Cry for help.......

IGWE

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2011
Posts
9,578
Reaction score
7,774
Salaam wakuu..

Mtoto wangu ana week 3 sasa,week ya pili sasa analia huku akirusha miguu na mikono kwa uchungu as if tumbo linamkata.Wazoefu wanasema eti akimaliza mwezi ataacha kujinyonga kwani ni kawaida kwa watoto wadogo..na hata nikimpeleka hospital hakuna dawa atakayopewa huko.

My take;Ni kweli ni kawaida na ataacha baada ya mwezi mmoja kuisha ama nimpeleke hospital.

Nawasilisha kwa msaada wakuu
 
Ndugu mtoto mkimbize hospitalini haraka
 
Ni kawaida watoto kati ya wiki moja mpaka nane kulia na kuna sababu tofauti ila mojawapo ni kujaa kwa gas tumboni ambayo huwaletea maumivu. Gripe water for infants inaweza kuwasaidia, ila ni muhimu sana umpeleke Hospitali ili waone tatizo ni nini na asiadiwaje,analiaje (kilio cha kuumwa au njaa, hasira n.k) analia wakati gani na kwa muda gani. Vilevile utashauriwa jinsi ya kunyonyesha (ni breastfeeding au unatumia chupa?)ili asivute upepo kama ni chupa. Vilevile kumfanyia massage tumboni taratibu kunaweza kumsaidia, nurses wengi wanaweza kukushauri vizuri hasa wanaofanya kazi kwenye wodi za watoto wadogo!
 

Asante sana Peace,.hiyo grip water anatumia with all in vain,ananyonya kwa maziwa ya mama..ni kama analia kwa uchungu i.e ni kama ana-struggle kwa maumivu ya tumbo huku akihema kwa shida.analia sana usiku

Point of correction..simnyonyeshi mimi anayemnyosha ni mama yake...mimi ni baba ninaye jali

Thanx again Peace...be blessed
 
Hakikisha anapomaliza kunyonya anawekwa begani ili acheue,na usimuweke kwa muda mfupi akae hapo hata dakika kumi atacheua mara nyingi na kupunguza gesi nyingi.Pia jitahidi kumlaza kwa tumbo, hivi ndivyo nilishauriwa na daktari kwani hii shida nimeshawahi kuipata,na pia madaktari wa watoto wanatushauri tusiwape grip water kwani wakati mwingine inaongeza tatizo.
 

hata mi njia hii ilisaidia sana mtoto akishacheu maumivu ya tumbo hupungua,ila mimi badala ya gripe water nilishauriwa nimtafutie Beladona ambayo ilisaidia sana kama vipi hebu itafute ujaribu.Pole sana mkuu najua hapo hamlali usiku dogo akianza kulia
 

Mungu akubariki sana Mamamkwe...ushauri muhimi sana huu
 

Asante sana Muangila,ntajaribu hiyo dawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…