OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Ni jambo la kawaida kwa vijana wanajihusisha na cryptocurrency kushawishi wengine kuwa huo ni uwekezaji ambapo watu wengi huingia wakiamini watapata faida kubwa lakini huishia kupata hasara au faida ya kawaida ambayo wangeweza kuipata katika masoko yoyote ya pesa
Kwa ufupi sana, Uwekezaji ni kuongezea mtaji katika biashara inayoenda kufanyika. Mfano watu hununua hisa ili kuzipa mitaji kampuni za biashara kisha wao hupata gawio linalotokana na faida kila mwisho wa mwaka
Cryptocurrency ni fedha ya mtandao ambayo kama itakuja kuwa fedha kwa kufanyia miamala mtu atakayekuwa anamiliki Cryptocurrency hatokuwa tofauti na anayemiliki fedha yoyote yenye nguvu i.e Riyali au Dola. Swali ni Je, Ukinunua Dola au Riyali, Utajiita Muwekezaji?
FIAT MONEY
Pesa tuliyonayo ni Fiat ambayo thamani yake haijaambatanishwa na Dhahabu kama ilivyokuwa miaka ya 1980 kurudi nyuma, ni suala ambalo limetajwa kusababisha thamani ya fedha kubadilika kila mara (Inflation) kwa kuwa thamani yake ina-hang hewani
Kwa hoja ya Fiat Money, Cryptocurrency haiwi-exempted kwa kuwa hata yenyewe haijaambatanishwa na Bidhaa iliyostable, mbali na kukosa bidhaa, pesa hizi zimekuwa zikipanda thamani na kushuka kiasi cha kuwa na ugumu wa kupredict thamani yake kwa usahihi hali inayofanya watu wanaojua uwekezaji kama benki za biashara kutojihusisha nayo
HOJA YA MSINGI
Cryptocurrency ni fedha ya mtandao kuwa nayo sio uwekezaji, labda unaweza kuitwa ‘Arbitrageur’ ikiwa utakuwa unacheza nazo kwenye Foreign Exchange. Lengo la fedha hii ilikuwa ni kuficha utambulisho wa mtu kwenye manunuzi ya mtandaoni na sio kumpa mtu utajiri kwa kuimiliki.
Hivyo kabla haujajitutumua kumiliki Cryptocurrency, jiulize, utakuwa na shida gani ukinunu fehda nyingine yenye nguvu na thamani duniani
Signed
OEDIPUS