Kinacho nishangaza kuna watu wana points 41 wana div 0 na kuna wengine wana points 44 wana div 4 yaani hapo ndio nilipo pigwa bumbuwazi
Wana jamvi naomba mnifuatilie kwa makini juu ya ufafanuzi wa matokeo haya. Naomba nianze upya kuwaelezea jinsi ya upangaji wa madaraja yaani divisions kama ifuatavyo:-
Div. I: Pts 7-17
Div.II: Pts 18-24
Div.III: Pts 25-31
Div.IV: Pts 32-40 + (41,42 43,44,45,46)
Div. O: Pts. + (41,42,43,44,45,46), 47-49
Hizo point zilizopo kwenye mabano zinaingia kotekote kama inavyoonekana yaani ukiwa na moja kati ya point hizo, factor nyingine huangaliwa, factor hizo ni ufaulu katika somo moja moja, yaani kama kuna A moja au B moja au C moja au D mbili, basi hapo daraja la nne yaani Div. IV hutolewa.
Lakini kama hakuna hata A moja, au B moja, au C moja, au D mbili basi daraja O yaani Div. O hutolewa.
Nadhani nimeeleweka.