CUF Bukoba watinga bungeni

Kiranja

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2007
Posts
751
Reaction score
336
Viongozi wa CUF Bukoba watinga bungeni. Spika awatambulisha. Je, hii ni sehemu ya mkakati wa kumkabili Lwakatare?
 
Viongozi wa CUF Bukoba watinga bungeni. Spika awatambulisha. Je, hii ni sehemu ya mkakati wa kumkabili Lwakatare?

Lwakatare atakabiliwa kule kule Bukoba na si Bungeni .Kwanza Bunge ni la wote bila ya kujali vyama .Sema kutambulishwa ni new twist kwa CUF maana hii ni tabia ya CCM sasa na CUF wameanza kuimba wimbo huo sawa ni haki yao .Kuna kampeni kule Dodoma jumba la baridi au sijaelewa ulitaka kutueleza nini ?
 
Waswahili wanasema ujanja kuwahi. CUF wanakumbuka shuka wakati kumesha kucha? CUF Tanzania Bara ilijikita katika MUAFAKA na CCM ikasahau kwamba Tanzania Bara Muafaka sio issue. Ikasahau kwamba suala la Ufisadi na Umasikini ni mambo muhimu kwa watu wa Bara. Matokeo yake Chadema imechukua nafasi Muhimu hasa baada ya Kampeni ya Operesheni Sangara. Kwa CUF kuanzisha Operesheni Zinduka wakati huu ni sawa na kukimbizana na mkia wa Mbwa! Bila Rwakatare CUF is as good as dead in Bukoba.
 
Huyo Katare alikuwepo katika kampeni B/muro na mbona sisieeemu wakavuna ushindi?Nenda muendako hawa jamaa ndio waongoza nchi tuu mtabaki kutosaini daftari ya matokeo halafu ndio nini?!
 
Hii misafara ya wanasiasa na Wapambe kushindana kwenda bungeni Dodoma inanitia kichefu chefu. Hawa watu wanafanya kazi saa ngapi?

Huenda kuna maskini huko wilayani anasubiri huduma zao na kila siku anaambiwa njoo kesho, mheshimiwa hayupo.

Tunahitaji mabadiliko makubwa TZ; mabadiliko ya fikra na matendo.
 
Ni kawaida hiyo hapo bungeni,huwepo na wageni waalikwa natumai hii hata mbunge akitaka kumpeleka mwanawe basi anaruhusika kwa kufuata taratibu na Soika atawajibika kumtambulisha.
Naona mna mchecheto hata mambu bado ,kwani Chadema mtamsimamisha Lwakatare kugombea ubunge ???
 
Ni kweli kabisa tunahitaji mapinduzi ya kifikra na kimatendo, tusikubari mawazo yao wala kujikomba kwao....CCM sasa wamejikita kwenye kununua shada za wapiga kura na kuwanunua wasimamizi wa upigaji kura.
Kinachoendele Dom ni mikutano ya kibiashara tu..
Wamejikita kwenye ufisadi wakusanye pesa za kuwapa ushindi.
Inatia kichefu chefu.
 
Huyo Katare alikuwepo katika kampeni B/muro na mbona sisieeemu wakavuna ushindi?Nenda muendako hawa jamaa ndio waongoza nchi tuu mtabaki kutosaini daftari ya matokeo halafu ndio nini?!

Majibu ya jazba yanakushushia mtu hadhi na mleta mada hii nadhani hakuiweka vyema maana CUF Bukomba kuwepo bungeni ni haki sema style ya kutangazwa kwamba wapo ndiyo inazua maswali .Mimi nimesha fika Dodoma pale Bungeni mara 4 kwa kuonana na waheshimiwa wa CCM na Chadema lakini sikuwahi kusema niombe wala kuwaza kutangazwa kwamba nimekuja kwa ajili mtu fulani .Mtizamo tu huo na sijaona faida yake .Mle mjenoni nimekaa sana na mara kibao lakini hata kujulikana niko mjengoni sijawahi kutaka .

Mleta mada alitakuwa ku save muda wetu tujadili hoja za maana hii si hoja .

Kusema CUF ndiyo cha kiongozi nakubali kwamba ni Chama kiongozi Visiwani lakini Bara CUF hailkubaliki hata mara moja .Kukandia kwamba Chadema wanakataa usaini daftari ni ujinga huu maana hata CUF hawajawahi kusaini walipo ibiwa na kupiorwa ushindi na hata leo wanalia na muafaka .

Jamani fikirieni acheni jazba .

Lazima tukubali kwamba Bara Chama pekee ni Chadema na CC na Visiwani ni CUF na CCM .
 
Huyo Katare alikuwepo katika kampeni B/muro na mbona sisieeemu wakavuna ushindi?Nenda muendako hawa jamaa ndio waongoza nchi tuu mtabaki kutosaini daftari ya matokeo halafu ndio nini?!

Kazi ya CCM ni kubaka ushindi wa wengine, na kujitangazia ,wameisha kama mchuuzi wa makongoro hawana hadhi kabisa , even among themselves ni majungu kulalamikiana tuu , kushitakiana wako total confused siku za enda mbio mwisho wao waja
 
Kile ni chuma cha moto...hao vijana ni sawa na DEBE SHINDA....na daima MBIO ZA SAKAFUNI....., tu usubiri mwisho wa mziki wenyewe.
 
Amosam naamini kuna siku utaujua ukweli, labda nawe kama ni kama wao. Hata hivyo wewe si mmoja wao kwani ,hawamo humu.
Pole ,hata kama hukuona yaliyotokea bmlo, na bado unafikiri miaka ya 95.
 
hiyo ni njaa tu inawasumbua si unajua tena uchaguzi umekaribi wale waliozoea kuisha kwa kutegemea si hasa ndio wakati wao huu.Mageuzi ya kweli yatatokea pale wananchi wote kwa pamoja watakapoacha unafiki na kutanguliza maslahi ya nchi mbele na sio maslahi binafsi.
 
Juzi Mwenyekiti wako Freeman Mbowe alitambulishwa bungeni na Spika akiwa ni mgeni wa Dr Slaa. Je Chadema na wanaiga tabaia ya CCM?

Juzi Mwenyekiti wako Freeman Mbowe alitambulishwa bungeni na Spika akiwa ni mgeni wa Dr Slaa. Je Chadema na wanaiga tabaia ya CCM?
Mkuu Masatu,

Kwa kuwakamata wanafiki na wewe ni bingwa. Lunyungu anaimba tu ya CCM, haoni ya CHADEMA, kawa kipofu!
 
Huyo Katare alikuwepo katika kampeni B/muro na mbona sisieeemu wakavuna ushindi?Nenda muendako hawa jamaa ndio waongoza nchi tuu mtabaki kutosaini daftari ya matokeo halafu ndio nini?!
wacha weee wakavuna ushindi kwa kura zinazosemekana za wizi.Kazi ipo! hapa najua mkuu kibunango atanishukia tu
 
Mkuu Masatu,

Kwa kuwakamata wanafiki na wewe ni bingwa. Lunyungu anaimba tu ya CCM, haoni ya CHADEMA, kawa kipofu!

Mkuu,

Kwa akina Lunyungu kunya anye kuku tu... bata anaharisha!
 
Mwiba.
Mgombea ubunge kwa CUF huko Mbeya vijijini amenunuliwa na Chadema juzi,jee unasema Ndugu Mwiba?
 
juzi mwenyekiti wako freeman mbowe alitambulishwa bungeni na spika akiwa ni mgeni wa dr slaa. Je chadema na wanaiga tabaia ya ccm?

hii sikuiona mkuu wangu.umekuwa kama field masrshal es na kumkoma nyani giradi?
 
Mkuu Masatu,
Kwa kuwakamata wanafiki na wewe ni bingwa. Lunyungu anaimba tu ya CCM, haoni ya CHADEMA, kawa kipofu!

Mkuu Mtanzania kweli unadiriki kumwita Lunyungu mnafiki ? Ndiyo lugha kweli za hapa kwa wanao heshimiana ?
 
Mkuu Mtanzania kweli unadiriki kumwita Lunyungu mnafiki ? Ndiyo lugha kweli za hapa kwa wanao heshimiana ?
Mkuu,

Kwa JF ukiwa mnafika utaitwa mnafiki; tunamkoma nyani giladi mchana kweupe. Hakuna urafiki wala kuheshimiana, JF where we dare to speak openly bila kuambiwa huyu si mwenzetu. Najua Lunyungu hatanyima soda tukionana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…