Cryptocurrency sio Uwekezaji

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Ni jambo la kawaida kwa vijana wanajihusisha na cryptocurrency kushawishi wengine kuwa huo ni uwekezaji ambapo watu wengi huingia wakiamini watapata faida kubwa lakini huishia kupata hasara au faida ya kawaida ambayo wangeweza kuipata katika masoko yoyote ya pesa

Kwa ufupi sana, Uwekezaji ni kuongezea mtaji katika biashara inayoenda kufanyika. Mfano watu hununua hisa ili kuzipa mitaji kampuni za biashara kisha wao hupata gawio linalotokana na faida kila mwisho wa mwaka

Cryptocurrency ni fedha ya mtandao ambayo kama itakuja kuwa fedha kwa kufanyia miamala mtu atakayekuwa anamiliki Cryptocurrency hatokuwa tofauti na anayemiliki fedha yoyote yenye nguvu i.e Riyali au Dola. Swali ni Je, Ukinunua Dola au Riyali, Utajiita Muwekezaji?

FIAT MONEY


Pesa tuliyonayo ni Fiat ambayo thamani yake haijaambatanishwa na Dhahabu kama ilivyokuwa miaka ya 1980 kurudi nyuma, ni suala ambalo limetajwa kusababisha thamani ya fedha kubadilika kila mara (Inflation) kwa kuwa thamani yake ina-hang hewani

Kwa hoja ya Fiat Money, Cryptocurrency haiwi-exempted kwa kuwa hata yenyewe haijaambatanishwa na Bidhaa iliyostable, mbali na kukosa bidhaa, pesa hizi zimekuwa zikipanda thamani na kushuka kiasi cha kuwa na ugumu wa kupredict thamani yake kwa usahihi hali inayofanya watu wanaojua uwekezaji kama benki za biashara kutojihusisha nayo

HOJA YA MSINGI

Cryptocurrency ni fedha ya mtandao kuwa nayo sio uwekezaji, labda unaweza kuitwa ‘Arbitrageur’ ikiwa utakuwa unacheza nazo kwenye Foreign Exchange. Lengo la fedha hii ilikuwa ni kuficha utambulisho wa mtu kwenye manunuzi ya mtandaoni na sio kumpa mtu utajiri kwa kuimiliki.

Hivyo kabla haujajitutumua kumiliki Cryptocurrency, jiulize, utakuwa na shida gani ukinunu fehda nyingine yenye nguvu na thamani duniani

Signed
OEDIPUS
 
Kikubwa na cha muhimu ni kufanya utafiti kabla ya kuingiza pesa yako sehemu yoyote lakini kwa Tanzania naona watu wengi kazi yao ni kupinga pesa yoyote inayopatikana kwa internet either ni Forex iwe Crypto lakini kuna madogo wapo wanakula zao pesa kwa mtindo huuhuu Anyway kikubwa kila mtu awekeze pesa ake mahali anapenda
 
Cryptos na NFTs zinaendeshwa kwa kwa mfumo wa PROMO na FOMO.

Yaani inatengenezwa HYPE kubwa kuhusu Cryptos na NFTs na hivyo watu wengi wakitaka kununua inapanda thamani.

Akitokea mtu mwenye ushawishi akiziponda ZINAPOROMOKA tena.

Yaani hata wewe unaweza kutengeneza Coin yako na ukaanza kuipush.

Na kibaya zaidi wamasema ni Coin lakini wakiziuza wanataka kupewa pesa za kawaida, sasa umajiuliza hizi ni Currency au bidhaa?
 
Mimi kama kuna jambo linanistaajabisha ni NFTs, yani eti mtu ananunua vi jpgs kwa millions of dollars. Ni ukichaa
 
Mimi kama kuna jambo linanistaajabisha ni NFTs, yani eti mtu ananunua vi jpgs kwa millions of dollars. Ni ukichaa
MIHEMKO inayotokana na PROMOTION.

Hebu jiulize,
Inawezekanaje MTU ananunua BIDHAA kwasababu MTU FULANI MAARUFU amepewa PESA ili aseme hiyo BIDHAA ni NZURI??

Yaani hizi Cryotos na NFTs zinavyofanya kazi ni sawa na KISA CHA MNUNUZI WA SUNGURA.

............ "Kwamba alikuja mgeni mmoja kijijini akasema ananunua SUNGURA mmoja kwa Tsh 500,000 watu wakampelekea sungura wake wote akanunua. Alivyojua singura wameisha kijijini ,AKAPANDISHA Dau kuwa SASA atakuwa ananunua SUNGURA kwa Tsh 2,000,000 kwa mmoja.

Wakati huo ameshampanga mtu awauze wale sungura aliowanunua kwa wanakijiji hao hao kwa Tsh 500,000.

Kwahiyo wanakijiji walitafuta SUNGURA kokote walipo mpaka kwa bei ya Tsh 1,000,000 maana jamaa ananunua kwa bei ya Tsh 2,000,000 kwa mmoja.

Mnunuzi wa SUNGURA na MTU wake walivyohakikisha wameshawauza SUNGURA WOTE kwa wanakijiji kwa bei ya Tsh 1,000,000 Wakatambaa.

Wanakijiji wakawa hawana tena sehemunya kuuza Sungura wao.
 
Akili yako kubwa mkuu, Mungu akuzidishie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NB: kununua Low kuuza High then weka pesa mfukoni.

Hayo mengine hayana mantiki.
 
Tatizo hizo pesa zenu za mitandaoni ni kama ghost money! Yani pesa ambayo haishikiki haiko tangible!

Halafu to make shit worse hio pesa imehusishwa sana na cases za utapeli wa baina ya wauzaji na traders!
 
Sio kweli. Wewe ulicheza forex, Kuwa mkweli.
Crypto Ina pesa sana ni vile wengi wenu hamjitambui kwenye hilo eneo.
Achana na forex ni utapeli wa kimataifa.
Hio Crypto pesa unapataje? Can you put money and grab it in real time kama Forex?
 
Nilinunua BNB Ikiwa low, nilinunua Etherium Ikiwa low, nilinunua Shibainu Ikiwa low, Feb-March 2020 nilinunua BTC Ikiwa low. Usiniulize leo nina kiasi gani cha pesa.
Hongera sana ila hizo currency walau angetokea mtu aka narrate kuwa zinafanyaje kazi na unanunua wapi na vipi na unapataje faida!
Kinyume na hapo ni biashara ya kuuziana sungura tu!
 
Tatizo hizo pesa zenu za mitandaoni ni kama ghost money! Yani pesa ambayo haishikiki haiko tangible!

Halafu to make shit worse hio pesa imehusishwa sana na cases za utapeli wa baina ya wauzaji na traders!
Nakubaliana na ww ndio maana nikasema kabla ya kufanya chochote ni lazima ufanye uchunguzi wa nguvu ni sawa na Mkulima analima ajachunguza masoko,hali ya hewa,ushindani wa kibiashara ana tofauti gani na hawa wa crypto kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…