SI KWELI CS Hanna Cheptumo aandaa Poster ya ‘Governor 2027’: Asema Hatawania Kiti Chochote

SI KWELI CS Hanna Cheptumo aandaa Poster ya ‘Governor 2027’: Asema Hatawania Kiti Chochote

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Picha inayosambaa mitandaoni inamuonyesha Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Huduma za Watoto, Hannah Wendot Cheptumo, akiwa kwenye poster inayodai kuwa anajiandaa kuwania nafasi ya Gavana katika Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Poster hiyo yenye nembo na rangi za UDA imeandikwa “Hon. Hannah Cheptumo – Governor 2027”, jambo ambalo limeibua madai kuwa huenda Waziri huyo ana mipango ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha ugavana.

Hata hivyo, Cheptumo mwenyewe amekanusha madai hayo na kusema poster hiyo si taarifa sahihi kuhusu mipango yake ya kisiasa.

Cheptumo kwa sasa anahudumu kama Cabinet Secretary, baada ya kuteuliwa katika Baraza la Mawaziri mwaka 2025.

800231328_1456168619748991_1875057513398784784_n.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwa na Picha inayosambaa mitandaoni inamuonyesha Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Huduma za Watoto, Hannah Wendot Cheptumo, akiwa kwenye poster inayodai kuwa anajiandaa kuwania nafasi ya Gavana katika Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Poster hiyo yenye nembo na rangi za UDA imeandikwa “Hon. Hannah Cheptumo – Governor 2027”, jambo ambalo limeibua madai kuwa huenda Waziri huyo ana mipango ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha ugavana.

Hata hivyo, Cheptumo mwenyewe amekanusha madai hayo na kusema poster hiyo si taarifa sahihi kuhusu mipango yake ya kisiasa.

Cheptumo kwa sasa anahudumu kama Cabinet Secretary, baada ya kuteuliwa katika Baraza la Mawaziri mwaka 2025.

Kuhusu poster inayosambaa, Cheptumo amekanusha madai kwamba anajiandaa kuwania nafasi ya kisiasa mwaka 2027. Amesema:

“Please avoid fake news and misinformation. I will NOT be vying for any political seat.”
Ameeleza kuwa kwa sasa analenga kutekeleza majukumu yake serikalini na kumuunga mkono Rais William Ruto katika ajenda yake pamoja na kampeni ya kuchaguliwa tena.

Hanna Wendot Cheptumo ni nani?

Hanna Wendot Cheptumo ni Cabinet Secretary wa Gender, Culture and Children Services, nafasi aliyoteuliwa na Rais William Ruto na kuapishwa Aprili 17, 2025. Katika wadhifa huo, anaongoza masuala ya usawa wa kijinsia, watoto, utamaduni na programu zinazohusiana na kupambana na ukatili wa kijinsia.

Hitimisho: Poster inayomtangaza Hannah Cheptumo kama mgombea wa Gavana 2027 ni taarifa inayokinzana na kauli yake mwenyewe na inapaswa kuchukuliwa kama taarifa potofu isipokuwa kuwe na tangazo jipya rasmi kutoka kwake.
Back
Top Bottom