Crystalline Canopy Theory na gharika la Nuhu

Mkuu aliyeandika hiyo nadharia ni pastor tena ana PhD ya theologia na mhubiri aliyeheshimika sana tu enzi za uhai hivyo sidhani kama hafahamu haya unayosema humu.

Kingine hapo mwisho nimeweka swali kwamba hayo maji yaliyo JUU ya anga ni yapi maana ya CHINI ya anga tumeyaona.... Na nimeleta hii mada ili nijifunze zaidi kuhusu uumbaji, hivyo ningeomba ufafanuzi hapo mkuu
 

Ni some vizuri huyo padre kajiumba mwenyewe ? Je una amini ana uwezo kumzidi Mungu? Au wewe huamini katika Mungu?

Swali lipi uliloliuliza labda ni melimiss?
 
Nimeomba unisaidie kutafsiri Mwanzo 1 sura ya 6 na 7....

Kwa nini hukubaliani na ukweli kuwa maji ya angani/mbinguni ndiyo hiyo hiyo mvua ama husababisha mvua?

Soma mwanzo 7:4, 11 na 12 na mwanzo 8:1-2. Utakuja kuona kuwa maji ya mbinguni na mvua ni majina yaliyotumika kwa kubadilishana ya kimaanisha kitu kimoja.
 
Mkuu sijaona kwenye hiyo mistari kuna MAJI JUU YA ANGA..... Mvua sijakataa ilikuwepo ila ni baada ya gharika maana hakukuwa na mvua wala mawingu kabla ya gharika na hiyo ni kwa mujibu wa biblia

Daudi kwenye zaburi ametofautisha na mistari nimeweka kwenye nyuzi kwamba Mawingu,mvua na MAJI JUU YA ANGA ni vitu viwili tofauti na ndio maana nikafungua uzi humu ili nipate mawazo yenu na hayo majina ni mawili tofauti kwa kiebrania sababu canopy imeitwa ''raqy'ila'' kwa kiebrania ikimaanisha mzingo fulani wa maji unaozunguka Dunia na halitumiki zaidi ya hiyo mistari miwili tu niliyoweka hivyo hakuna possibility kuwa ni mvua au mawingu unless kamusi ya kiebrania imebadilika

Na hata msomi credible wa kiyahudi Flavius Josephus kwenye kitabu cha Antiquities...anathibitisha kwamba kulikuwepo na huo mzingo wa maji hivyo basi kama sio Mvua au mawingu je hayo MAJI JUU YA ANGA ni yapi

Son of Gamba SALA NA KAZI mitale na midimu mpite huku
 
Sijui kama niko sawa kuamini hata Maji Muumbaji aliyakuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoa uzi jaribu kuwa katikati ktk hili ili wengi tupate mawazo ya wengine... Usilazimishe kujibiwa habari za maji ya angani as if kuna aliyeandika biblia, bali kama kuna watu walichunguza na kugundua ndio yaliyotumika kwenye gharika na wewe ukawaamini basi amini hivyo.
Ila hata hayo maji Biblia inatuambia yalikuwepo kabla ya uumbaji wa dunia na vilivyomo sasa tukikuuliza hayo maji yalitoka wapi mpaka yakatengwa juu na chini utapata majibu?
Kama wote hatujui yalipotokea basi tuheshim mawazo na maono ya wengine other wise ungeishia kuamini hyo theory bila kuleta uzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hawa ndiyo huishia kumeza tu theory za kwenye vitabu ili afaulu tu mtihani na matokeo yake ndiyo haya tunayaona anaona watu wanao hoji wanajichosha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu inaweza kuwa ni sahihi maana ukisoma kitabu cha Petro kinaelezea kwamba miaka elfu moja kwa Mungu sawa na siku moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu tukienda kibiblia ni kwamba hayo maji yaliumbwa na Mungu.... Na vyote vilivyoumbwa kwenye hizo siku 6 mpaka leo vipo ndio maana sijauliza ila kuhusu MAJI JUU YA ANGA ndio nikakwama kwamba yalikuwa maji gani ?? Wala hakuna mahali nimelazimisha kuwa hii theory ni ya kweli au lah bali nimeuliza kama si ya kweli je HAYO MAJI ni yapi nikiamini humu kuna wasoma maandiko wengi tu wanaweza kunisaidia so kama unafahamu unaweza tusaidia na jibu pia
 
Zitto junior
Je hivi sasa hayo maji ya angani yapo? Jibu ni yapo, ndio maana tunapata mvua.

Unasema mawingu hayakuwepo lakini hapo hapo umetoa aya inayotaja ukungu, hivi hujui kuwa ukungu na mawingi ni kitu kimoja sema tafauti, ni kuwa kwenye anga yanaitwa mawingu na kwenye uso wa ardhi ni ukungu, kwa hiyo tunapata mvua kwa sababu ya maji ya angani, maana nyingine ya neno mawingu ni maji ya angani, ndio maana sometimes tunapataga hata mvua ya barafu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unaposema haya maji ya juu kwamba ni mawingu naomba usome hii mistari.

Mwanzo 1:6-8
[6]Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.
[7]Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.
[8]Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.

Hapo alitenga maji kwa kutumia anga na hilo anga ndio mbingu sasa, unavyosema mawingu ndo hayo maji ya juu sidhani kama ni sahihi. Hii ina maana kwenye mbingu juu yake kuna maji.

sent using samsung galaxy s8
 
Kama unakubaliana na hoja kwamba mawingu au ukungu ni maji anga, na uwazi uliopo kati maji ya juu na chini anga au mbimgu, sasa ugumu unakuja wapi sasa. Maana mawingu ndio yanaleta mvua, we we unayatafuta maji ya angani yapi hayo zaidi ya haya.

Kama mawingu yangekuwa siyo chanzo cha mvua ningeilewa hoja yapo, maana hata wanasayansi wanaprove mvua inatokana na mawingi, ingekuwa siyo hata mimi ningeyatafuta hayo, japo zamani wakati nipo mdogo nilijua mawingu ni moshi ulioganda, au mkuu ulitaka juu nako kuonakane kama bahari au ziwa, alichofanya mungu aliyabadilisha yakawa mvuke ila yakirudi chini yanakuwa yakawaida maana alijua2 watu kama nyie mngekuja kuyatafuta maji ya angani.

Ni kama binadamu tumeumbwa kwa udongo lakini sisi hatupo kama sanamu la udongo, ila prove inakuja pale utakapokufa unarudi unakuwa udongo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu labda nimekuelewa ila biblia imetofautisha kati ya MAWINGU na haya maji JUU YA ANGA......

Zaburi 147:8
Huzifunika mbingu kwa mawingu,Huitengenezea nchi mvua,Na kuyameesha majani milimani

Na sura inayofuata anaonyesha tofauti
Zaburi 148:4
4 Msifuni, enyi mbingu za mbingu,Nanyi maji mlioko juu ya mbingu.
5 Na vilisifu jina la BWANA,Kwa maana aliamuru, vikaumbwa

Biblia kwenye MAJI JUU YA ANGA neno lililotumika ni raq'ila ikimaanisha mzingo fulani kama "sufuria" alafu neno WINGU kwenye biblia imetumika neno "anan" ikimaanisha "alama ya agano" maana ni baada ya gharika ndio Mungu analeta mawingu soma hapa

Mwanzo 9
14 Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni

Hivyo mpaka hapa tunaweza kubaliana kuwa MAJI JUU YA ANGA na MAWINGU ni vitu viwili tofauti ndio swali linabaki hayo maji JUU YA ANGA ni yapi na yaliishia wapi na kama ni mawingu ni kwanini Daudi na Biblia alitofautisha hivyo vitu viwili kuonyesha havina uhusiano??
 
Kabla hatujafika mbali, naomba niukuulize.
Mbingu au jina jengine anga lipo sehem gani?

sent using samsung galaxy s8
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…