Cruyff baba wa tik tak football duniani (Sehemu ya 1)

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Usiku mmoja wa baridi kali April 28, 1988 saa1 usiku, kwenye hotel ya Hesperia, mitaa ya Carrer dels Vergos, Jijini Barcelona nchini Hispania, wachezaji 21 wa klabu hiyo wakiongozwa na kocha Luis Aragones waliweka mgomo kutokana na matendo ya Rais wa Barca, bwana Josep Lluis Nunez.

Ujio wa mwamba wa Uholanzi Johann Cruyff, mnamo Mei 4, 1988 wakiamini kuwa atakuja kufanya mapinduzi makubwa kwenye soka lao.

Siku ya kwanza darasani, Cruyff aliwachorea wachezaji mfumo wa 3-4-3 alioubadili kutoka 4-3-3, wachezaji walishangaa akiwemo Eusebio, dunia hii ya 4-4-2 na 3-5-2 unaleta mfumo mwingine? Waliwaza sana wachezaji wake.

Akili ya Cruyff ilikuwa ni kubadili alichofundishwa na Mwalimu wake Rinus Michels miaka ya 1970 ili kuleta kitu kipya, kumbuka aliuza wachezaji 15 aliowakuta na kuleta wachezaji watakaofit mfumo wake.

Cruyff alimleta winger Txiki Begiristain, Jose Mari Bakero 'Attacking Midfielder', Julio Salinas 'Centre Forward' na Eusebio 'Defensive Midfielder' hawa walikuwa spinal cord ya soka lake, ikumbuke alimbakiza Alexanko ambaye ndie Nahodha na umri wake wa miaka 32.

Wakati anaanza kuisuka Barca mpya kupata ile style ya Barcelonismo aliwahi kumfokea Rais Nunes kutokana na tabia ya kumuingilia kwenye mambo yake, alimwambia ukitaka kuongea na mimi nitakuja ofisini kwako, ila hupaswi kuja dressing room kwangu, mimi ndio Boss hapa[emoji2]

Wakati falsafa mpya inatengenezwa Cruyff aliagiza La Masia yote watumie mfumo wa 3-4-3 kuanzia U8, wakati anaisuka Barca mpya alikuwa na kikosi cha wachezaji vijana, wembamba na wafupi ila yeye ndio aliwahitaji zaidi.

Tuendelee, wakati wachezaji wapo Darasani wakamuuliza, Kocha hapo tunajilinda vipi na mabeki watatu?

Cruyff alijibu kirahisi tu[emoji2] mnataka mabeki wanne wakabe maforwad wawili, mnasahau kuwa tutabaki 6 kwenye kiungo wao wakiwa 8, hapo ni kazi kushinda, "Ukiruhusu kupoteza kiungo umeruhusu kupoteza mchezo"

Wakati Cruyff anasuka trademark akagundua kuwa mfumo wake unahitaji Tactical Artists, mafundi haswa wa mpira, wale football decoraters, asubuhi moja kwenye viunga vya Camp Nou akaja na wazo

Itaendelea
 
mbona ushazingua mapema yote hiiiii?
naisubiria hii makala kwa mara nyengine ila usije ukaingia mitini
 
Sehemu ya 2

 
Usisahau mkuu!
 
guardiola kamkopi cruyf na wenger,alienda arsenal pale kuisoma invicibles ya wenger,pia nyuma huko alimbembeleza sana wenger acheze arsenal
 
cruyff kavu,hakumpa kibarua mshikaji wake sunday manara aliyecheza nae timu moja
 
guardiola kamkopi cruyf na wenger,alienda arsenal pale kuisoma invicibles ya wenger,pia nyuma huko alimbembeleza sana wenger acheze arsenal
Yah amechanganya falsafa


Aliisoma invincible akamix na Cruyff ndio unakuja kumpata pep na hii tik tak
 
Lakini ndio anasumbua na huo huo , kila anapoenda
epl pale nafikiri dawa ishapatikana,na timu kama chelsea,arsenal na man u wataendelea kutumia hela kama yeye,so janja yake kwisha,natabiri ataondoka tu na kurudi spain,bayern waliona anawaharibia tu timu...timu yake inacost 1bl pounds
 
pep alienda arsenal kuisoma arsenal ya wenger,kama linakukera hili pole

Hapo Arsenal ni moja ya sehemu alizokwenda Pepe na nikawaida ya makocha wachanga kupita sehemu tofauti kwa kujiendeleza lakini haimaanishi ndio kapata ujuzii unaoutumia mbona kaenda sehemu nyingi. Pep alianza kusomea ndani ya Barca na baadae akenda Italy Brecia na alikaa huko kwa mda mrefu kuliko sehemu yoyote, Pia Argentina kwa Bielsa.
 
baada ya kutoka arsenal,akaenda marekani kutengeneza falsafa ambayo kimsingi siyo yake ni ya cruyff
 
Acha kujifurahisha, Pep kamkopi nini Wenger?
Kama.hujui kitu uliza ,sio unaropoka

Pep mwenyewe anasema hivi

pep anakiri kwa mdomo anasem

" I was always looking on Wenger's football tactics before join this Field"

Na alisema yeye ni shabiki mkubwa wa Wenger na cruyff
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…