawasilisha ombi hili kwa mujibu wa kosa la jinai na makosa ya mtandao.

Maswali kwa Shahidi..

Mtobesya: Unaelewa kama washtakiwa wanashtakiwa kwa kosa gani hapa mahakamani?
Shahidi: Sijui

Mtobesya: Nitakuwa sahihi kama nitasema Polisi hamjui mlitakiwa kufanya nini wakati mnatafuta taarifa?
Shahidi: Mimi nilitaka nipate details

Mtobesya: Kwa hiyo taarifa ulizokuwa unazitaka zilikuwa kwenye mtandao?
Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Naomba niishie hapo

Wakili wa Jamhuri: Uliwahi kupata majibu kutoka uongozi wa JamiiForums?
Shahidi: Sikuwahi kupata

Kesi itaendelea kesho..
 
Angalia lawyer anvyokutana na engineer kwenye kiti cha shahdi wakati wa cross examination.

 
Defense lawyer apambana kumkinga mteja wake wakati wa cross examination ya mteja wake.



Huyo defense lawyer ni kiboko kwelikweli; "Don't lecture me; I was doing this when you were still chasing cheerleaders." LMAO!!!!!!!
 
Kirambasi
Duh! Mzee umenirudisha hapa; huyo Lawyer mimi nikiwa na kesi ndiye wa kutafuta, siyo Mr Macharia wa Nairobi aliyeyumbishwa na swali dogo sana la yule mama jaji kuanzia dakika ya 2:50
 
Duh! Mzee umenirudisha hapa; huyo Lawyer mimi nikiwa na kesi ndiye wa kutafuta, siyo Mr Macharia wa Nairobi
Ahahaha hatari sana, Lamwai yalikua mambo yake hayo enzi zake.
 
Jamaa anatwanga kila swali kwa jibu moja tu:

Objection: Argumentative, calls for speculations , no foundation, vague and ambiguous
 
Back
Top Bottom